Don Williams V/S Kenny Rogers

View attachment 825894View attachment 825896
Napenda muziki. Kuanzia reggae, blues, kwaito, hip hop, zouk hadi rhumba kote huko nimepita ila ladha ninayoipata nisikilizapo muziki wa country sijawahi kuipata kwenye muziki mwingine wowote ule. Akili, ubunifu, juhudi, maarifa na utulivu unaotumika katika kuandaa nyimbo za country huzifanya ziwe na upekee wenye kusuuza nafsi na roho lakini pia kuipa akili fursa ya kutafakari na kuchanganua mambo katika upeo wa juu zaidi.

Leo nimemkumbuka gwiji wa muziki huo, hayati Don William. Ile sauti, lile gitaa, yale mashairi huwezi kuvipata popote pale zaidi ya kwenye muziki wa Don William. Nimepitia rekodi zake kuanzia Desperately, I am in love, We got love halafu nikamalizia na I believe in you, hakika sijajutia kuwa shabiki wa huyu jamaa. Kabla sijamvisha taji la ufalme wa muziki wa country masikio yangu yakasikia mdundo murua ikabidi nisubiri kidogo, ulikuwa ni wimbo uliopangiliwa vyema, kila chombo kikisikika kwa uzuri kutoka kwake Kenny Roggers ngoma ikiitwa gambler. halafu ukafuata mfululizo wa nyimbo kutoka kwa fundi huyo kutoka Texas, nikaisikiliza coward of the county kisha Luccile halafu we have got tonight, nikamalizia na lady. Kila kitu kilikuwa sawa sawa yaani very perfect.

Hawa jamaa wawili wana mchango mkubwa katika muziki wa country ila nimeshindwa kujua nani nimpe taji la ufalme wa muziki huu maridadi. Haya wakongwa niambieni nani funsi zaidi ya mwenzake baina ya hawa manguli wawili.

Kama ulikuwa hujui; Wimbo maarufu wa I will always love you kwa mara ya kwanza ulitungwa na kuimbwa na mwanamama Dolly Parton ukiwa katika mahadhi ya country mwaka 1974 ndipo ukaja kurudiwa na mwanamama Witney Houston mwaka 1992. najua Witney aliweka nguvu kubwa sana katika matumizi ya sauti ila ukitaka kuona hisia zinazopaswa kuwekwa kwenye huo wimbo msikilize Dolly Parton.

CC
Copenhagen DN Heci Consigliere mng'ato elmagnifico Mr Miller Nahirat
MBITIYAZA ArD67 Inanambo kilambimkwidu kiumbe kipya bombei_safaya Shepherd kidadari Kyalow


Kwa generation yako unawajua hao

Ila USA Jimmie Rodgers ndio father of country music
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom