Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,903
- 30,243
Wanaukumbi,
Kilichonifanya nimrudishe shujaa huyu wa uhuru wa Tanganyika ambae
wengi hawamjui ni kuwa nimekuta picha yake katika nyaraka zangu.
Hii picha nimekuwanayo kwa zaidi ya miaka 40.
Nimeona itapendeza sana kama hii picha nitaiweka hapa jamvini ili JF
wafurahi.
Kwa haraka haraka nimeokota hapa na pale kutoka kitabu changu mle
ambapo nimemtaja Dome Budohi na kuweka hapa jamvini.
Naamini haya yatatufikirisha lau kama kiduchu kuhusu yale ambayo
hayajulikani katika historia ya nchi yetu.