Dola hatengenezi Mwigulu wala Rais Samia, ni Udumavu wa akili kuendelea kujadili jambo lililoko wazi na linaloelewaka

Nkerejiwa

Senior Member
Feb 25, 2014
146
214
1. Kuna upungufu wa dollar duniani kama ambavyo kila mtu anakiri na hata jarida maarufu la Forbes linakiri katika andiko lao "Africa Becomes A Casualty In The War Against Inflation As Dollars Dry Up." kwamba tatizo lipo na Africa ni mhanga mkuu.

Na kwa upande wetu kama nchi kuna mazingira tunakiri kwamba katika mzunguko wetu na reserve yetu kama nchi tuna makadirio yanayonyesha by November tunahitaji usaidizi wa Dollar hadi Milioni mitano kufuatia athari za maboresho katika sera za fedha za Marekani ambazo ndo zimetufikisha katika hii hatua ya uhitaji.

2. Kitu cha pili tutakubalina ni kwamba; kama ilivyo katika nukuu mwanzoni mwa hili andiko, nafasi yetu kama nchi kuamua dolar ipatikane vipi na kiaje iko limited kwa sababu kadhaa. a) Sababu za ukosefu wa dollar kwa sasa hazitokani na sababu zetu za ndani bali ni zile za nje ambazo kimsingi hatuna uwezo nazo at all.

Dollar hatengenezi Mwigulu, Samia. Dollar ni bidhaa kama bidhaa zingine na muundo wa upatikanaji wake hutegemea dhana ile ile ya kiuchumi ya Demands and Supply ambayo again uwezo wetu wa kui dictate uko limited kama nchi.

3. Tutakubaliana kwamba zile top dollar earning schemes kama uwekezaji na utalii bado zipo katika hatua za kufufuka baada ya kupigwa na matukio makubwa mawili vita na janga la covid ambavyo kwa ujumla wake viliathiri our earnig schemes na zaidi viliathiri hadi muundo wa uchumi wa Dunia ambao kimsingi tunaoumia ni sie nyasi maana wanaogombana ni tembo.


Ni jambo Sahihi Kabisa nampongeza Waziri kwa Kuendelea kushugulikia Changamoto hii ya ulimwengu Mzima ya kuadimika kwa dola DUNIANI kote (sio Tanzania tu)

Tanzania haitengenezi dola, hatuzalishi dola hata noti moja, hatuchimbi dola, hivyo hata iweje lazima watengenezaji ambao ni nchi husika( USA) na mashirika ya nje yaombwe ili yatoe kwenye reserves zao

Hili analofanya Waziri ni Jambo Sahihi na anawambia Watu sahihi

Kuna Wabongo wana Upungufu wa Maarifa Wanadhani dola inaokotwa, wanadhani dola inachimbwa bhulyankulu, Wanadhani dola inalimwa mtwara, Wanadhani dola inapandwa kama Mbegu pale BOT na kuvunwa Kwenye Bureau change, kimsingi itoshe kusema watu hawa ni washamba wengi wao hawajui hata dola inafananaje, Wengi wana Stress za Maisha Wanadhani kucontrol Uchumi wa Nchi ni kama kuongoza michepuko yao( ambayo nayo inawashinda wanaishia kujinyonga daily)

Tuacheni usimbe linapokuja suala la Changamoto za kidunia, Marekani yenyewe wanalia USD Sembuse sisi waomba MUNGU? Kenya hapo kuna shida ya dola Chungu Nzima kutuzidi sisi lakini huwaono raia wao wakipiga makelele mitandaoni kwasababu wanaelewa dola sio pesa ya nchi yao (Wakenya wana Exposure kubwa hawana utoto kwenye mambo serious)

Huu ni ulimbukeni na ushamba wa kukosa exposure, tumwombe Dkt Mwigulu Nchemba Atenge Fungu la Kupeleka Vijana wa Kitanzania nje wakatoe Ushamba Kwanza ndio turudi kuelendelea na Mambo Mengine

Wengine Wenye Chuki Zenu dhidi ya Dkt Mwigulu Nchemba naona mnaendelea kutafuta pakujipozea maumivu, maana kila mlipotegemea anachomoka, linawashuka, Mnapata aibu. Ebu jiulizeni ni mara Ngapi Mmesuka Umbea na Ushamba wenu dhidi ya Waziri Mwigulu na Mkaishia kulamba nyasi?

Chuki zenu hazina mashiko,
nchi hii haingozwi kwa mihemko Jiulizeni mihemko yenu kwa kipindi chote hicho imewasaidia nini? Mabwana zenu wanaowatuma na mnaowapambania wameishia kupata viharusi, na sisi kazi inaendelea, Uchumi unakua, Changamoto zote zinatatuliwa bila kuacha maumivu kwa watu

Dkt Mwigulu Nchemba wewe endelea kuchapa kazi hawa Wasimbe washamba wasiokuwa na EXPOSURE ya mambo tuachie sisi tutadeal nao perpendicular mpaka tuwavue ujinga

Nchi iko katika Muelekeo Sahihi wa kiuchumi,
hakuna kilichosimama, changamoto zipo kila mahali DUNIANI na hapa kwetu zinashugulikiwa kiulaloulalo.
 
MWALIMU NYERERE ANAMALIZA KWA USHAIRI KWENYE KITABU CHAKE.

UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.

Ole wake Tanzania Tusipoisaidia
Niwezalo nimelifanya kushauri na kuonya nimeonya.

tahadhali nimetoa ushauri na kuonya nimeshatoka kitini zaidi nifanye nini.

Namlilia Jaalia atumulikie njia Tanzania ailinde WAOVU wasiishinde.

Amina Tena Amina Amina Tena amina


UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.
MWALIMU JK NYERERE
 
Dollar anatengeneza mzalishaji wa bidhaa na huduma zinazouzwa nje, hivyo wanapaswa kufacilitate uzalishaji wa huduma na bidhaa zinazounjwa nje ili tupate dollar, kama wameshindwa kazi hiyo waseme.

Pia waache kujishtaki ICSID ambapo tukioihwa faini kwa dollar wanaenda kugawana
 
MWALIMU NYERERE ANAMALIZA KWA USHAIRI KWENYE KITABU CHAKE.

UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.

Ole wake Tanzania Tusipoisaidia
Niwezalo nimelifanya kushauri na kuonya nimeonya.

tahadhali nimetoa ushauri na kuonya nimeshatoka kitini zaidi nifanye nini.

Namlilia Jaalia atumulikie njia Tanzania ailinde WAOVU wasiishinde.

Amina Tena Amina Amina Tena amina


UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.
MWALIMU JK NYERERE
Naona Mnyambi umekuja na ID fake ujitetee humu.
Wizara imekushinda.Shtuka!
 
Pesa ikiwemo dollar inasaidia katika kibadilishana bidhaa au huduma (thamani huwekwa katika fedha/pesa).
Kitu muhimu au utajiri ni bidhaa au huduma uliyo nayo ambayo wengine wanaihitaji.
Ili upate pesa au dollar kwa wingi ni lazima uzalishe bidhaa au huduma ambayo wengine wanaihitaji sana.
 
Sure, let's blame others!! UPUMBAVU kabisa.

Na kwa bahati mbaya thamani ya fedha inabebwa na imani ya watu katikati serikali yao. Watu wakishapoteza imani, basi hata ukikopa dola milioni 500 kutoka WB watu watazichangamika kuzinunua ili waweke akiba yao kwenye USD.

It happened in Zimbabwe, inaweza kutokea na hapa.
 
Ukichimba Dhahabu au ukinunua dhahabu kwa Tsh, chukua mbegi wako wa dhahabu panda ndege mpaka USA ukikanyaga ardhi ya USA tu unapata mteja haraka sana fast tu anakupa hizo dolla. Unarudi hapa Bongo na mbegi umejaa dolla.
 
Ukichimba Dhahabu au ukinunua dhahabu kwa Tsh, chukua mbegi wako wa dhahabu panda ndege mpaka USA ukikanyaga ardhi ya USA tu unapata mteja haraka sana fast tu anakupa hizo dolla. Unarudi hapa Bongo na mbegi umejaa dolla.
Wapigieni magoti Mafisadi yaliyotoroshea pesa nje ya nchi yazirudishe, ni dollari tupu maana yalizibadili😃😃

CCM na sirikali mtakimbia wenyewe kututawala, muda ni mwalimu.
 
Back
Top Bottom