Alloyce PR
JF-Expert Member
- Nov 15, 2020
- 595
- 714
Kwa Ndugu, Stephen Wasira, na CPA Amos Makala.
Kwa heshima na taadhima, naomba kutoa ushauri huu wa bure kwa viongozi wawili muhimu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Stephen Wasira (Makamu Mwenyekiti wa CCM) na CPA Amos Makala (Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM):
Katika mikutano yenu ya hadhara na majukwaa ya kisiasa, ni vyema kupunguza sana kuzungumzia masuala ya ndani ya CHADEMA, ikiwemo migogoro yao ya ndani, kesi zao mahakamani, au kauli mbiu yao ya kisiasa kama vile “Pasipo Mabadiliko Hakuna Uchaguzi.” Kwa kufanya hivyo, kuna hatari ya kuwaletea umaarufu na nguvu ya maudhui, nyie wenyewe pasipo kujua au pengine mkijua lakini mkadharau athari zake.
Ni wakati sasa kwa CCM kuelekeza nguvu zake katika kunadi sera na ujumbe wa chama cha CCM kwa wananchi. Kama kauli mbiu ya “KAZI NA UTU” ndiyo rasmi, basi ipeni nafasi ya mbele kwa kuielezea kwa kina na kueleza namna inavyogusa maisha ya Watanzania wa kawaida. Kama bado kuna kauli mbiu nyingine mbadala, basi isimamiwe na kuenezwa kikamilifu, mfano, “Oktoba Tuna Tiki” kama ilivyokuwa ikitajwa.
Mwisho kabisa,
Ni muhimu kwa vijana wa UVCCM kuwa hai na makini katika kujibu hoja zinazotolewa na vyama vya upinzani au wananchi mitandaoni na kwenye majukwaa ya kiraia. Tunahitaji vijana, hapa haina budi kuwapa vipaumbele vijana waliokomaa kisiasa na kitaaluma, wanaoweza kuandika na kutoa maudhui yenye majibu thabiti na yenye kueleweka kwa umma juu ya masuala yanayozungumzwa kwenye jamii.
Kwa maneno machache: mzingatie kuonesha nguvu ya CCM kupitia hoja zenu wenyewe badala ya kujenga majukwaa kwa wapinzani. Naomba kuwasilisha. -Alloyce, P.R.