The Mastermind
Senior Member
- Dec 3, 2012
- 107
- 50
Dogo kaingia saluni ya mtaani kwao, kinyozi akamnong'oneza mteja: unamuona huyo dogo anayeingia, ni kilaza na mbulula hakuna mfano.
Booonge ya mjinga. Ziro kabisa. Angalia, ngoja
nikuhakikishie kwamba dogo ni --------.
Kinyozi
akachukua noti ya buku 2 akaweka upande mmoja wa meza na noti ya buku 1 akaweka upande mwingine. Akamuita dogo akamwambia unataka
ipi kati ya hizo noti mbili? Dogo akanyonya kidole, akachukua noti ya buku 1 akaondoka zake.
Kinyozi akamwambia yule mteja, umeona? Mara zote dogo
ndo hivyo hivyo. Hajifunzi kabisa ipi kubwa ipi ndogo. Kilaza. Baadaye yule mteja akaondoka saluni, mtaani
akakutana na yule dogo analamba booonge la ice cream, akamuuliza: hivi kwa nini ulichukua noti ya buku ukaacha ya buku mbili?
Dogo akamjibu: siku nikichukua noti kubwa, yule kinyozi atajua nimeanza
kuwa na akili na mchezo wa kufaidi hela utaisha. Muache aendelee kuniona mbulula nifanye yangu.