Dogo hali anataka kuhama shule na comb

sikuuona ulazima wa kwenda Advance,,,dogo 2 yake iligeuka 3 ndoto ikayeyuka mwisho wa siku akarudi diploma ya CO na anajuta kuupoteza mda wake Advance,,co lazima kwenda moja kwa moja CO,kama anajiamini hatopoteza mda,mtafutie private zipo nyingi tu
 
Mwambie asikule hata mwaka then ataenda kusoma hiyo PCB kwa Mungu.,nyambafu..,anasusa Ugali kwa mambo ya kijinga...ambayo kesho tu yatarekebishika...
 
Sasa atampelekaje wakati anasusa kula????
 
sikuuona ulazima wa kwenda Advance,,,dogo 2 yake iligeuka 3 ndoto ikayeyuka mwisho wa siku akarudi diploma ya CO na anajuta kuupoteza mda wake Advance,,co lazima kwenda moja kwa moja CO,kama anajiamini hatopoteza mda,mtafutie private zipo nyingi tu
Ushaambiwa hataki anasusa kula Amalia siku mzima anataka akasome PCB,sasa na hiyo CO si ndo atalia mwaka mzima
 
nimekuelewa,kwahiyo kuhama shule inaruhusiwa??? mana tulikua hatuna uhakika hapo.
Inaruhusiwa kabisa. Kuna uwezekano wa kwenda wizarani na ukahamishwa juu kwa juu ila kama utaripoti mpaka shule hua wanasema mpaka ukae miezi sita.

Wengi hua tunafeki ugonjwa hivyo hatufikishi miezi sita. Ila kwakua ndugu hapo ishu yake ni kombi kitachofanya awahi kuondoka ni kama shule aliyoenda kombi anayoitaka haipo.

Kama ipo atangoja miezi sita au afanye utapeli
 
nimekuelewa,kwahiyo kuhama shule inaruhusiwa??? mana tulikua hatuna uhakika hapo.
Kuhama aende wapi,kijana mtafutie ujuzi kwa kwenda kusoma Diploma moja kwa moja..huu ni ushauri tu,na wewe usije ukasusa kula na kuanza kulia,maana kawaida dogo hufanya mambo alowahi kufanya kaka/dada ake
 
A level ni kwa ajili ya kupunguza vijana, mimi binafsi sishauri mtu kupitia A level
Kuna vyuo vingi sana vya diploma, piga zako diploma then angalia mambo mengine
Ni kweli, Kama mtu una pesa za kutosha usipitie A level ruka diploma
 
hajasusa,hana appetite kwasababu ya stress. Anahisi ndoto zake zinafifia.
Kwahiyo akisusa ndo ndoto zake zitatimia,na nyie wakubwa ndo mnalea watoto kizembe zembe,Leo hii anaweza tishia kunywa sumu akawaletea matatizo...anasusa unamchekea tuu..we jamaa
 
pesa za kutosha tena?
Yea kwa sababu degree mtu aliyepitia diploma anakua na chansi kubwa ya kukosa mkopo, ambao familia zisizo na pesa za kutosha huuhutaji ili kupunguza makali.
 
Ushaambiwa hataki anasusa kula Amalia siku mzima anataka akasome PCB,sasa na hiyo CO si ndo atalia mwaka mzima
kulia ni dalili ya kuzidiwa maji mwilini tu,hata akilia vipi hawezi kuibadili shule kwa machozi,apo ili aone issue iko serious,hatakiwi kufutwa machozi,ashauliwe kistaarabu tu,kuwa "hii ndo selikari yetu,unatakiwa utumie akili ulioitumia kufaulu ili ikuletee manufaa baadae" wamuache alie tu,kula najua hatomaliza wiki atakua kajitambua tayari
 
kweli kama ukifanikiwa kapata chuo cha science itakuwa vizuri sana kwenye ajira iyo 5&6 aje kupata 2 au 1ya mwisho no mkopo anarudi tena kwenye diploma ndo ada zinagusika kidogo mwambie kuna njia nyingi zakutimiza ndoto
 
asante mkuu,akimaliza hiyo diploma si ataweza tu kuendelea na chuo kama kawaida au hairuhusiwi?
Ndiyo mkuu...tena kama anataka kuwa daktari diploma ndo njia nzuri ya kupitia kuliko hata form six...form six wanaobahatika kwenda kusoma course za afya wanakuwaga wachache mno
 
Kama hakupangiwa hiyo combination bhasi sifa za kusoma hiyo combination hana.Tatizo vijana wengi wanapenda sifa za kusoma advance afu combination pcb..

Namuona mdogo ako akiililia zero au four ya mwisho kabisa,Serikali wamejua uwezo wake ndo mana hawakumpangia pcb,

Mshauri dogo asifosi,kama una uwezo mpeleke chuo chochote cha Afya,
 
Kama shule aliyochaguliwa ina PCB sio kesi akifika atawaambia wamtambadilisha but kama atakidhi vigezo vya matokeo yake ya form 4 so make sure anaenda na result slip.
Na kama shule haina PCB wahini kutuma maombi wizarani abadilishiwe shule but hapa kuna hitaji refa sio unapeleka kibarua chako mimi kuna mzee mstaafu alinimalizia msala hapo nasema hivi coz kuna watu nilikutana nao shuleni walishindwa kubadilishiwa licha ya maombi kutumwa wizarani.
 
hajasusa,hana appetite kwasababu ya stress. Anahisi ndoto zake zinafifia.
Mwambie kitaa tupo kibao ambao ndoto zetu zimepotea, ila bado tunadunda vizuri. Mwambie ndoto za maisha za Mwisho kabisa ni kujua jinsi unavyoweza kutafuta na kupata fedha.
 
Inawezekana kuhama Lakini kubadilisha combination itakuwa ngumu!!
Kwa mawazo yangu
Kuhama combie ni rahisi as long hyo shule ina PCB...ana switch tu hapo hapo shule
kuhama shule haswa boarding to boarding ndio kazi sana...angalau boarding to day
 
long process.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…