Dodoma yazingirwa, BAVICHA wawindwa

Dodoma yazingirwa, BAVICHA wawindwa

Hivi vitu vinahitaji askari kanzu sanasana na si kutumia resource yote ile,
askari kanzu ndo atainfiltrate kikundi kinachoelekea kuleta shida,atajua mipango yao kisha atawatonya hao wavaa uniform

Ndivyo majeshi ya usalama yanvyofanya kazi na siyo mbwembwe na vitisho.
 
kijani ktk ubora wake.
Hata useme nn siku zote huwez kumlazimisha mtu awe chama unachoshabikia.
Upinzani unauhumuhimu wake, kwan kijan hawanywi viroba?
Yule wazir aliyetumbuliwa bungen alikuwa amekunywa maji?

Wewe ongea sana
Kama mwanaume vaa hilo linguo la Wanywa Viroba
Upitenalo Dodoma
 
Safi sana jeshi la polisi. Mmeonyesha mfano. Hivi ndivyo tunavyotaka mfanye: Yaani mtimize wajibu wenu wa kulinda amani na usalama na kuviacha vyama vya siasa kufanya shughuli zao za siasa. Hii ndiyo ile "neutrality" ambayo watanzania wanataka kuiona badala ya jeshi la polisi kupiga marufuku mikutano na shughuli nyingine za vyama. Hongereni.
 
Polisi leo wamezua taharuki kwa watu wa Dodoma Baada ya kuanza kufanya zoezi la utayari ili kukabiliana na vurugu na kuonyesha kuwa wako imara na yeyote atakayefanya vurugu atashughulikiwa.

Chanzo :ITV
 
Wale vijana waliopanga kwenda dodoma kuwasaidia polisi nawasihi wasithubutu kwenda kwa sababu mbalimbali
1. Wao si polisi
2. Polisi walioko dodoma wanatosha na hawataki msaada wao .
 
Jeshi la polisi limefanya zoezi kwa kuandamana barabarani kama ishara ya kutoa vitisho kwa bavicha wasijaribu kuja kuwasaidia kusimamisha mkutano wa ccm.
 
wacha movie iendelee siye watazamaji tuuu.

Tutatoa reviews movie ikiisha.

Ila wakumbuke wataacha legacy gani ten years to come wasiangalie leo.

Last ten years Bush was the shit duniani ukiongea jina Bush kila mtu anatetemeka.

Ila leo anaonekana kama ni mpuuzi flani yani hamna kitu alicho'accomplish duniani.

Wakumbuke kuna maisha ya baadaye.
 
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma leo limefanya mazoezi ya utayari wa kukabiliana na uvunjifu wa amani mkoani humo. Mazoezi hayo yaliongozwa na Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma,Kamanda Lazaro Mambosasa.

Polisi hao waliokuwa kwenye pikipiki,magari ya kutosha na vikosi vya miguu na mbwa walizunguka mitaa mbalimbali ya Dodoma. Kamanda Mambosasa ametoa onyo kali kwa wanaotaka kuvunja amani.

Pia,amekwepa kuyahusisha mazoezi hayo ya utayari na mkutano mkuu maalum wa CCM utakaofanyika tarehe 23 mwezi huu mkoani Dodoma. Amewataka wanaotaka kujua yahusuyo CCM wawasiliane na viongozi wa CCM kwakuwa yeye si Msemaji wa chama hicho.
 
Hii ni aibu kabisa. Kwahiyo wanawaambia vijana wa BAVICHA kwamba wakitia timu dodoma wanatakutana na kichapo kikali? Sikuelewa walikuwa na maana gani
 
Kwakweli nimeangalia mpaka NIKASHANGAA na kujiuliza maswali mengi ambayo yalikosa majibu kabisa .
 
Kupoteza gharama bila sababu yyte,wangewaacha watu wakafanya mikutano yao haya yote yasingekuwepo kwa namna yyte,kweli serikali ya mizuka
 
Hivi hao ukawa tuliwachagua ili wakazuie mikutano ya ccm?? Ama kweli naijutia kura yangu alooooo!
 
Back
Top Bottom