Dodoma yazingirwa, BAVICHA wawindwa

Dodoma yazingirwa, BAVICHA wawindwa

Nadhani serikali ikubali tu kuwa imekosea kuvuruga katiba kwa kuzuia mikutano ya kisiasa wakati yenyewe ikifanya siasa. Haya yanayofanyika sasa dunia nzima inaona na serikali ijue huo udikteta inaoutangaza yenyewe kwa kufanya mambo bila kutulia. Hivi mikutano ya siasa inaweza kumzuiaje Magufuli kutekeleza ahadi zake? Hivi serikali haijui kuwa upinzani ndio kioo chake cha kuisaidia kujirekebisha? Hakuna popote duniani watu wanaweza kuwa na mawazo au imani moja. Mbona dini ziko nyingi na kila dini au waumini wanafanya shughuli zao za kidini kwa kufuata misingi na imani zao. Je nani anaweza kulazimisha watu kuwa waumini wa dini fulani nao wakakubali? Na mbona watu wanaendelea na imani zao bila kusababisha uvunjifu wa amani kama intelijensia ya polisi inavyosema? Na kwanini katika siasa watu wasiachwe waendelee na vyama vyao kama dini zilivyo kwa kuzingatia sera na miongozo ya vyama vyao? Nadhani polisi neno intelijensia hawalijui vizuri na wanalitumia out of context kuzuia watu kufanya shughuli zao za kisiasa na kijamii. Sasa CCM wanakwenda kufanya shughuli za kisiasa ambazo jeshi la polisi limezuia Sasa watoe maelezo huo mkutano wa CCM unatofauti gani na mahafali ya wanafunzi wa vyuo vikuu wa chaso au na mikutano ya CHADEMA? Je wa kwao ni wa kidini? Ni dini gani? Aibu tupu nchi inafanywa ionekane ya hovyo kutokana na maamuzi ya watu wachache wasio kuwa na busara na hekima. Kitabu kitakatifu kinasema heri masikini mjinga kuliko mfalme mpu.mba.vu
 
BAVICHA taifa jingine!. Polisi waumie busara zaidi ya mabavu kwa sababu mwisho wa siku watajikkuta wanawamwagia washawasha hao hao wanaowasaidia kuvunja amri yao bila hata huyo BAVICHA kumwona!.


Polisi wasianzishe vita wasivyoviweza. Ninashauri watumie busara.

View attachment 365536

MJI wa Dodoma umezingirwa na Jeshi la Polisi. Gari la maji ya kuwasha na yaliyobeba polisi muda huu ndiyo yanayoonekana kwa wingi kwenye maeneo mbalimbali tofauti na ilivyo kawaida,anaandika Dany Tibason.

Polisi wanaonekana kuwa tayari kwa lolote, wamejaa kwenye magari yao huku wakizunguka maeneo mbalimbali ya Mji wa Dodoma sambamba na gari la maji ya kuwasha ili kukabiliana na kile kinachojulikana kuwa ni vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA (BAVICHA).

BAVICHA wamedhamiria kuzuia mkutano huo uliolenga kukabidhiwa uenyekiti wa CCM kwa Dk. John Magufuli kutoka kwa mwenyekiti wa sasa, Dk. Jakaya Kikwete.

Awali, Jeshi la Polisi lilipiga marufuku mikutano yote ya hadhara na ya ndani ya vyama vya siasa, hali ambayo imeathiri mikutano ya CHADEMA hivyo BAVICHA kudhamiria mkutano wa CCM kutofanyika. Marufuku ya mikutano ya kisiasa ilianza kutolewa na Rais Magufuli.

Kutokana na dhamira hiyo, UVCCM walionya mkutano wao kutoingiliwa na yoyote, hata hivyo Jeshi la Polisi limeshindwa kuzuia mkutano huo huku wakibadili kauli kwamba, mikutano ya ndani haikuzuiliwa.

BAVICHA wamedhamiria kukutana Dodoma ‘kuisaidia’ polisi kuvuruga mkutano huo, hata hivyo polisi inatetea mkutano huo.

Mjini Dodoma leo, wananchi wamelazimika kusimamisha shughuli zao na kushangaa magari zaidi ya 20 yakiwemo ya kuwasha, magari ya askari wa mbwa na askari wengi wakiwa na sare zao, silaha za moto pamoja na mabomu ya machozi.

Kwa mujibu wa Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma amedai, ni mazoezi ya kawaida ambayo wameamua kuyafanya muda wa mchana badala usiku kama walivyozoea.

Mambosasa amesema, wamelazimika kufanya mazoezi kwa kutumia vifaa vya kipolisi ili wananchi waweze kutambua kuwa, Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma lipo imara zaidi.

Amesema, mazoezi hayo ni sehemu tu ya mazoezi huku akitamba kuwa, Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma lipo imara “na asiwepo mtu yoyote ambaye atajaribu kuingilia kazi za polisi.”

“Wale wote ambao watajipendekeza kwa madai ya kutaka kulisaidia Jeshi la Polisi, watakipata cha mtema kuni,” amesema na kuongeza;

“Hakika nataka kuwaeleza wananchi, asiwepo mtu wa kujaribu kwani tutawakamata na ijulikane wazi kuwa, kuingia rumande ni rahisi lakini kutoka itakuwa ngumu.”

Patrick Ole Sosopi, Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa amesema, kitendo cha Jeshi la Polisi kuzunguka mji mzima kwa kuonesha vifaa vyao vya kivita ni dalili za uoga.

“Kitika kitendo ambacho kimefanya na Jeshi la Polisi ni dalili uoga na inaonesha ni jinsi gani BAVICHA walivyo na nguvu kiasi cha kulitikisa jeshi hadi kufikia hatua ya kufanya vitisho,” amesema Sosopi.
 
ha ha haa na bado povu lishaanza kuwatoka, wasimamie walichosimamia mwanzo.. shame on you
 
Jishaueni kama mmepaka shedo

Mkatize na vifulana vyenu vya lichama la Wanywa Viroba muone
Hahaha
 
police wasiwe na wasiwasi hatutavaa nguo za chama lakini Tutakuwa pamoja kuwasaidia police bila shuruti.

swissme
0678 718216 namba ya mkaka wako ukifika Dodoma. Usipate shida kila kitu umeandaliwa
 
Siku hiz viongoz wetu wanajichanganya sana. Hawasemi kweli.
Ila nashukuru watanzania kwa ss wameelimika wanajua kat ya mbivu na mbichi. Humdanganyi ila anakuvumilia tu
 
Jishaueni kama mmepaka shedo

Mkatize na vifulana vyenu vya lichama la Wanywa Viroba muone
Hahaha
kijani ktk ubora wake.
Hata useme nn siku zote huwez kumlazimisha mtu awe chama unachoshabikia.
Upinzani unauhumuhimu wake, kwan kijan hawanywi viroba?
Yule wazir aliyetumbuliwa bungen alikuwa amekunywa maji?
 
Kwahiyo ukivaa gwanda tu maji mwaaaaa. Mbona watakoma? Kama mbabu kapelekewa gwanda na mjukuuu wake je itakuwaje?
 
police wasiwe na wasiwasi hatutavaa nguo za chama lakini Tutakuwa pamoja kuwasaidia police bila shuruti.

swissme
Dawa ya kufukuza mdudu UKAWA ni Dr Tulia.

Popote ukiona mdudu ukawa pulizia Dr Tulia. Wote watakimbia
 
Hivi vitu vinahitaji askari kanzu sanasana na si kutumia resource yote ile,
askari kanzu ndo atainfiltrate kikundi kinachoelekea kuleta shida,atajua mipango yao kisha atawatonya hao wavaa uniform
Hwawezi kuwa na strategies kama zako Mkuu. Wao ni kukurupuka tu. Dunia ya leo nchi nyingi zinawekeza kwenye intelejensia. Kutafuta habari. Hatoa taarifa wanawezeshwa vilivyo. Mbona hata polisi wasingekuwa na kazi. Wao wazunguka mitaani adui anawaona wale!!! hahahahaah Mambosasa arudi chuo akaijifunze mbinu za kukabiriana na uharifu.
 
Duuu Ccm waogaaa hao Bavicha tu je yangekuwa maandamano ya nchi nzima? Nilishasema Ccm bila Polisi ni weupe kama nywele za Lowassa
 
Back
Top Bottom