Dodoma: Wabunge wadai nyongeza ya Posho na Mishahara yao kwa Hoja Dhaifu

kikwete huna wabunge

Wabunge sio wa Kikwete mkuu.Wabunge ni wetu sisi wananchi tuliowachagua.Ndio maana wanatutumia kama madaraja yao ya kuupandia utajiri!Tazama wanatusingizia sisi wananchi kwamba ni ombaomba.Tunawalilia shida kila siku!Binafsi mbunge wangu hata kwa sura simfahamu.Wanajenga hoja kama watu waliolaaniwa vile.Nauchukia sana huu mhimili<BUNGE>kwa maana umegeuka kuwa ni mhimili kandamizi katika nchi hii.
 
WanaJF hii imekaaje? tangu awali najua msimamo wa chadema ni kupunguza posho za wabunge na hili lilisimamiwa kwa nguvu kubwa na Mbowe na Zitto na wakatofautiana na Shibuka kiasi cha kutupiana maneno ndani na nje ya bunge.

Kujitokeza tena jana kwa mbunge wa chadema Joseph Selasini (Rombo - kilimanjaro) kwamba posho ni ndogo na ziongezwe na zaidi akasema wanaokataa kuongeza posho wana vyanzo vingine vya pato alikuwa anamlenga mbowe na Zitto kwa misimamo yao kuhusu posho. mbowe alirudisha gari la mkuu wa kambi ya upinzani bungeni ili kukoleza msimamo wake

Najiuliza je mzimu wa posho utaigawa chadema? je mbowe na zitto watakuja na kauli gani.
 
tofautisha posho za kujikimu na maposho ya (seating allowance) ndo yasiyo takiwa.
 
chadema wanakula matapishi yao. je kweli chadema wanaweza kusimamia kauli na misimao yao
 
hayo ndio aina ya maneno ya chadema kucheza na lugha punguza posho hii ongeza ile ndio nini sasa
 
Njaaa ni ndio inawagawa CCM naona imeingia na chadema. kuendekeza njaa ndio mwanzo wa ufisadi katika uongozi. viongozi wajifunze kutosheka haina maana kupata faida ya fedha kwenye uongozi
 
Wabunge wetu wapendwa kwanini mstitake kuwa na hummer na majumba ya wabunge majimboni nyie vipi daini bwana
 
kuna jambo linanifurahisha kweli hapa kwa hawa jamaa zangu...upande mmoja wanahubiri kuonyesha serikali imeishiwa au imefilisika but on the other hand wanapigania kuinyonya zaidi hiyo hiyo serikali ambaya wanatuaminisha imefulia. jamani hapa ni hivi, na mapambano yetu yote hayo ya kila siku kuwa maisha ni magumu hawa jamaa wanataka tuendelee kujinyima zaidi tulipe kodi wao wapate pesa ya kuongezewa posho na mishahara. yaani hako kamshahara kenu ka milioni saba na ushee hakatoshi wanataka zaidi. uzuri wa hii stori ni kuwa wamesema watu wa kaskazini so haitakomaliwa sana na hawa makamanda wa cdm,noma angekuwa kasema zitto au shibuda au mwingine yeyote kutoka nje ya huko kaskazini ungesikilizia mziki wake..... oohhhh msaliti na majina mengine meeeeeeeeeengi angepatiwa.
 
SUALA la nyongeza ya maslahi kwa wabunge limeibuka tena safari hii, wabunge wote wakiwamo wa Chadema, wakitaka nyongeza za mshahara na posho. Wakizungumza wakati wa mkutano wa kuelezwa kazi zitakazofanyika katika Mkutano wa Tano wa Bunge ulioanza juzi, wabunge hao walisema mshahara na posho wanazopata ni ndogo na haziwatoshi.

Habari kutoka katika mkutano huo ulioanza baada ya kipindi cha maswali na majibu, zilisema aliyeanzisha hoja hiyo alikuwa Mbunge wa CUF. “Mara baada ya kuzungumzia hilo la posho na tabu wanazopata wabunge wanapotaka kutoa magari bandarini, hoja yake ya nyongeza ya maslahi iliungwa mkono na wabunge wote wakiwamo wa Chadema,” alisema mmoja wa wabunge aliyehudhuria mkutano huo.

Miongoni mwa wabunge wa Chadema waliopingana na kauli ya chama chao ya kupinga nyongeza hiyo katika mikutano ya Bunge iliyopita, ni Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, aliyesema maslahi hayo ni madogo kulinganisha na shughuli za wabunge. Selasini anakaririwa akimwambia Spika, “Mheshimiwa Spika nilivyokuwa nje ya Bunge, nilikuwa nikifikiria tofauti na nilivyokuwa Mbunge, leo naomba Mungu anisamehe, kumbe malipo ya wabunge hayatoshi.” Katika hoja yake, Selasini alieleza kuwa kauli iliyotolewa na Chadema haikuwa msimamo wa chama, bali ni ya mtu binafsi na kubainisha kuwa wanaopinga nyongeza hiyo, wana vyanzo vingine vya mapato tofauti na wenzao akiwamo yeye.

Mbunge mwingine wa Chadema, Mustapha Akunaay (Mbulu), alizungumzia nyongeza hiyo ingawa alionesha wasiwasi wa kutokuwapo usiri kwenye suala hilo na yote yanayozungumzwa kutolewa nje ya kikao hicho. Hata hivyo, Spika Anne Makinda aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, alitaka wabunge wasihofu kuzungumzia maslahi yao na kuwaeleza kuwa suala hilo limeshafikishwa kwenye vyombo husika na linashughulikiwa.

Mshahara wa wabunge ni Sh milioni 2.3 kwa mwezi na pamoja na posho kiwango cha juu anachopokea mbunge kwa mwezi kinafikia Sh milioni saba. Katika mikutano iliyopita ya Bunge hilo, suala la posho liliibuka huku baadhi ya wabunge wa Chadema wakipinga kupokea posho za vikao vya Bunge wakisema zinastahili kupelekwa kwenye miradi ya wananchi.

Hata hivyo, Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, alitofautiana na wabunge wenzake akisema wabunge wanastahili kulipwa posho hizo kwani wanazolipwa sasa Sh 70,000 bado haziwatoshi na badala yake ziongezwe hadi Sh 500,000. Kauli hiyo ilizusha mtafaruku mkubwa ndani ya chama hicho hata kutishia mustakabali wake pale alipolazimika kujadiliwa na Kamati Kuu ya chama hicho kwa ilichokiita utovu wa nidhamu kutofautiana na sera ya chama chake. Shibuda alijiunga Chadema siku chache kabla ya uchaguzi mkuu mwaka jana akitoka CCM ambako alienguliwa katika kura za maoni za ubunge

HabariLeo
 
Kama na wabunge wetu wana tamaa hivyo basi tumekwisha...nani atamwakilisha mnyonge sasa kama hata wale tuliowaamini wamekuwa "chukua chako mapema?"
 
SUALA la nyongeza ya maslahi kwa wabunge limeibuka tena safari hii, wabunge wote wakiwamo wa Chadema, wakitaka nyongeza za mshahara na posho. Wakizungumza wakati wa mkutano wa kuelezwa kazi zitakazofanyika katika Mkutano wa Tano wa Bunge ulioanza juzi, wabunge hao walisema mshahara na posho wanazopata ni ndogo na haziwatoshi.

Habari kutoka katika mkutano huo ulioanza baada ya kipindi cha maswali na majibu, zilisema aliyeanzisha hoja hiyo alikuwa Mbunge wa CUF. "Mara baada ya kuzungumzia hilo la posho na tabu wanazopata wabunge wanapotaka kutoa magari bandarini, hoja yake ya nyongeza ya maslahi iliungwa mkono na wabunge wote wakiwamo wa Chadema," alisema mmoja wa wabunge aliyehudhuria mkutano huo.

Miongoni mwa wabunge wa Chadema waliopingana na kauli ya chama chao ya kupinga nyongeza hiyo katika mikutano ya Bunge iliyopita, ni Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, aliyesema maslahi hayo ni madogo kulinganisha na shughuli za wabunge. Selasini anakaririwa akimwambia Spika, "Mheshimiwa Spika nilivyokuwa nje ya Bunge, nilikuwa nikifikiria tofauti na nilivyokuwa Mbunge, leo naomba Mungu anisamehe, kumbe malipo ya wabunge hayatoshi." Katika hoja yake, Selasini alieleza kuwa kauli iliyotolewa na Chadema haikuwa msimamo wa chama, bali ni ya mtu binafsi na kubainisha kuwa wanaopinga nyongeza hiyo, wana vyanzo vingine vya mapato tofauti na wenzao akiwamo yeye.

Mbunge mwingine wa Chadema, Mustapha Akunaay (Mbulu), alizungumzia nyongeza hiyo ingawa alionesha wasiwasi wa kutokuwapo usiri kwenye suala hilo na yote yanayozungumzwa kutolewa nje ya kikao hicho. Hata hivyo, Spika Anne Makinda aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, alitaka wabunge wasihofu kuzungumzia maslahi yao na kuwaeleza kuwa suala hilo limeshafikishwa kwenye vyombo husika na linashughulikiwa.

Mshahara wa wabunge ni Sh milioni 2.3 kwa mwezi na pamoja na posho kiwango cha juu anachopokea mbunge kwa mwezi kinafikia Sh milioni saba. Katika mikutano iliyopita ya Bunge hilo, suala la posho liliibuka huku baadhi ya wabunge wa Chadema wakipinga kupokea posho za vikao vya Bunge wakisema zinastahili kupelekwa kwenye miradi ya wananchi.

Hata hivyo, Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, alitofautiana na wabunge wenzake akisema wabunge wanastahili kulipwa posho hizo kwani wanazolipwa sasa Sh 70,000 bado haziwatoshi na badala yake ziongezwe hadi Sh 500,000. Kauli hiyo ilizusha mtafaruku mkubwa ndani ya chama hicho hata kutishia mustakabali wake pale alipolazimika kujadiliwa na Kamati Kuu ya chama hicho kwa ilichokiita utovu wa nidhamu kutofautiana na sera ya chama chake. Shibuda alijiunga Chadema siku chache kabla ya uchaguzi mkuu mwaka jana akitoka CCM ambako alienguliwa katika kura za maoni za ubunge

HabariLeo

Wacha walipane vizuri mkuu nchi ikifilisika tutawatafuta tugawane umaskini pia. Hakuna wazalendo nchini mzalendo pekee ni Zitto tu wengineo wachumia tumbo tu.
 
Ni moja ya mambo ya kufedhehesha sana. Hawa watu lazima wadhibitiwe na nguvu ya umma kwani huo nao ni ufisadi. Ndio uwakilishi tuliowatuma? Hivi Selasini anataka michango anayotoa sisi ndio tugharamie? Kaambiwa na nani kuwa mchango ni lazima! Tumbafu kabisa.
 

Imeandikwa na Mwandishi Wetu - Habari Leo, Dodoma; Tarehe: 9th November 2011 @ 23:23



SUALA la nyongeza ya maslahi kwa wabunge limeibuka tena safari hii, wabunge wote wakiwamo wa Chadema, wakitaka nyongeza za mshahara na posho.


Wakizungumza wakati wa mkutano wa kuelezwa kazi zitakazofanyika katika Mkutano wa Tano wa Bunge ulioanza juzi, wabunge hao walisema mshahara na posho wanazopata ni ndogo na haziwatoshi.


Habari kutoka katika mkutano huo ulioanza baada ya kipindi cha maswali na majibu, zilisema aliyeanzisha hoja hiyo alikuwa Mbunge wa CUF.


"Mara baada ya kuzungumzia hilo la posho na tabu wanazopata wabunge wanapotaka kutoa magari bandarini, hoja yake ya nyongeza ya maslahi iliungwa mkono na wabunge wote wakiwamo wa Chadema," alisema mmoja wa wabunge aliyehudhuria mkutano huo.


Miongoni mwa wabunge wa Chadema waliopingana na kauli ya chama chao ya kupinga nyongeza hiyo katika mikutano ya Bunge iliyopita, ni Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, aliyesema maslahi hayo ni madogo kulinganisha na shughuli za wabunge.


Selasini anakaririwa akimwambia Spika, "Mheshimiwa Spika nilivyokuwa nje ya Bunge, nilikuwa nikifikiria tofauti na nilivyokuwa Mbunge, leo naomba Mungu anisamehe, kumbe malipo ya wabunge hayatoshi."


Katika hoja yake, Selasini alieleza kuwa kauli iliyotolewa na Chadema haikuwa msimamo wa chama, bali ni ya mtu binafsi na kubainisha kuwa wanaopinga nyongeza hiyo, wana vyanzo vingine vya mapato tofauti na wenzao akiwamo yeye.


Mbunge mwingine wa Chadema, Mustapha Akunaay (Mbulu), alizungumzia nyongeza hiyo ingawa alionesha wasiwasi wa kutokuwapo usiri kwenye suala hilo na yote yanayozungumzwa kutolewa nje ya kikao hicho.


Hata hivyo, Spika Anne Makinda aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, alitaka wabunge wasihofu kuzungumzia maslahi yao na kuwaeleza kuwa suala hilo limeshafikishwa kwenye vyombo husika na linashughulikiwa.


Mshahara wa wabunge ni Sh milioni 2.3 kwa mwezi na pamoja na posho kiwango cha juu anachopokea mbunge kwa mwezi kinafikia Sh milioni saba.


Katika mikutano iliyopita ya Bunge hilo, suala la posho liliibuka huku baadhi ya wabunge wa Chadema wakipinga kupokea posho za vikao vya Bunge wakisema zinastahili kupelekwa kwenye miradi ya wananchi.


Hata hivyo, Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda, alitofautiana na wabunge wenzake akisema wabunge wanastahili kulipwa posho hizo kwani wanazolipwa sasa Sh 70,000 bado haziwatoshi na badala yake ziongezwe hadi Sh 500,000.


Kauli hiyo ilizusha mtafaruku mkubwa ndani ya chama hicho hata kutishia mustakabali wake pale alipolazimika kujadiliwa na Kamati Kuu ya chama hicho kwa ilichokiita utovu wa nidhamu kutofautiana na sera ya chama chake.


Shibuda alijiunga Chadema siku chache kabla ya uchaguzi mkuu mwaka jana akitoka CCM ambako alienguliwa katika kura za maoni za ubunge.
 
Hizo ni tamaa,kuna tofauti gani na ufisadi mnaojidai kuupinga au ndio unafiki. Je huyu mfanyakazi hasa Mwalimu kwa mwezi anapata kiasi gani?. Haya pambaneni wenyewe huko lakini ipo siku hawa wananchi wanaowapigia kura watawakana kwani huko Bungeni mmepeleka maslahi yenu na siyo ya Wananchi.

Utamu Mtaupata 2015 shibisheni hayo Matumbo kwa sasa...
 
Patriote siku zote hakuna kitu kinanikera mimi kama hii kauli ya Wabunge kwamba wanaitaji nyongeza ya mishahara na posho zao kwasababu wanaporudi majimboni mwao wananchi huwa wanakwenda kuwalilia shida. Ni matusi makubwa kweli kweli wanashindwa tu kusema kuwa wananchi ni omba omba na hilo wala si kweli. Pesa wazopata Wabunge huwa wanasaidia jamaa zao na familia zao, kwa mfano jimbo moja lina takribani watu laki tatu unawasaidia vp na huo mshahara wako kama si kuongopeana.
Mimi naona wajaribu kutafuta sababu zingine lakini sio hiyo ya kila kitu kuwasingizia wagombea wao kwenye majimbo ili hali wabunge wengi wanaishi Dar kula raha kwenye majimbo huwa wanajisogeza kunapokaribia uchaguzi. Ningewaona wana uchungu sana kama wangekuwa wanawatetea wafanya kazi wanaopata laki moja na thelathin kwa mwezi na wana watoto wanaowasomesha kwa mshahara huo, watu hawa hawanunuliwi mafuta, hawana posho, hawana hela ya jimbo. Viongozi wetu wengi tunawachagua bila kutambua kuwa ni vilaza, tukiona mtu anajua kuongea sana basi mawazo yetu tunamuona anatufaa. Ni tofauti na nchi za wenzetu zilizoendelea mtu kuingia kwenye siasa kwanza wewe mwenyewe ujitosheleze kimaisha bila ya kutegemea posho, pindi linapotokea tatizo kwenye jimbo lako basi kabla ya msaada wewe mwenyewe ujue unaanza vp kulitatua.
Tatizo lilianzishwa na wao wenyewe wakati wa kuutafuta ubunge, kwani badala ya kuwaeleza wapiga kura wao wajibu na majukumu ya kibunge wao waliwaahidi mbingu wapiga kura, sasa wanapokumbushwa ahadi zao za uongo wanaanza kulia lia! nyambafu!
 
Inabidi walipwe shs. millioni 80/= kwa mwezi., wanafanya kazi ngumu kweli ya kusinzia kwenye lile jengo.
 
Back
Top Bottom