Dodoma: Wabunge wadai nyongeza ya Posho na Mishahara yao kwa Hoja Dhaifu

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,047
SUALA la maslahi ya wabunge jana liliibuka tena wakati wabunge walipokutana kupewa maelekezo kuhusu mkutano wa tano, huku wabunge wa CCM na wale wa upinzani wakionekana kuwa na kauli moja ya kudai maslahi zaidi. Hivi sasa wabunge wanalipwa mshahara wa Sh2.3 milioni kabla ya kukatwa kodi, kiwango ambacho wanadai hakilingani na kazi wanazofanya na kwamba, kiwango hicho kimepitwa na wakati kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.

1.Hoja: Kiwango cha mshahara tunaolipwa sasa kiliwekwa muda mrefu na inawezekana wakati huo kilikuwa kikitosheleza, lakini kimebakia hapo kwa muda mrefu licha ya watumishi wengine viwango vyao kubadilika, sasa tunadhani ni wakati mwafaka jambo hili kufikiriwa,” alisema mmoja wa wabunge aliyehudhuria kikao hicho.

Maoni yangu: Kama kiwango cha Tsh 2.3M kiliwekwa muda mrefu, je mmewafikiria mwananchi wa kima cha chini ambao toka nchi imepata uhuru hadi leo hajafikia mshahara wa Tsh 130,000/= kwa mwezi???Mnajua kuwa viwango vya nyongeza ya watumishi wa kima cha chini haizidigi Tsh 10,000 kwa ongezeko??Wabunge mna Posho zaid ya mara mbili ya mishahara yenu, mwananchi huyu KCC hana hata Posho moja yaani hata posho ya nauli ya kumfikisha kazini. Hivyo mshahara anaolipwa kwa ajili ya familia yake inabidi atenge nauli ya kwendea kazini. Mnaona ni sawa????Kwanini msimfikirie huyu KCC kuongezewa mshahara na kulipwa posho muhimu????

2. Hoja: “Hapa nina mialiko 26 ya kwenda kuchangia ujenzi wa shule na shughuli nyingine za maendeleo kule Rombo, zote hizi zinanihitaji kama mbunge nitoe fedha, sasa jamani fedha hizi zinatoka wapi,?” chanzo chetu kilimnukuu mbunge huyo akihoji na kuungwa mkono na wabunge wengi. Aidha alisema kuwa wabunge hukutana na kero ya wananchi kuomba fedha ili wakatatue matatizo yao mbalimbali nakwamba ni vigumu kukwepa jukumu hilo kutokana na hali ya maisha ilivyo sasa nchini.

Maoni yangu: Huyu ndo kaungea upupu kabisa na kawadhalilisha wananchi wake wa Rombo. Hivi kweli mbunge unaweza kujenga hoja ya kibabaishaji kama hii?? Wananchi wanahitaji wawezeshwe kuvua samaki sio uwape samaki na kujenga utegemezi kwako. Mambo ya kadi za mialiko yako ni personal issues. Huwezi wataka wananchi watoe kodi zao eti ili wewe uchangie watu wako kitchen party. huu ni upuuzi kabisa.
3. Hoja: Mbunge wa Mbulu (Chadema), Mustafa Akunaay, ambaye alimuunga mkono Selasini akisema malipo ya mbunge hayalingani na wajibu wake kwa umma.

Maoni yangu: Wabunge wengi wanatumia hiki kama kichaka, ni majukumu gani ya bunge mnayotekeleza bila kulipwa Posho nyinyi???Mbona mnalipwa posho hata mkitekeleza majukumu ya msingi ya ajira yenu-Double payment??Ukikaa kikao cha kamati unalipwa posho, Ukikaa kikao cha bunge unalipwa posho, ukitumwa kazi yoyote ya bunge unalipwa posho nono tu, kila kitu ninyi ni posho, ni posho, ni posho. Je mnataka nini zaidi kama sio ulafi na ubinafsi???

4 Hoja:
“Malipo yetu ni kidogo sana, hayatoshelezi kabisa lakini wananchi tunaowawakilisha hawatuelewi katika hili, maana wanadhani tuna fedha nyingi, sasa hapa kuna tatizo. Nadhani kuwapo utaratibu wa kuwaelimisha, wajue hata kazi nyingine tunazofanya siyo wajibu wetu ila tunajitolea na nyingine hizi zina gharama kubwa,” alinukuliwa Lusinde.

Maoni yangu:
kwani unalazimishwa ujitolee??kwa nini usiache???kama kazi si yako na umeamua kuifanya kwa hiari yako kwa kujitolea kwanini unapiga mayowe uongezewe posho kwa kufanya kazi isiyo yako???na anayepaswa kuifanya hiyo kazi yupo wapi hadi umfanyie wewe???je wewe huna kazi zako za kufanya hadi ufanyie wenzako???Je mimi nikimsaidia kazi mzazi wangu nyumbani, nije kuiomba serikali iniongezee mshahara na posho kwa vile nimemsaidia mzee wangu kazi nyumbani???Ujengaji hoja wa aina hii unatia shaka sana, hasa kama utatoka kwa mtu aliyekabidhiwa jukumu zito la kutunga sheria za nchi.


5. Hoja: Spika kwa mujibu wa taarifa hizo naye aliwalaumu baadhi ya wabunge ambao wamekuwa vinara wa kutangaza kuwa maslahi ya wabunge ni makubwa, ilhali wakifahamu fedha hizo ni kidogo hasa ikilinganishwa na wabunge wa nchi jirani.

Maoni yangu: Spika sio kila wanachofanya wenzetu wa nje basi na sisi lazima tuige. Anataka kusema wabunge wa mabunge ya nchi jirani wakitembea uchi basi na wa hapa kwetu nao sharti watembee uchi, bunge la kenya likikataa kupitisha bajeti yao basi na sisi hivyo hivyo. Spika anajifanya hajui kuwa uchumi wa nchi upo dhohofu lihali, Spika anaona productivity yetu na ya wenzetu zipo sawa. Mbona hamjalinganisha viwango vya chini vya mishahara na vya nchi jirani???
Hapa Spika umejitia aibu na kudhalilisha hicho kiti na wale waliokupa hicho kiti mana mnaonekana wote thinking yenu ni ya aina moja. Hivi kweli sababu ya kuongezwa posho na mishahara iwe tu kwa vile wa Kenya wanalipwa zaidi?Naimani mawazo ya namna hii wachunguzi wa mambo ndo wanaiita poor thinking.

WanaJF naomba mawazo yenu je kwa hoja hizi za wabunge wetu wanafaa kuongezewa Posho na Mishahara???Na kama wakijiongezea nini kifanyike ili wote tupandishiwe mishahara na tuanze kupewa posho za msingi km Posho za nauli, nyumba, likizo n.k. mana kama kushuka kwa thamani ya shilingi kumeshuka kwa wote, kama gharama za maisha zimepanda kwa wote na kama kuwajibika nadhani inawezekana wananchi wa chini tunawajibika kuliko wabunge. Naomba kuwasilisha.

Source Mwananchi 09/11/2011
 
Hii thread utadhani imeandikwa kijapani..

Na wabunge wa Chadema nao wataka pesa ziongezwe?
 
wabunge wote waungana kudai posho zaidi. Hii kali kumbe kelele zao ni bure kwenye posho ni wamoja hawana huruma na hali ya nchi. Kikwete unayo kazi hujamaliza tatizo la hali duni ya watumishi serikali wabunge wanakutana na kukesha kuvuna hazina ya fedha ya walipa kodi. kama ni kweli hawa ni wabinafsi bila kujali wanatoka chama gani
 
Patriote siku zote hakuna kitu kinanikera mimi kama hii kauli ya Wabunge kwamba wanaitaji nyongeza ya mishahara na posho zao kwasababu wanaporudi majimboni mwao wananchi huwa wanakwenda kuwalilia shida. Ni matusi makubwa kweli kweli wanashindwa tu kusema kuwa wananchi ni omba omba na hilo wala si kweli. Pesa wazopata Wabunge huwa wanasaidia jamaa zao na familia zao, kwa mfano jimbo moja lina takribani watu laki tatu unawasaidia vp na huo mshahara wako kama si kuongopeana.
Mimi naona wajaribu kutafuta sababu zingine lakini sio hiyo ya kila kitu kuwasingizia wagombea wao kwenye majimbo ili hali wabunge wengi wanaishi Dar kula raha kwenye majimbo huwa wanajisogeza kunapokaribia uchaguzi. Ningewaona wana uchungu sana kama wangekuwa wanawatetea wafanya kazi wanaopata laki moja na thelathin kwa mwezi na wana watoto wanaowasomesha kwa mshahara huo, watu hawa hawanunuliwi mafuta, hawana posho, hawana hela ya jimbo. Viongozi wetu wengi tunawachagua bila kutambua kuwa ni vilaza, tukiona mtu anajua kuongea sana basi mawazo yetu tunamuona anatufaa. Ni tofauti na nchi za wenzetu zilizoendelea mtu kuingia kwenye siasa kwanza wewe mwenyewe ujitosheleze kimaisha bila ya kutegemea posho, pindi linapotokea tatizo kwenye jimbo lako basi kabla ya msaada wewe mwenyewe ujue unaanza vp kulitatua.
 
Hadi tutakapokuwa na Watanzania wengi walio middle class wanasiasa wataendelea kufanya haya wanayoyafanya leo. Sio ajabu sehemu zilizopo nyuma kimaendeleo watu wake ndio wasiotaka/wasioshinikiza mabadiliko maana hawana uelewa.
 
.........kwenye posho wanajilinganisha na wabunge wa nchi jirani, hawakawiii hawa kukubali ushoga ili walipwe zaidi, maana hatukawii kujilinganisha na Uingereza! hovyooooo
 
Wanajf hapa kuna mambo ambayo wananchi kama wananchi hatujawa makini na wengi hawajui kwa nini amchague mbunge.
Nchi nyingine uelewa wa mambo ya kijamii na kisiasa hupo juu sana ndo maana ata wakikubali kujiongezea mishahara na posho watakao pinga au kuandamana wananchi wasio jua watasema ni wajinga na wapinga maendeleo!
Kuna watu au watumishi wanafanyakazi mwaka mzima lakini hana posho ya nyumba,nauri etc na mshahara wake mdogo kama nini.
Kuna msemo huu kuwa POLITICS IS A GROWING INDUSTRY IN POOR COUNTRIES.
 
hao sio wabunge ni wabunge maslahi ni wabunge posho. serikali haijaweza kukidhi mahitaji mengi tu katika sekta nyingine za kijamii wao wanalia posho ndogo wakati kuna wengine hata posho hiyo moja hawapati sambamba na mishahara duni
 
Wabunge wanatumia fedha nyingi wakati wa uchaguzi na wakifika bungeni wanataka kuzirudisha kwa gharama yoyote. wabunge wetu inaonyesha hawajui nini shida ya wananchi.
 
wabunge punguzeni matumizi ili kuisaidia serikali kukidhi mahitaji mengine ya wananchi sio vizuri kujiona kwamba ni nyinyi pekee mko kwenye shida kuliko wananchi wote
 
Du! kazi kweli kweli. Hawa ndio wanaodai jkt iludishwe ili kuleta uzalendo kwa vijana. Uzalendo ni nini kwao? Wao wanazani uzalendo ni kwa vijana wanaoajiriwa kwenda vijijini tu. Wakati wengi wao wakichaguliwa wanaamia ktk 'jimbo kuu la' dar. Nchi iko hoi. Hawa wadau ni usanii tu ktk siasa, hakuna uzalendo hapa. Ni wachache sana kati ya wabunge wetu wenye uchungu wa kweli na hali ngumu kwa wakulima na wafanyakazi wa nchi hii. HI HAIKUBALIKI HATA KIDOGO.
 
Wabunge badala ya kuibana serikali iwajibike kukusanya kodi; kudhibiti wizi wa fedha/mali ya umma; rushwa/ufisadi na kusimamia uwajibikaji ili kupeleka maendeleo kwenye majimbo yao wao wanajipa jukumu la wasaidia wananchi shida zao kwa kuwapa pesa na kuchangia miradi ya maendeleo kwa pesa ya mshahara ili hali wanajua hawatafika mbali kwa kutoa fedha zao za mifukoni! Walivyo na akili fupi wanadhani posho zikiongezwa zitawasaidia kumaliza matatizo katika majimbo yao! Hizo posho hata ziongezwe kwa 100% hazitamaliza shida za hao wananchi wanao waomba misaada! Wala hazitaweza kujenga shule, hospitali na kuleta dawa!
 
Patriote siku zote hakuna kitu kinanikera mimi kama hii kauli ya Wabunge kwamba wanaitaji nyongeza ya mishahara na posho zao kwasababu wanaporudi majimboni mwao wananchi huwa wanakwenda kuwalilia shida. Ni matusi makubwa kweli kweli wanashindwa tu kusema kuwa wananchi ni omba omba na hilo wala si kweli. Pesa wazopata Wabunge huwa wanasaidia jamaa zao na familia zao, kwa mfano jimbo moja lina takribani watu laki tatu unawasaidia vp na huo mshahara wako kama si kuongopeana.
Mimi naona wajaribu kutafuta sababu zingine lakini sio hiyo ya kila kitu kuwasingizia wagombea wao kwenye majimbo ili hali wabunge wengi wanaishi Dar kula raha kwenye majimbo huwa wanajisogeza kunapokaribia uchaguzi. Ningewaona wana uchungu sana kama wangekuwa wanawatetea wafanya kazi wanaopata laki moja na thelathin kwa mwezi na wana watoto wanaowasomesha kwa mshahara huo, watu hawa hawanunuliwi mafuta, hawana posho, hawana hela ya jimbo. Viongozi wetu wengi tunawachagua bila kutambua kuwa ni vilaza, tukiona mtu anajua kuongea sana basi mawazo yetu tunamuona anatufaa. Ni tofauti na nchi za wenzetu zilizoendelea mtu kuingia kwenye siasa kwanza wewe mwenyewe ujitosheleze kimaisha bila ya kutegemea posho, pindi linapotokea tatizo kwenye jimbo lako basi kabla ya msaada wewe mwenyewe ujue unaanza vp kulitatua.
Nadhani tatizo ni kukubali kuongozwa na watu wababaishaji, nafasi za uongozi tumewaachia watu wasio na upeo wa kufikiri vizuri, Pia hatma ya nchi yetu tumeacha iamuliwe na watu wa vijijini wasio na exposure yakutosha-wanainfluence kubwa yakuchagua viongozi bila kujua sifa za viongozi.

Waamerika wakati wa uchaguzi mkuu wanafunzi wa vyuo vikuu walikuwa wanakwenda vijijini kwao kuwaelimisha wanakijiji wenzao juu ya elimu ya uraia na nani anafaa kwa sera zipi na nani hafai kwa sera zipi, in that sense, wengi waliweza kujua kipi pumba na kipi mchele. Zaidi ya hayo its high time sasa wasomi muingie kwenye sisa tuachane na ujengaji hoja dhaifu kama wa Lusinde. Kwa mawazo hayo ya wabunge wetu, tusishangae nchi kuingia kwenye mikataba mibovu mana sometimes nadhani hata lugha ya mikataba hiyo inaweza kuwa kikwazo kwao.
 
Back
Top Bottom