Dodoma: Wabunge wadai nyongeza ya Posho na Mishahara yao kwa Hoja Dhaifu

He, jamani hela ni tamu..! Yaani katika vitu ambavyo unaweza kubet kuwa wabunge watakuwa wamoja ni suala la minoti. Hapa hakuna cha CCM wala upinzani. Wakati mwingine huwa nakuwa sympathetic kwamba pengine na mimi ningekuwa bungeni ningekuwa mroho kama hawa watu. Kitendo cha Zitto kukataa posho peke yake katika bunge lote kinastahili ushujaa wa namna yake (na kwa hili namponeza sana). Lakini hawa wabunge nao wawe wanatumia common sense. Kama gharama za maisha zimepanda zimepanda kote. Ubinafsi huu wa kujitanguliza kabla ya kuangalia maslahi ya watu wengine ni umasikini mbaya sana. Jamaa wanataka kutajirikia bungeni ati? Na hela serikali itatoa wapi?
 
Kama mshahara hautoshi waache kazi wakatafute kazi inayolipa zaidi.
Nadhani hili ndilo sluhisho sahihi, kwa kuwa hakuna kinachowafunga kuendelea na ubunge, waachie ngazi kama alivyofanya Rostam ili tuchague wengine wanaoweza kuwatumikia wananchi katika maslahi hayo duni km wanavyoyaita wao. Kwa kuwa wameamua kuwa kama wafanyakazi, kikawaida mfanyakazi ukiona maslahi unayopata ni madogo, unatafuta green pasture na kuhamia huko unapoona kunalipa zaidi, so milango ipo wazi kwa wabunge kuacha kazi ya ubunge na kusaka well paid jobs of your choice.

After all wabunge wengine ukilinganisha na elimu waliyonayo hawadeserve hata kufungua mdomo, hivi kweli wasingekuwa wabunge, kwa elimu yao ya form four au Darasa la saba wangetegemea Serikali iwalipe hayo mamilioni???
 
Mimi naendelea kusema Nchi hii tunawahitaji wanaharakati zaidi ya tunavyowahitaji wanasiasa, maendeleo na mageuzi ya kweli yataletwav na wanaharakati na si wanasiasa, wanasiasa wa vyama vyote ukiwachunguza kwa makini lao ni moja MATUMBO, yao wao na familia yao. Jamani tuungane watanzania wote kuikataa na kuikemea hii tabia ya kikundi flani cha watu kutaka kuonekana wao ni Miungu watu hapa Tanzania, tukiendelea kuwachekea watatupeleka pabaya hawa....Tufike mahali tukatae vyama vyote na tuungane watanzania kuupindua huu mfumo dhalimu usio na maslai kwa Taifa letu hili changa. Jamani wana siasa wanatupeleka pabaya tusema IMETOSHA.
 
hawa jamaa ni kiboko, ni sawa na kuwa na bakuli lenye nyama tatu, baba anataka kula mbili then mama na watoto wagawane moja - careless dad can do that.
 
Hii Post kama vile umefumaniwa na mkeo?
Si wote wenye hiyo tabia ya kutoka nje ya ndoa zao, so ni better ungefafanua vizuri mtu anayefumaniwa huwa ana behave vipi na wewe umemlink vipi mtu aliyefumaniwa na mke wake na hii thread.

Kwa mawazo ya aina ya Wabunge tulio nao sitashangaa wewe ukiitwa Mhe. Mbunge flani. Sababu sijaona wapi hupaeleweki ktk hii thread. Hii thread hutoielewa tu iwapo wewe ni kati ya hao wanaodai Maslahi bila kuangalia tija ya kazi wanazozifanya.
 
Wabunge badala ya kuibana serikali iwajibike kukusanya kodi; kudhibiti wizi wa fedha/mali ya umma; rushwa/ufisadi na kusimamia uwajibikaji ili kupeleka maendeleo kwenye majimbo yao wao wanajipa jukumu la wasaidia wananchi shida zao kwa kuwapa pesa na kuchangia miradi ya maendeleo kwa pesa ya mshahara ili hali wanajua hawatafika mbali kwa kutoa fedha zao za mifukoni! Walivyo na akili fupi wanadhani posho zikiongezwa zitawasaidia kumaliza matatizo katika majimbo yao! Hizo posho hata ziongezwe kwa 100% hazitamaliza shida za hao wananchi wanao waomba misaada! Wala hazitaweza kujenga shule, hospitali na kuleta dawa!
Kimsingi wabunge wanataka kujenga Taifa la watu tegemezi kwao ili wao waabudiwe na kuonekana kama miungu watu. Hii ni tabia ya kishenzi kabisa na haipaswi kufumbiwa macho hata kidogo. Nionavyo mimi kuwapa hela wananchi kwa kuwa wewe ni mbunge ni kama unatoa rushwa tu
 
Hii thread utadhani imeandikwa kijapani..

Na wabunge wa Chadema nao wataka pesa ziongezwe?


Yani wewe hapo umeona Chadema tu? Chadema ishakua SI unit ya lolote linaloendelea tanzania? mtaweweseka sana
 
Zile fedha za Jimbo ambazo zipo chini ya Mbunge kazi yake ni nini! Naombeni nipite kwanza.
 
Nadhani tatizo ni kukubali kuongozwa na watu wababaishaji, nafasi za uongozi tumewaachia watu wasio na upeo wa kufikiri vizuri, Pia hatma ya nchi yetu tumeacha iamuliwe na watu wa vijijini wasio na exposure yakutosha-wanainfluence kubwa yakuchagua viongozi bila kujua sifa za viongozi.

Waamerika wakati wa uchaguzi mkuu wanafunzi wa vyuo vikuu walikuwa wanakwenda vijijini kwao kuwaelimisha wanakijiji wenzao juu ya elimu ya uraia na nani anafaa kwa sera zipi na nani hafai kwa sera zipi, in that sense, wengi waliweza kujua kipi pumba na kipi mchele. Zaidi ya hayo its high time sasa wasomi muingie kwenye sisa tuachane na ujengaji hoja dhaifu kama wa Lusinde. Kwa mawazo hayo ya wabunge wetu, tusishangae nchi kuingia kwenye mikataba mibovu mana sometimes nadhani hata lugha ya mikataba hiyo inaweza kuwa kikwazo kwao.

Ndugu yangu Patriote, sio kwamba hakuna watu wenye akili and they are grate thinkers in this country ambao wapo kwenye siasa na wanataka kuingiza timu huko waokoe jamii yetu lakini kinachotuuwa sana sana ni ubinafsi wa who knows who na rushwa inayonuka wazi wazi kabisa. Yaani mwananchi yupo teyari kumpigia kura yake zumbukuku mmoja anayetoa elfu kumi kumi kwa wananchi(wenyewe wanaita wekundu mmoja) na yule anayehamasisha wengine anaongezewa kidogo halafu wanachagua mtu ambaye hafai kwenye jamii na kujali maslahi yake na watoto wake.
Hivi kweli mtu mwenye posho ambazo hazisemeki kwa maneno ya kawaida kwa watanzania kwa hali ya sasa pamoja na safari kibao za nje ya nchi wakipewa sijui ndio per diem au outfit allowance kila kukicha na mshahara wa zaidi ya milioni 2 kila mwezi, leo kweli unasimama na wananchi wa kima cha chini wanakuangalia unasema unahitaji nyongeza kweli? kweli kabisa huo ni uwakilishi wa wananchi wako au uwakilishi tumbo lako na familia yako.
Sasa hata kama ukipewa say 5m. kwa mwezi unafikiri kwamba kadi zitakuwa tena 20? na je ni ukweli hizo kadi za michango ya kujenga shule wanachangia zote? na kwa kiasi gani?, mfuko wa mbunge wa jimbo upo wapi? wewe mbunge unafanya nini kuendeleza na kuendeleza jimbo lako, je jimbo litaendelezwa na mishahara minono ya wabunge au fikra zenye tija katika maendeleo?
JE HIZO WANAZOTOA WABUNGE SASA NI HOJA ZA NGUVU AU NGUVU ZA HOJA?
Sielewi kabisa where are we going now days, labda bado ni huu umri wangu, wakubwa niambieni mnaona nini huko mbele? nyie wakubwa ndugu zangu msiniache wakubwa.
 
Jimbo la Rombo lina mahitaji makubwa lakini haihalalishi mbunge wa Rombo kutumia kigezo hicho kuhalalishwa mshahara mkubwa.Je alipogombea aliwaahidi wananchi atakwenda kudai nyongeza ya Mshahara?Jimbo la Rombo linahitaji kilimo ncha umwagiliaji,maji yanastahili kuvutwa kutoka mbali hasa ukanda wa chini

Mbunge aandike project proposals apate fedha kutoka nchi rafiki na mashirika rafiki.Shughuli za maendeleo jimbo la Rombo zinahitaji fundraising ya kutosha strategic.Wanasiasa tufuate ushauri tusiogope kwamba pengine wanaotushauri wana mpango wa kutupindua kwenye majimbo yetu

Sasa sijui hawa wabunge wa chadema wanaodai mishahara wanasimamia wapi.Hapa wanatoka nje ya mstari wa chama.ni kwa nini nyongeza hiyo isielekezwe kwenye mfuko wa jimbo?Huu ni usaliti kwa wananchi,hoja zilizojengwa ni hoja za kijinga na hazina maslahi hata kidogo kwa Wananchi
 
]Kimsingi wabunge wanataka kujenga Taifa la watu tegemezi kwao ili wao waabudiwe na kuonekana kama miungu [/COLOR]watu. Hii ni tabia ya kishenzi kabisa na haipaswi kufumbiwa macho hata kidogo. Nionavyo mimi kuwapa hela wananchi kwa kuwa wewe ni mbunge ni kama unatoa rushwa tu

Mkuu nakuunga mkono katika hili. Hii ndio njia dharimu ya kuwatawala watu maskini ambayo iko hapa nchini. Ndio maana wakati wa kampein utakuta wambunge wanawapelekea watu T-shirt, Kofia, wali etc ili wananchi waone wamesaidiwa ni ushenzi mtupu. Unatakiwa kumjengea mwanachi uwezo wa kujitegemea sio kumsaidia. Mtoa hoja amejitahidi sana kuchambua kila kipengele na utakuta kila mbunge alie toa hoja amekosea. Kama maisha yamepanda wabunge wanapaswa kujadili kwa nini tumefika hapa tulipo na inflation kubwa namna hii na nani awajibishwe katika hili, hatua gani zichukuliwe. Sio kutafuta wingi wa hela. Je wafanyakazi wengine wa serikali itakuwaje?
 
Mda mwingine huwa naona kama hatuna chombo cha kuwawakilisha wananchi serikalini bali chombo cha kuwawakilisha wanachi kwenye vyama vyao. Bunge linashindwa kujenga hoja kuibana serikali juu ya ukali wa maisha, Matumizi a USD katika nchi yetu, Rushwa katika taasisi za serikali kama ilivyo thibitishwa na kamati za bunge na mengine mengi. Wewe unaona posho ndio jambo la kwanza. Sasa anzeni kuongezewa nyinyi baadae tutakuja sisi, polisi, mahakama, jeshi, walimu, etc halafu tuone huo moto kama mtauzima. Ole wenu.
 
Back
Top Bottom