Dodoma: Mwigulu, Serukamba na Nkamia matatani!


Makubwa haya. Tunajua na kuthibitishwa bungeni kuwa JK ni muasisi, mratibu na mkurugenzi mtendaji wa udine. Je imekuwa hivyo pia kwa matusi ya Bungeni?
 
Kwa mtu mwenye akili timamu anaweza kutambua kuwa kitendo wanachotufanyia wabunge sisi watanzania ni mzaha na utani mpaka baadhi ya mawaziri.

Ni mwananchi gani aliyesota kwenye mstari tangu asubuhi atumie demokrasia yake ya kupiga kura halafu ategemee kusikia maneno kama:


1.Siongei na mbwa,naongea na mwenye mbwa
2."....mtoto wa Dr. Slaa ana wiki mbili..."
3."...pumbavu...."
4."....huyu niachieni mimi na mwigulu..."
5.----y you...!
6."....kuna wabunge wana mimba zisizo tarajiwa....." nk.
Najua kuna watu walikuwa wanatumia lugha za picha kumaanisha jambo fulani,ni sawa, lakini kwa hali nchi ilivyo sasa,nadhani wabunge hawa wangejikita kujadili matatizo ya wananchi na nchi kwa ujumla kuliko kuonyeshana ufundi wa kuongea na kushambuliana wao kwa wao.

Pili nilitaka kujua kama wabunge hawa wapotumia muda huu kulumbana kwa matusi,je,majimboni kwao hali ikoje katika mabo haya?
1.barabara
2.elimu
3.afya
4.mfumuko wa bei
5. maji
6.watoto na wazee wenye mazingira magumu nk.
Tatu,kwanini wasijadili hali amani ya nchi,anguko la elimu,mikataba mibovu,ufisadi, utendaji mbovu,mafuriko,nk?
Mawazo yangu,kama hali ni hii ni heri nchi kutokuwa na bunge,na itafutwe namna nyingine ya kujadili na kuendesha nchi kuliko kuwalipa watu kwa kodi zetu ,lakini kazi yao nikuonyeshana ufundi wa matusi.

Aksante.













K
 
nani kakwambia kwamba wana wa mfalme wanaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu??? ni sisi wananchi wapenda mabadiriko tunaoweza kuwachukulia hatua kupitia sanduku la kura! kipindi cha kampeni wakija kuomba kura tunawapokea kwa kelele kama za mbwa anayebweka maana mbunge mwenzao alitamka Bungeni kwamba hawezi kuongea na mbwa bali mwenye mbwa!
 
Hili ndio Bunge la ukweli.....bunge la Ukraine

Nakumbuka hii ni baada ya kiongozi wa upinzani kutoa hotuba yake kwa lugha la ki-Russia. Hilo tu lilitosha kusababaisha ngumi kurushwa ukumbini. Ingekuwa ni upuuzi kama wa akina Chemba nadhani watu wangerushiwa risasi.
 
Landa Filikunjombe lakini naye wameishamkana kuwa sio CCM tena!.
 
Labda Filikunjombe, lakini naye wameisha mkana kuwa sio mwenzao!. MaCCM bwana wanajitenga na ukweli wowote ule.
 
Ngoja tusubiri,lakini napata mashaka kama kweli watafanya hivyo yaani kuwahoji,maana kama lengo ni kujisafisha mble ya watanzania walioshuhudia matusi hayo yakiporomoshwa walitakiwa maspika kuwachukulia hatua za kinidhamu haraka tena hadharani kama walivyowafanyia kina Lissu,kinyume chake wakapotezea leo hata wakijifanya kuwaita kwenye kamati ya siasa bado haitakuwa sabuni ya kuwatakatisha kwa uchafu unaonuka mbele za watanzania.
 
 
Last edited by a moderator:
Nadhani hivyo ni viini macho tu. Lkn hata hivyo hukumu yao yaja si wanadhani wananchi wamewachagua kuoneshana ufahari wa matusi badala ya masuala muhimu ya wananchi. Siku hizi sifa pekee ya promotion ktk chama hicho ni kiasi gani mtu ni bingwa wa kuporomosha matusi kwa wapinzani. Kweli mwovu mti hauzai matunda bora kamwe.
 
Nawaambia waache uwendawazimu! kama ni vikao wawafanyia Mbwa mkubwa na mbwa msaidizi ndio wanaowaachia hao mbwa waliotajwa kwa majina yao kuki-Serukamba chama chao!.
 
 
Last edited by a moderator:
January ,m ametulia sana jamani utafikiri amesomea hekima na busara yani yuko kimya hataki kelele kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…