Dodoma: Mwigulu, Serukamba na Nkamia matatani!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Kuna uwezekano mkubwa Wabunge Mwigulu Nchemba,Peter Serukamba na Juma Nkamia wakahojiwa na Kamati Maalum ya Nidhamu ya Wabunge wa CCM kwa kile kinachosemwa kuwa ni kukichafua chama-CCM. Wabunge hao,kwa nyakati tofauti,wamesikika wakitukana na kutumia lugha ya kuudhi Bungeni. Nani atawagusa watukanaji hawa? Taarifa zaidi zitafuata kadiri zitakavyopatikana. VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam(sasa Dodoma)
 
Last edited by a moderator:
Wakati wamewatuma wenyewe!

Hicho ni kikosi maalum cha kuyumbisha mijadala bungeni, hasa ile yenye mitazamo ya kizalendo
 
Ni uhuni na usanii mtupu mithili ya zile kamati za maulaji ama ni upepo tu kama kauli za mzee mwenye kaya, ndo walivyo wapuuzii hao kutoa uzushi.
 
Migulu Nchemba na Nape wana matatizo vichwani mwao
 

Kazi ya Nchemba hii View attachment 90592
 
Hawawezi kuwachukulia hatua hata kidogo, CCM hakuna wa kumnyooshea kidole mwenzake
 
Hahahahaha! Nkamia Oyeeee! Lameck Oyeeee! Serukamba Oyeee! Jitokezeni wengine msiangushe chama, CCM Oyeeee! CCM tuko vizuri.
 
Chama cha MATUSI kiwahoji WATUSI, haitawahi kutokea asilani, na kama itatokea itakuwa geresha hiyo.
Refer LUSINDE Mtukanaji Arumeru Mashariki.
 
Na kile kibajaj cha Mtela wamekisahau aliyesema kuna wabunge wa mimba zisizotarajiwa.
 

Mkuu VUTA-NKUVUTE, Lusinde Livingstone mbona hayupo kwenye hiyo listi?
 
Wana baraka za Mwenyekiti mwenyewe nani atawahoji? Hiyo ndiyo ile nginjanginja to 2015. Reference Mwenyekigoda mkutano mkuu wa CCM 2012 Dodoma.
 
"In ignorance,a farmer breaks an egg to prove that the embryo is alive"
CCM mnajizika wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…