Dodoma inahitaji mabadiliko ya kifikra | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dodoma inahitaji mabadiliko ya kifikra

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Worshiper, Oct 11, 2012.

 1. T

  The Worshiper JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 301
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dodoma ni moja ya mikoa iliyo nyuma kimaendeleo hapa nchini na haufanani kabisa na jina kubwa ililobebeshwa na serikali ya CCM kwamba ni mji mkuu na makao makuu ya serikali.Mambo mengi bado hayako vile inavyotakiwa kuwa kama Mji mkuu,KWAKIFUPI mambo bado sana bila kusahau ndio mkoa unasifika na unaotoa omba omba wengi hapa nchini.

  Nimekuwa nikifuatilia sana siasa za nchi hii na zaidi hasa hapa Dodoma.Kwa ujumla mambo yote haya yanachangiwa na serikali ya CCM,kwanza kwakutambua udhaifu wa watu wa mji huu (zaidi wenyeji-wagogo na warangi) katika eneo la ukabila.Siasa za ukabila ziko kwa kiwango chakutisha mno, hapa nazungumzia kwa makabila haya mawili,ni ngumu mno tena mno kwa mtu yeyote kutoka nje ya makabila haya kupenya na kushika nafasi kisiasa kuongoza, hapa haupimwi kwa uwezo ama nia thabiti uliyonayo bali kabila ulilonalo.CCM imetumia udhaifu huu kujenga ngome imara vijijini ambako ndiko walipo watu wengi.Na lugha zinazotumika katika kampeni kushawishi ni za makabila hayo.

  CCM pia inatumia ujinga mwingi wa wenyeji wa mkoa huu katika kushinda.Mfano wakati wa kampeni utashuhudia ombaomba wengi (wanajulikana)na vikundi kibao vya ngoma vya akina mama wakiwa wametinga furana na kofia za CCM wakijimwaya kwa nyimbo,ngoma na mapambio wakifurahia shilingi elfu mbili mbili wanazopewa wakiitukuza CCM na kusahau kwa muda shida zao na kuipigia kura ya ushindi.Lakini baada ya kampeni huwa ni kilio na kusaga meno,Ndio kampeni zimeshaisha nguo na elfu mbili mbili watatoa wapi tena ni mpaka baada ya miaka mitano ambapo cha kushangaza huwa wanarudia makosa yaleyale miaka nenda rudi?,ombaomba nao kama kawaida hurejea fani yao nakujaza mitaa tena.Ukweli wengi wa wanaotaka maendeleo na mabadiliko ya kweli ya mkoa huu ni wageni kutoka mikoa mingine na wenyeji walioshika nafasi hakuna chochote wanachofanya.

  Hofu ya kufanya mabadiliko na hali ya mazoea ni tatizo pia miongoni mwa wenyeji wa mkoa huu.Wengi ni waoga wa mabadiliko huku hali mbaya ya umasikini ikiwa imeshamiri miongoni mwao,vijiji vingi vipo katika hali mbaya,huku kila mwaka ahadi zikimiminika.Wengi wao wameshaizoea hali mbaya waliyonayo na wanaona hivyo ndivyo wanavyopaswa kuwa.Wao suala la Dodoma kuwa Makao makuu au kutokuwa kwao sio kitu cha msingi sana,hali na gharama ya maisha kupanda kwa kiwango cha juu kwao si jambo la maana,mji kuwa mchafu,umasikini uliotopea wao ni kawaida,kupungua kwa huduma ya maji huku vijijini ikiwa ndiyo taabu kabisa kwao ni sawa na hakuna haja ya kufanya mabadiliko.
   
 2. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Umenena vyema. Mimi ni mmoja wa makabila haya. Lakini hali ilivyo inatia huruma. Jumapili nikuwa kule Msalato ambako kampeni za udiwani zinaendelea. Yaani inaniuma sana jinsi watu bongo zao zilivyolala. Kila leo wananiomba fedha lakini hawajui kwa nini wao ni masikini na bado wanataka kuchagua tena ccm. Mungu awasaidie tu, Nuru imekuja na wao wamependa giza kuliko Nuru, si Warangi si Wagogo.
   
 3. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono, miongoni mwa mikoa masikini tanzania dodoma upo, nenda kondoa unaweza lia, nenda bahi nk. Ndo maana lusinde alipita kirahis mno. Kiufupi elimu ni shida.
   
 4. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Dodoma ilipaswa kuwa mbali sana kwa sababu iko strategically positioned. Iko kwenye one of the busiest highway in East Africa, kuna reli ya kati. Kuna ofisi nyingi sana za serikali ukiachana na bunge lenyewe. Kuna vyuo ambavyo as we know wanafunzi huwa wanapeleka pesa nyingi sana huko, kwanini bado wana-supply ombaomba kuja Dar? Wanahitaji viongozi wa kuwaonyesha jinsi ya kutumia hizi fursa.
   
 5. B

  Bryson Mbeula Member

  #5
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wakuu kila tatizo lina chanzo,kwa hapa dodoma chanzo hicho ni elimu duni,kwa mkoa mzima utapata shule chache sana za secondary ambazo ni za uhakika...hivyo ni wakazi wa chache sana wanaopata fulsa ya kusoma kiuhakika wakawa revolutionalists,..

  Hali hi pia imesababishwa na watawala wa nchi yetu toka uhuru,CCM imeshindwa kutekeleza sera zake,,na saa zingine ni kwa makusudi kabisa,mfano ni hili la elimu...na ni kwali kuwa ujinga wa wakazi wa mkoa huu ni mtaji mkubwa sana wa kura za CCM,sasa kama ni hivyo kwanini tena iwapelekee elimu?

  Vyama vya upinzani inatakiwa wawe stratergic sana kuweza kuwateka kimawazo watu kama hawa wa dodoma...where is m4c dodoma??mnasubiri 2015,ili mje kushindana na wachonga barabara za muda na wagawa kanga??mtaweza nanyie kugawa hivyo vitu??naamini hamtaweza.

  Hivyo wakati wenu ni sasa...huwa naumia sana kuuona mkoa wangu ukisuasua.
   
 6. M

  Mtoto wa tembo Senior Member

  #6
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli ni watu waliotawaliwa na uoga na ni wagumu kufikiri ya mbele.hakuna kitu kibaya kama uoga,sasa hawa jamaa ndio wametawaliwa na hiyo kitu,alakini kutakua na sababu za kisayansi hebu mwenye uelewa huo ashuke ataufafanulie.NYERERE aliona udhaifu wao akaamua kuwapelekea makao makuu na bunge labda watazinduka kumbe bure kabisa.
   
 7. ABEDNEGO CHARLES

  ABEDNEGO CHARLES JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Mimi ni mwana Dodoma pia,Kwa sehemu nakubaliana na uchambuzi uliotolewa kwanini Dodoma iko nyuma. Hata hivyo, ni km kuna exaggeration ya maelezo kuhusu changamoto zilozoko Dodoma. Kwa wasiojua Dodoma ina makabila haya; Wagogo, Warangi,Waburunge, Wasandawe na Waasi(Wa alagwa). Ni wilaya ya Kondoa tu iliyo na makabila yote niliyoyataja ukiondoa wagogo. Kwa asili, warangi ni waislam kwa 90% kwasababu za kihistoria. Wakristo ni wachache sana. Kwasababu hiyo CUF na CCM ndio wenye mvutano na influence kubwa kisiasa wilayani Kondoa. Kwasababu za kihistoria hizohizo, mwamko wa elimu Kondoa ulichelewa sana. Kwa sasa angalau kuna mabadiliko km ilivyo kote nchini. Key people kutoka Kondoa wamekuwa ni Jaji Damian Lubuva, Balozi Mustafa Nyang'anyi na kwasasa Juma Nkamia nk.
  Wasandawe kwa asili ni primitive sana km historia za bushmen type zilivyo. Hata hivyo wanabadilika. Key people ni km akina Paschal Degera na Severine Supa. Umaskini Kondoa ulichangiwa na ukosefu wa elimu na hali za kijiografia pia.

  Kwa wilaya nyingine kabila la wagogo ni dominant. Na wao wamegawanyika. Jamii za wafugaji ni primitive na aggressive. Hawa msitofautiane kidogo, hawakawii kukugeuza nyama kwa visu. Ni mafundi sana wa kupigana kwa fimbo . Ndio jamii za wagogo walioko machinjioni km kule Pugu. Jamii nyingine za wagogo ni loyal na waoga pia. Elimu Dodoma ilichelewa na waliopata bahati ya kusoma walikuwa wachache na ninachelea kusema walikuwa wabinafsi sana kusaidia wenzao. Hadi leo hii ni kasumba. Hawakuendeleza wenzao na kuleta hamasa ya elimu. Wasomi na watu wenye hadhi kubwa tu kitaifa na wa haja wapo km Mh Dr John Samuel Malecela, kaka yake Balozi Job Lusinde, Mh Captain John Chiligati, Mh Job Ndugai, Prof Manoris Meshack, Prof Paramagamba Kabudi, Prof Gabriel Mwaluko, Prof Msanjila, Mh Gregory Teu, Mh George Simbachawene, na wengine wengi tu.

  Tatizo la wagogo ni kutosaidiana na kutonyanyuana. Wanatakiwa wajifunze kwa wachaga, wahaya na hata wanyakyusa. Wamekuwa wakitumika km dodoki na kuachwa na wanasiasa. Serikali kwa makusudi kabisa, waliacha kujenga barabara zinazoiunganisha Dodoma na Arusha na bado wanasiasa wakongwe wa Dodoma wakakaa kimya kabisa. Huu ulikuwa ni usaliti mkubwa na mbaya sana.

  Tatizo la omba omba haliishi kwasababu za kisiasa tu, sio vinginevyo. Wapo barabarani kimkakati. Hata viongozi wengine wasio wenyeji wa Dodoma wanashindwa kuchukua hatua kwa kuogopa reaction ya wanaowaweka ombaomba hao.

  Hata hivyo, zama za mabadiliko zimefika. Dodoma iliyokuwa CCM damu damu sasa ina madiwani toka CHADEMA. Na kwa hali ilivyo sio ajabu Dodoma mjini ikawa upinzani 2015. Kwangu mimi mabadiliko ni chachu ya maendeleo.

  Mwisho, nimalize kwa kusema Dodoma iko nyuma japo iko kwenye standard za hali za Watanzania wengine pia km ilivyo kwa mikoa yote tu ya Tanzania. Tofauti na too minimal kwa kweli. Potentiality ya Dodoma kubadilika na kuwa mbele ya mikoa mingine ni kubwa sana.
   
 8. josefast

  josefast JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  kuna jamaa yangu alinambiaga dodoma inaifunika moshi mbali sana sijajua hebu ngoja nitafiti kidogo
   
 9. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,936
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  doom ni makao makuu ya chama cha matofali
   
 10. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Fr Severine Andrea Supa si Msandawe, ni mgogo, ila amefanya kazi muda mrefu Ovada, alikofungua shule ya ufundi miaka ile.
  Simbachawene ni Mhehe/Mtiliko.

  Otherwise maelezo mengne yako ok.
   
 11. ABEDNEGO CHARLES

  ABEDNEGO CHARLES JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Matusi dhidi ya kabila lingine si jambo lenye tija no matter wewe na kabila lako mmeendeleaje. Kwanza kwa maendeleo gani mliyonayo Tukuyu? Hakuna watu wanaotukuza kuongea kinyakyusa kama wa Tukuyu. Ukiwa mgeni ni manyanyaso matupu, lugha wanayoijua ni Kinyakyusa tu hadi benki, hospitalini, sokoni, nk

  Lakini pia nikufahamishe tu kuwa maendeleo ni broad na relative term. Maendeleo kwa watu wa Mbeya si lazima yabebe dhana ile ile kwa watu wa Dodoma. Mfano kwa wagogo kutahiri wanawake na wanaume ni jambo la lazima naam ni ''maendeleo'' lakini kwa wanyakyusa hawatahiri wote wanawake na wanaume. Mwanaume kuwa na govi ni maendeleo pia. Ni rahisi mnyakyusa kujisifia asichokuwa nacho. Empty ''compliment'' kwa mnyakyusa ina raise sana ego yake. Kwa mfano yaweza kuonekana ni kejeli kusema Mbeya wameendelea sana kwa 'ukimwi' kuliko Dodoma. How would you view it? Unajivunia hilo? Dodoma wanaweza kuwa maskini lakini si wazinzi hivyo. Ukitaka tuchambue makabila kwa mkabala wa kuangalia negatives unaweza kuhama JF kabisa.

  Mambo ya kipuuzi puuzi yako kote hata Mbeya siyo Mpwapwa tu kama unavyotaka watu waamini. Mbeya kuna dhehebu kila baada ya nyumba tatu. Kila mtu anamwamini Mungu lakini usiku wanachuna watu ngozi na kuzini. Ukitaka kumdanganya mnyakyusa sema unamwamini Mungu hata kama huyo Mungu ni 'mungu' Kama sio upuuzi huo ni nini?

  Nimepokea maoni yako ila nimeitumia haki yangu kukupa kile usichokiona.
   
 12. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  chama cha majina
   
 13. ABEDNEGO CHARLES

  ABEDNEGO CHARLES JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Asante kwa correction. Ni constructive. Bila shaka masomo yanaenda vizuri huko majuu. Ni mimi jembe ulaya wa Kigamboni Dodoma
   
 14. ABEDNEGO CHARLES

  ABEDNEGO CHARLES JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Nyerere hakupeleka makao makuu Dodoma kwa lengo la kuwazindua wenyeji wa Dodoma. Ingekuwa hivyo angeanza na mkoa wa Pwani, Mtwara, Lindi, nk. Bunge lililetwa na Mwinyi.
   
 15. C

  Chiya Chibi JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 485
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nadhan hamuitendei vema Dom. Kipind nyie mnasonga mbele kimaendeleo wao walipatwa na majanga ya ukame ambayo yalileta njaa na magonjwa mbalimbal ikiwemo ukoma na trachoma. Tafuten historia kidogo, msiwatukane watu bure. Vile vile Dom hawazalish zao la maana kutokana na hayo mazingira ambayo kwa sasa kuna uwafadhar kidogo. Siwatetei CCM ila nimekuonyesha tofaut iliyopo huku na huko kwenu, usitukane watu kijana. Karibu Dom
   
 16. K

  KUTATABHETAKULE JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 80
  Sababu ni moja tu, walitoa "ndigwa" na si vinginevyo.
   
 17. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,621
  Likes Received: 16,576
  Trophy Points: 280

  Sidhani kama maoni haya yanajenga hoja sababu upande wangu sijaona matusi kwenye maoni ya wengine ila ulivyochangia wewe kidogo inaleta mushkeli.Inawezekana hata aliyechangia siyo mnyakyusa au anayetokea Mbeya.Ningeomba wana JF tusitumie lugha za kuudhi.AbednegoCharles maoni yako haya yana lugha ya kuudhi,badilisha lugha yako haipendezi hata kidogo.
   
 18. Bartazar

  Bartazar JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 805
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Mkuu yawezekana wewe ni mwenyeji wa Dom kwa hiyo umeguswa negatively na mtoa mada! Nadhani ingekuwa vema kukabiliana na ukweli usoni ili uwe changamoto ya namna ya kutoka hapa tulipo! Nimesoma huu uzi na hakuna sehemu mleta uzi ametukana hata moja! sana sana lugha uliyoitumia wewe ndo yenye mushkeli!
   
 19. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Dodoma ni makao makuu 'kivuli' ya Tanzania. Na mnajua ukishakuwa 'kivuli' inakuwaje. Piga ua ukichunguza sana utakuja kugundua kuwa ukosefu wa sera mahsusi na utendaji mbovu wa serikali yetu uliikosesha Dodoma fursa ya kuendelea kama makao makuu ya nchi. Naamini pia strategic location ya Dodoma ingechochea maendeleo ya mikoa jirani kama serikali isingehadaa watz kuhusu makao yetu makuu. Wana Idodomya pambaneni mtoke.
   
 20. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kuna mtu kasema "wagogo ni watu wenye akili duni sana"
  Hayo si matusi?
  Hiyo post ilikuwa juu hapo asubuhi, na niliiripoti, nadhani imetolewa, na Abednego ame react kwa ajili hiyo.
  Hayo ya Dom kuwa nyuma tunayakubali na kuyatambua, lkn sio kuita kabila fulani lina akili duni!
  Haikubaliki.
   
Loading...