Dodoma: Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete kuzindua Bunge la 10, Nov 2010

HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, AKIFUNGUA RASMI BUNGE JIPYA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

DODOMA, 18 NOVEMBA 2010


Mheshimiwa Spika,

Napenda nianze kwa kukupongeza wewe kwa kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hongera sana!

Hakuna asiyejua kwamba unao ujuzi, uwezo, uzoefu, na umahiri wa kutosha wa kutekeleza majukumu ya Spika wa Bunge letu. Nafarijika sana kwamba sisi katika Chama cha Mapinduzi tumeijengea heshima na kuitengenezea historia nchi yetu kwa kuiwezesha kuwa na Spika mwanamke wa kwanza tangu uhuru. Haukuwa uamuzi rahisi. Lakini tulipoona wamejitokeza wanawake watatu wazito wenye uwezo kushika Uspika kuomba nafasi hiyi kupitia Chama chetu, tukasema fursa ndio hii sasa ya kuondoa dhana kwamba mwanamke hawezi
kukabidhiwa kuongoza mhimili wa dola. Kwa uamuzi huu, tumepiga hatua kujenga fahari ya mwanamke katika nchi yetu na tumeonyesha kwa vitendo kwamba wanawake ni sawa kabisa na wanaume kwa uwezo. Hii sio mara ya kwanza kwa CCM kufanya uamuzi wa aina hii na haitakuwa mara ya mwisho.

Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Samuel Sitta kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuliongoza Bunge la Tisa. Nina imani kabisa kwamba kazi nzuri aliyoifanya itaendelezwa na Spika mpya ambaye alipata fursa ya kufanya kazi chini yake, akiwa Naibu wake, kwa miaka mitano. Binafsi namuahidi Spika wetu mpya ushirikiano wangu, pamoja na ushirikiano wa Serikali yangu nitakayoiunda.

Mheshimiwa Spika,

Napenda pia kutoa pongezi kwenu nyote, Waheshimiwa Wabunge, kwa kuaminiwa na wananchi na kuchaguliwa kuwa wawakilishi wao katika Bunge hili.

Hiyo ni heshima kubwa mliyopewa. Nawatakieni kila la heri mnapojiandaa hivi sasa kuonyesha kuwa kweli mmestahiki heshima hiyo.

Wajibu wa Wapinzani Bungeni

Nawapongeza Wabunge wa vyama vya upinzani. Chama cha Mapinduzi ni chama kikubwa na chenye nguvu kuliko vyote nchini. Ni kazi kubwa kweli kupambana nacho. Hivyo, mnastahili pongezi za pekee kwa kuongeza idadi ya wabunge. Imani yangu ni kwamba wingi wenu tafsiri yake ni dhamana zaidi na mchango zaidi kwenye kusukuma mbele maendeleo ya nchi yetu na sio fursa kubwa zaidi ya kulaumu, kushambulia, kubeza, na kupambana. Watanzania wenzetu wamewachagua wakiamini hali zao za maisha zitabadilika na kuwa bora zaidi. Uhodari wenu hautapimwa kwa kauli kali au kutema cheche hapa Bungeni wala kwa umahiri wa kuainisha matatizo ya nchi yetu. Tutapimwa kwa mchango wetu katika kuboresha hali za maisha ya wapiga kura wetu: wapate huduma ya afya, maji, umeme, barabara, na huduma nyinginezo, na kipato chao kiongezeke. Hilo ndilo wananchi wanalotarajia.

Mheshimiwa Spika,

Serikali ndio inayopanga mipango ya maendeleo na kuitekeleza. Wajibu huo tutautimiza kwa umakini katika kila kona ya nchini yetu, bila kubagua kama wananchi wa eneo fulani wamechagua chama cha upinzani au la. Wananchi wote hata kwenye majimbo ya wapinzani ni watu wa Serikali na wako chini ya utawala wa Serikali. Tunachotegemea kutoka kwenu ni ushirikiano na ushauri kwa Serikali ili tupange mipango hiyo vizuri na kuitekeleza kwa ufanisi.

Sisi katika CCM tunawashukuru ndugu zetu hawa wa vyama vya upinzani kwa kutupa changamoto katika uchaguzi huu ulioisha. Tumejifunza tumeteleza wapi, na tunajipanga kuvirudisha viti tulivyovipoteza na kuongeza vingine zaidi. Tunawashukuru kwamba mmetushtua mapema na kutupa fursa ya kujipanga upya wakati bado tukiwa ni Chama tawala.

Mheshimiwa Spika,

Narudia tena shukrani zangu kwa wananchi kwa kunirejesha mimi na Chama Cha Mapinduzi katika uongozi wa nchi yetu. Maelezo yake ni ya aina tatu tu.
Kwanza, ni kwamba Watanzania wanaienzi na kuithamini rekodi na historia ya Chama chetu katika dhamana ya uongozi wa nchi yetu.
Pili, wameridhika na kazi tuliyoifanya na mafanikio tuliyoyapata katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Na, tatu, wamekubaliana na hoja tulizozitoa kwenye kampeni kote nchini, na wana imani, juu ya mipango yetu ya kukabiliana na changamoto za nchi yetu na kusukuma gurudumu la maendeleo kama tulivyoahidi kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka huu.

Nawashukuru wana-CCM wenzangu wote, kuanzia viongozi wa kitaifa hadi kwenye mashina, na wapenzi na washabiki wa CCM kote nchini kwa kuutafuta na kuuwezesha ushindi tulioupata. Kazi yetu mbele yetu ni kutimiza ahadi zetu kwa Watanzania na kufanya tathmini ya kina ya uchaguzi huu na kujipanga upya, kujiimarisha upya kwa kujenga upya umoja, upendo na mshikamano ndani ya Chama chetu ili tuendelee kukamata dola katika chaguzi zijazo. Mbio za kusaka ushindi wa mwaka 2015 tunazianza sasa.

Mheshimiwa Spika,

Nawashukuru Wabunge kwa uteuzi wangu wa Waziri Mkuu, Mheshimiwa.......... Wengi wenu mnamjua vizuri. Naomba Waheshimiwa Wabunge mumpe ushirikiano mkubwa akiwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni. Naomba pia muwape ushirikiano unaostahili Mawaziri nitakaowateua. Nisaidieni kuwashtua watakapokuwa wanasuasua, lakini pia wapongezeni wakifanya vizuri.






Uchaguzi Umekwisha

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge,

Uchaguzi Mkuu sasa umekwisha. Sasa ni wakati wa kufanya kazi tulizotumwa na wananchi. Wajibu wa wanasiasa wote, ndani na nje ya ukumbi huu, ni kuacha malumbano yasiyokuwa na msingi, ambayo wananchi walio wengi wanaona hayana tija kwao, na kufanya kazi wanazotazamiwa kuzifanya. Nchi yetu ni maskini. Baada ya muda mrefu wa kampeni, wananchi wamekinai malumbano ya kisiasa. Sasa wanataka tufanye kazi ya kumaliza matatizo yanayowakabili na kuwaletea maisha bora.

Bahati nzuri Serikali yangu iliyopita imeweka mazingira mazuri ya kuongeza kasi kwenye safari ya kuelekea kwenye maisha bora. Dhamira yetu, sasa kama ilivyokuwa huko nyuma, ni kuwaletea maisha bora Watanzania. Haijabadilika na haitabadilika. Tumepiga hatua kubwa lakini kwasababu tunaanzia kutokea kiwango cha chini sana cha umaskini, itachukua muda
matunda ya kazi yetu kuanza kuonekana. Lakini lazima tuendelee na safari hiyo kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi.

Vipaumbele 11

Mheshimiwa Spika,

Katika ujumla wake, katika kutekeleza majukumu yake, na katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2010, Serikali nitakayounda itasukumwa na vipaumbele 11:

1. Kuhakikisha kwamba nchi yetu inaendelea kuwa na umoja, amani na usalama, na Muungano wetu unaendelea kuimarika.

2. Kujenga misingi ya uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea kwa kuchukua hatua madhubuti za kuharakisha zaidi mapinduzi ya kilimo, ufugaji, uvuvi na viwanda. Nataka tuanze safari ya kuelekea kuwa taifa la uchumi wa kati, ambalo viwanda ndio mhimili mkuu.

3. Kuongeza jitihada na mipango zaidi ya kuwawezesha kiuchumi wananchi hasa wa hali ya chini, ili waweze kushiriki na kunufaika na uchumi wetu unaokua. Lakini vilevile tutaweka mkazo katika kulitambua na kuliwezesha kwa namna yake kundi la wajasiriamali wa tabaka la kati ili waweze kushiriki katika uwekezaji mkubwa katika nchi yetu.

4. Kutumia fursa ya kijiografia ya nchi yetu kwa kuifanya lango kuu la biashara na usafirishaji kwa nchi za Afrika ya Mashariki, Kusini na Kati, hasa kwa kuimarisha ufanisi wa reli na bandari zetu.

5. Kuongeza jitihada za kuhakikisha Taifa letu linanufaika zaidi na rasilimali za asili za nchi yetu kuanzia madini, misitu, wanyamapori hadi vivutio mbalimbali vya utalii.

6. Kuweka mkazo sasa kwenye kuboresha elimu ya msingi na sekondari, na kupanua elimu ya ufundi na elimu ya juu, hasa katika masomo ya sayansi.

7. Kuongeza jitihada za kupanua na kuboresha huduma muhimu za kijamii hasa huduma za afya na maji, na huduma za kiuchumi hasa umeme, miundombinu ya usafirishaji na mawasiliano na huduma ya fedha.

8. Kuimarisha utawala bora, utawala wa sheria, na demokrasia nchini, hasa kwa kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka, na ubadhirifu wa mali ya umma; na kuendelea kuviwezesha kirasilimali, kitaasisi/kimuundo na kisheria vyombo vya kutoa na kusimamia haki nchini;

9. Kuipa dola na vyombo vyake husika uwezo mkubwa zaidi wa kupanga mipango ya uchumi na kusimamia uchumi wa nchi kwa ufanisi, bila kuingilia sekta binafsi, ili kulinda maslahi ya nchi yetu na watu wake.

10. Kulinda mafanikio tuliyoyapata katika nyanja zote tangu uhuru wa nchi yetu, ikiwemo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, na kukamilisha yale tuliyoyaahidi mwaka 2005 ambayo, kwa sababu moja au nyingine, hatukuweza kuyakamilisha katika miaka hii mitano.

11. Kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri yaliyopo baina ya nchi yetu na majirani zetu, na mataifa mengine duniani, pamoja na taasisi mbalimbali za kimataifa, na kuendelea kutafuta marafiki wapya kwa manufaa ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika,

Amani, Umoja, Ulinzi na Usalama

Katika miaka mitano iliyopita, tumefanikiwa kudumisha amani na utulivu wa nchi yetu na umoja baina ya Watanzania wote na kati ya pande mbili za Muungano wetu. Jukumu la kwanza la Serikali nitakayoiunda ni kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuwa nchi moja, watu wake wanabakia wamoja, na amani na utulivu unaendelea kutawala.

Hatari ya Uchaguzi 2010 kwa Umoja

Naomba nirudie kuelezea kusononeshwa na kusikitishwa kwangu na baadhi ya
viongozi wa dini na wanasiasa waliowataka Watanzania wawachague watu kwa dini zao. Jambo hili linapaswa kukemewa kwa nguvu zote na kila mmoja wetu. Nawaomba viongozi wa kisiasa ambao vitendo hivi vya kibaguzi vilifanywa na vinafanywa kwa niaba yao au kwa kuwanufaisha wao wasikae kimya. Watoe kauli kukemea uovu huu. Hapa nchini Watanzania wenye dini mbalimbali wanafanya kazi pamoja, wanasaidiana, wanashirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii bila kujali dini zao, wanaishi pamoja.

Tusikubali zipandikizwe mbegu za chuki baina ya Watanzania.

Nawapongeza na kuwashukuru Watanzania kwa kukataa kugawanywa kwa misingi ya dini katika uchaguzi huu. Narudia wito wangu kwamba sasa viongozi wote wa siasa, wa dini, wanahabari, viongozi wa kimila, kijamii na wengineo wanaoipenda nchi yetu, tuungane kuziba nyufa na kutibu majeraha yaliyoletwa na uchaguzi huu.


Inaendelea... angalia attachment

(Upuuzi mtupu na uwongo uliokomaa.)

tujadili hii hotuba.
Hii hotuba inaonekana kabisa Kikwete ana hofu na wabunge wa upinzani bungeni, hasa pale anaposema "Imani yangu ni kwamba wingi wenu tafsiri yake ni dhamana zaidi na mchango zaidi kwenye kusukuma mbele maendeleo ya nchi yetu na sio fursa kubwa zaidi ya kulaumu, kushambulia, kubeza, na kupambana. Watanzania wenzetu wamewachagua wakiamini hali zao za maisha zitabadilika na kuwa bora zaidi. Uhodari wenu hautapimwa kwa kauli kali au kutema cheche hapa Bungeni wala kwa umahiri wa kuainisha matatizo ya nchi yetu"

Huu ni ushahidi tosha kuwa anaogopa malalamiko ambayo kwa kiasi kikubwa yana ukweli.
 
wataimarisha mahakama na kuongeza uhuru kwa mahakama.
wataongeza majaji na kuongeza mahakimu
wataboresha mfumo wa kuongeza utawala katika mahakama
 
watahakikisha mrundikano wa wafungwa unatafutiwa dawa, atakutana na wakuu wamagereza kuatua tatizo hilo
 
Wadau, MKOA WA KILIMANJARO UMEME UMEKATWA, DAR PIA NASIKIA UMEKATWA, EBU MIKOA MINGINE TUPENI UPDATE KUHUSU UMEME,
 
Mkulu akiwa kwenye shehere la IDD

Ila naona kama amepungua, ana mawazo ya kuchakachua nini?
 

Attachments

  • Idd-Kikwete.jpg
    Idd-Kikwete.jpg
    15.4 KB · Views: 27
wataimarisha mahakama na kuongeza uhuru kwa mahakama.
wataongeza majaji na kuongeza mahakimu
wataboresha mfumo wa kuongeza utawala katika mahakama

Anaahidi pia kuboresha magereza kwa kuwa watu wanalala mzungu wa nne!
 
Mbona haotuba ya mkuu haina kipya wala cha kujivunia bali nasikia maneno yakupeana matumaini

Mh spika tunagemea
1.kuongeza bajeti ya kilimo......
2.kufungua benki ya kilimo...
Kuanzisha viwanda......

Naahidi kuongeza mishahara ya wafanyakazi....

Tutapambana na rushwa...

Tutanzisha kanda maalum za mifugo

AHADI BADO ZINAENDELEA???????

Mzee ulikuwa hufahamu. Nafikiri umejionea na kusikia mwenyewe. Seif anacheka meno yote thelathini na mbili nje. Ndoa ya CUF na CCM
Wateule wa kula Nje.

Hakuna Jipya Mkuu
 
wataongeza nafasi za wanawake kataika mabaraza ya maamuzi.
watajitahidi wafikie 50-50 ukianzia na mjengoni.
 
Hivi anamalizia au yupo katikati ya hotuba? kuna muda anaonekana kama vile anaconclude halafu anaanza upya!!! maskini sijui nani kamuandalia hii hotuba???? au Vick Kamata
 
wahariri wa vyombo vya habari huwa wakati mwingine wanapewa kabla ila kwa sharti kuwa wasiitoe mpk rais aisome 'embergo'
 
sema makao makuuu yako ya wilaya hayana umeme tuupeleke..... tutasambaza mjini na vijijini tufikie 30% sasa hivi ni 14%

Watu mkinywa maji ya bendera ya chama sijui mnakuwaje? Kwa hiyo MGW 195, zinatosha kusambaza umeme na vijijini? Au hujui maana ya MGW 195? Mijini kwenyewe hadi hivi sasa kuna uhitaji wa zaidi ya megawati 200, na hizo ni zile sehemu za makao makuu ya wilaya na mikoa tu. Bado hujaongelea tarafa, kata na vijiji.
 
When your house is leaking you do not continue building until you take care of the leaking problem. Today the house of Tanzania is reeking of ufisadi. Granted it is not the only problem, it is a major problem and you cannot fix other problems if you ignore corruption and its effects on efforts to bring about development, in education, health, infrastructure, etc.etc. Have you ever wondered why a lot of young people abroad are flocking to join CCM? Because it is a ticket to get rich quick. Ule moyo wa kulitumikia taifa letu aliotuasa Mwalimu Nyerere umeuawa kabisa na tabia za kifisadi. Look at Lowassa! Look at Chenge! Do I need to go on?

I agree. And not only Chenge, Lowassa. The entire Tanzania bureaucracy is reeking corruption. From lowest police officer, to city workers, to wafanyakazi wa wizara ya Ardhi. And Rushwa sio kwa mpokeaji tu, but also to the one who is offering. My point is that the fight against corruption is not only government work, ni kwa kila mTanzania. Kwa sababu, if you live in Tanzania, everybody offer and accept rushwa. And while you are fixing ufisadi, bunge needs to make pro-maendeleo laws and sio kupoteza 5 years discussing rushwa and watu wanashangilia.
 
Wabunge wamechoka yaaani hakuna makofi hata yale yaliyotajwa na MPOTO kwenye ADELA, NAONA anajitahidi kutabasamu ila mmmmmhhhhhhh
 
Back
Top Bottom