ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,114
- 49,840
Dodoma Haina Mpango wa kupoa ππNafasi yenu kwenye list ya mikoa maskini
5. Dodoma
Umaarufu wa mkoa huu hautokani tu na zabibu zake tamu ambazo hutumika kutengeneza aina mbalimbali za mvinyo bali kuhamishiwa kwa shughuli za Serikali kwa kuufanya kuwa makao makuu ya nchi kumeuongezea hadhi na umaarufu zaidi.
Idadi ya watu kwenye mkoa huu uliopo katikati mwa Tanzania si ya kutia shaka, kwani mpaka mwaka 2022 walikuwa na zaidi ya wakazi milioni 3 ambao wastan wa kipato chao kwa mwaka mzima ni Sh1.7 milioni ambacho bado ni cha chini ya wastani wa pato la taifa kwa zaidi ya nusu.
Uchambuzi wa takwimu hizo za NBS unaonesha kuwa ukuaji wa pato la mtu mmoja mmoja uliporomoka kwa asilimia 2.4 mwaka 2022 ukilinganisha na ule wa 2021 ambao ulipanda kiduchu kutoka mwaka 2020.
Huenda ujenzi wa miradi mikubwa ya Serikali kama barabara, miradi ya kilimo, pamoja na reli ya kisasa ikachechemua ukuaji wa uchumi wa wakazi wa mkoa huo jambo litakaloinua pato lao.
View: https://twitter.com/Nnauye_Nape/status/1767449471636345010?t=2dCPaHlS_O8o4TbvtPZr2w&s=19
My Take: Punguza wivu Kwa Dom,bila Serikali kujenga Arusha ingekuwa kama Monduli ππ