figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,890
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani linatarajia kuanza mkutano wake wa kumi na tano siku ya kesho, Aprili 2 huku mkutano huo ukitarajiwa kumalizika tarehe 28 Juni mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Bunge, mkutano huo utakuwa mahsusi kwa ajili ya kujadili utekelezwaji wa bajeti za wizara kwa mwaka wa fedha 2018/19 pamoja na mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20.
Kwenye mkutano huo, wastani wa maswali 515 ya kawaida yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa na serikali huku wastani wa maswali 88 ya papo kwa papo yakitarajiwa kuulizwa kwa waziri mkuu siku za Alhamisi.
Sambamba na maswali hayo pia mkutano huo wa kumi na tano unatarajiwa kujadili hotuba ya hali ya uchumi wa taifa na bajeti ya serikali itakayowasilishwa na wizara ya fedha na mipango.
Miswada miwili ya sheria ya fedha za matumizi ya mwaka 2019 (The Appropriation Bill, 2019) na Muswada wa Sheria ya Fedha mwaka 2019 (The Finance Bill, 2019) pia inatarajiwa kujadiliwa na kupitishwa.