Dodo ya AliKiba: Mapato ya Youtube yamebuma, Shows hakuna, tutegemee ukimya wa muda mrefu

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
1588761182610.png

Hakuna mwanamziki anaependaga kuwa kimya kama wengi tunavyodhani, iwapo msanii hana tatizo za vituo vya redia, n.k basi mara nyingi ukimwya husababishwa na ishu ya "UKATA WA PESA".

Ali kiba ni miongoni mwa wasanii wanaokaa kimya na kusingizia ndivyo walivyo ila ukweli ni kwamba pesa huwa zimekata na kazi za msanii kama alikiba ni gharama sana, kurekodi tu yaweza kuwa milioni na video isipungue milioni 10.

Hakuna jipya katika skendo za uchumi binafsi wa Ali Kiba kwamba aliwahi kukosa pesa za kuwalipa watayarishaji wa muziki (Maprodyuza) kama man walter na abba. Kitendo hiki kilimkasirisha Producer Man water na kuamua kuzifungia nyimbo za Ali Kiba ambazo hazikutoka kwenye stoo yake mpaka pale atakapopata stahiki ya jasho lake, Lilikuwa pigo kubwa kwa Ali, Alikaa kimya muda mrefu.

Kuzorota kwa uchumi kulimtikisa kweli kweli hadi wasanii wa label yake kumkimbia maana palikuwa pakavu pale.

Kwa hii hali ya sasa ambayo hakuna mikusanyiko hivyo shows kukosekana, wasanii wengi wamebaki kutegemea mapato ya youtube ila sasa hawa wengi hata wakigonga views milioni 2 wakapata milioni 3 basi imetosha maana video zao wanafanya hata kwa laki 8.

Ishu inapokuja ni kwa wasanii wakubwa kama kina alikiba, Video tu ya dodo inaweza ikawa imetumika milioni 12 (Usichukulie poa kazi za kiba) ila video imepata views milioni 4 hadi sasa, kwa makadirio ya fasta fasta pesa aliyopokea kutoka youtube kwa video hii ni kama milioni 6 hivi, ndio kwanza kafikia nusu ya gharama alizotengenezea video hii,

Yawezekana kijana alikuwa na mategemeo ya kupata hata robo ya views anazopata mdogo wake, ila kiukweli hali imekuwa tofauti, Kwa hali hii ya mapato kuwa madogo kutokana na views chache ukiunganisha na shows kupigwa marufuku basi msishangazwe kabisa ngoma nyingine itoke mwisho wa mwaka kijana akidunduliza
 
Attachments

  • 1588762322484.png
    1588762322484.png
    40.5 KB · Views: 1
HII ISHU KAMA INAUKWELI HIVI, HAIWEZEKANI WASANII WAWILI WAKIMBIE KWA PAMOJA TENA KATIKA KIPINDI CHA MUDA MFUPI
 
Ila kusema ukweli bila kupepesa macho ngoma yake ya Dodo haina mvuto, haichezeki yaani imepwaya kwaya. Kama asemavyo Baba Lebo, ikipigwa huwezi kujimimina😜
Nashangaa japo kapewa promo na stations radio za bongo kama zote na tv stations tena wengine baada ya lisaa ngoma inapigwa, cha kushangaza kama inavyosema ngoma imevuna.
 
Dodo mbona inafanya poa huku mtaani au kwakuwa mnaona hakuna misheshe kama upande wa pili! Sie mashabiki wake hatupendi show off kama ilivyo kwa king🚶‍♀️
 
u
View attachment 1441463

Hakuna mwanamziki anaependaga kuwa kimya kama wengi tunavyodhani, iwapo msanii hana tatizo za vituo vya redia, n.k basi mara nyingi ukimwya husababishwa na ishu ya "UKATA WA PESA".

Ali kiba ni miongoni mwa wasanii wanaokaa kimya na kusingizia ndivyo walivyo ila ukweli ni kwamba pesa huwa zimekata na kazi za msanii kama alikiba ni gharama sana, kurekodi tu yaweza kuwa milioni na video isipungue milioni 10.

Hakuna jipya katika skendo za uchumi binafsi wa Ali Kiba kwamba aliwahi kukosa pesa za kuwalipa watayarishaji wa muziki (Maprodyuza) kama man walter na abba. Kitendo hiki kilimkasirisha Producer Man water na kuamua kuzifungia nyimbo za Ali Kiba ambazo hazikutoka kwenye stoo yake mpaka pale atakapopata stahiki ya jasho lake, Lilikuwa pigo kubwa kwa Ali, Alikaa kimya muda mrefu.

Kuzorota kwa uchumi kulimtikisa kweli kweli hadi wasanii wa label yake kumkimbia maana palikuwa pakavu pale.

Kwa hii hali ya sasa ambayo hakuna mikusanyiko hivyo shows kukosekana, wasanii wengi wamebaki kutegemea mapato ya youtube ila sasa hawa wengi hata wakigonga views milioni 2 wakapata milioni 3 basi imetosha maana video zao wanafanya hata kwa laki 8.

Ishu inapokuja ni kwa wasanii wakubwa kama kina alikiba, Video tu ya dodo inaweza ikawa imetumika milioni 12 (Usichukulie poa kazi za kiba) ila video imepata views milioni 4 hadi sasa, kwa makadirio ya fasta fasta pesa aliyopokea kutoka youtube kwa video hii ni kama milioni 6 hivi, ndio kwanza kafikia nusu ya gharama alizotengenezea video hii,

Yawezekana kijana alikuwa na mategemeo ya kupata hata robo ya views anazopata mdogo wake, ila kiukweli hali imekuwa tofauti, Kwa hali hii ya mapato kuwa madogo kutokana na views chache ukiunganisha na shows kupigwa marufuku basi msishangazwe kabisa ngoma nyingine itoke mwisho wa mwaka kijana akidunduliza
Kwa kuwa kampapasa shemeji yenu Hamisa ......Na jamaa alishakulaga kabla ya domo wenu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom