DNA ya kimila

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
6,767
2,000
Baadhi ya Wachaga wana utamaduni wa kuwaenzi watoto hasa mzaliwa wa kwanza kwa kuchinja mbuzi baada ya mtoto anapotimiza miezi mitatu kisha mtoto huyo hupakwa damu kwenye paji la uso kwa kutumia Isale.

Inaaminika kuwa kitendo hicho hufanyika kwa lengo la kuondoa mashaka juu ya baba wa mtoto na wengine hufanya hivyo ili kuonesha tofauti ya mtoto wa kwanza na watoto wengine kwani mtoto wa kwanza kupewa heshima na wakati mwingine anakuwa na nguvu ya kufanya maamuzi kuliko watoto wengine.

Kitendo cha kuchinja mbuzi hufanyika kwa lengo la kumkaribisha mtoto kwenye familia husika, kumlinda na mabaya pia kumtakia maisha mema na kumuombea baraka kutoka kwa mababu wa ukoo.

Wachaga wanaamini kwamba ikiwa mtoto aliyepakwa damu sio wa ukoo husika anapatwa na mikosi na misukosuko itakayoashiria si damu ya ukoo husika na kama mama wa mtoto akichelea kutubu mtoto anakufa au kupotea katika mazingira ya kutatanisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom