Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan tarehe 10 Septemba 2021 alimteua Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dkt. Stergomena Tax aliteuliwa katika nafasi za wabunge kumi wanaoteuliwa na Rais. Wakati huo alikuwa amemaliza muda wake kama Katibu Mtendaji wa SADC mwezi Agosti 2021.