Dkt. Slaa atua na kutoa maoni yake kupitia Radio One kuhusu hali ya siasa nchini

Burnaboy

JF-Expert Member
Dec 2, 2019
473
1,000
Dr W. Slaa kaingia Tanzania jana Jumanne 10/03 usiku. Leo amefanya interview kwenye kipindi cha "Kumepambazuka" cha Radio One.

Amezungumza mengi kama vile diplomasia ya uchumi nk ila kuhusu siasa hizi ni dondoo muhimu kwenye interview hiyo:

1. Alijiuzulu siasa za vyama (active party politics). Hajarudi CCM na hategemei kurudi CCM. Si lazima arudi CCM (awe mwanachama) ili alitumikie taifa lake.Yeye kule Sweden hamuwakilishi mwenyekiti wa CCM, anamuwakilisha Rais.

2. Slaa anasema kama wapinzani walishindwa kuiondoa CCM 2015 hawataweza kuiondoa tena. Chama tawala kimebeba na kutekeleza agenda iliyoipa umaarufu upinzani 2015. Anasema upinzani unajenga mawazo chama tawala kinatekeleza. Hakuna kosa kwa chama tawala kuiba mawazo. Vyama vya upinzani vinapewa ruzuku kuwa "Viwanda vya Mawazo" ambayo chama tawala kinayatumia sababu upinzani hawana mahali (platform) ya kutekeleza mawazo yao.

3. Slaa anasema hakuna waraka (decree) unaowazuia wapinzani kuendesha shughuli zao. Serikali haifanyi kazi kwa matamko. Anasema kilichotokea ni kwamba kuna matamko ya upinzani (Chadema) yalileta sura ya kuchafua utulivu (Civil Disobedience). Walisema wataandamana kila kona - mkoa hadi mkoa, kijiji hadi Kijiji, mtaa hadi mtaa. Anasema kwa tafsiri yake, sheria inayotumika kudhibiti shughuli za wapinzani ni ya kipolisi sababu ikifika mahali unakwamisha mambo hauwezi kuachwa.

Anatoa mfano ofisi yake ya ubalozi Sweden ilipokea taarifa ya "Maandamano ya Mange Kimambi." Mamlaka ya Serikali ya Sweden ilitaka maelezo ya kina (details) za waandamanaji ikiwemo majina yao. Mamlaka hiyo ilielekeza idadi yao, sehemu ya kusimama na masharti mengine kama kutotumia vipaza sauti, nk. Anasema hii ni kuonyesha hata kwenye nchi kama Sweden, masharti yapo ili kuepuka kusumbua wananchi. Kati ya wale 100 walioruhusiwa kuandamana ni 6 tu walijitokeza.

Slaa anasema aliwaasa Chadema wajirekebishe kuhusu hili ila wameshindwa. Anasema ukombozi haupatikani kwa "Red Brigade" kuwa barabarani.

Anawaasa wanaotaka kujua Chadema ilipoanza kukosea wasome kitabu chake cha "Nyuma ya Pazia"
 

MVB Jr

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
299
1,000
I really love Dr. Slaa..

Those days he made me feel proud of CDM.

Dr. aliteka moyo wangu sana hasa kwenye umahiri wake wa kujenga hoja.

Nilimpa kura yangu 2010 ingawa sikupiga kwa sbb ya umri.

I reserved my vote for 2015 election, lkn ikawa hivyo tena.

When he resigned siasa za vyama, I resigned also.

Binafsi katika era hii ya siasa za bongo sijaona kama Dr.

All the best my role model.
 

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
702
1,000
CHADEMA hawatakuja tena kupata Secretary General aliye Smart Upstairs, Strategist, Daring na very Brave Politically kama huyu Dkt. Wilborad Slaa. Uwezo wake huu mkubwa ndiyo uliifanya CCM ikose Usingizi 24/7 na sishangai baada ya Yeye kuachana na CHADEMA ndipo nao ( CCM ) wakapumua huku wengine wakimshukuru Mwenyezi Mungu.
 

The iron batterfly

JF-Expert Member
Jul 31, 2018
1,960
2,000
CHADEMA hawatakuja tena kupata Secretary General aliye Smart Upstairs, Strategist, Daring na very Brave Politically kama huyu Dkt. Wilborad Slaa. Uwezo wake huu mkubwa ndiyo uliifanya CCM ikose Usingizi 24/7 na sishangai baada ya Yeye kuachana na CHADEMA ndipo nao ( CCM ) wakapumua huku wengine wakimshukuru Mwenyezi Mungu.
Eti smartDr mihogo huyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kesaboso

JF-Expert Member
Apr 16, 2019
426
500
Alisha shindwa aende zake, mchungaji gani mwenye kujiunga na mbwa mwitu kula kondoo MUNGU na amhukumu sawasawa na mayendo yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Juzi kuna askofu mmoja mnae mwaminia kawambia mjirekebishe, mkamzodoa na matusi wengine, dhambi zitaendelea kuwaandama sana, chama kimetekwa na watoto wasio wajua baba zao, midom yao inanuka na kutoa mapovu hovyo, badilisheni tabia kumbuka tabia ya kitanzania na africa ikoje kabla ya kutoa povu kwa wakubwa. Hilo tu litakuwa na faida kwako.
 

jd41

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,758
2,000
Huyu mzee nilikuwa namkubali sana alipokuwa CHADEMA, ila alikuja kuni prove wrong alipokubali kutumika kwa maslahi ya CCM.

Huyu mzee alikuwa na marafiki Usalama wa Taifa waliokuwa wanampa taarifa nyeti alizokuwa anajidai nazo pindi akiwa Katibu Mkuu CDM, sasa ulipofika wakati wa kulipa fadhila kwa hao jamaa wakamwambia aondoke CHADEMA ili kudhoofisha nguvu ya UKAWA baada ya Lowassa kujiunga.

Ndio maana jamaa wakampa ulinzi kule hotelini alipokwenda kujificha kuogopa usaliti wake, hayo mengine yote anayoongea siku hizi ni kumfurahisha bosi wake tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

jd41

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,758
2,000
Hoja namba moja Dr. Slaa; hawezi kumtofautisha Rais na Mwenyekiti wa CCM, huyo ni mtu mmoja japo ana vyeo tofauti, kusema unamfanyia kazi Rais na sio M/kiti wa CCM ni uongo kwasababu kwenye ufanyaji kazi wake atakuwa analinda interest za M/kiti wa CCM, ambae ndie bosi wa Dr. Slaa; mfano ni pale alipoulizwa maoni yake baada ya Lissu kupigwa risasi, akajibu ili kumfurahisha M/kiti wa CCM ambae ndie bosi wake; alijibu kwamba Lissu sio wa kwanza kupigwa risasi. Hili jibu kimsingi alilenga kumfurahisha M/kiti wa CCM.

Hoja mamba mbili nimeipenda; na hii kina Sabaya na wenzake waisome vizuri, zile kelele zao kwamba wapinzani waoneshe walichofanya leo zimepewa jibu na rafiki yao, kwamba wapinzani hawana mahali pa kutekeleza mawazo yao, hivyo kelele za kina Sabaya na wale "wananchi"' wa Hai hazina maana, wasimsumbue Mbowe.

Hoja namba tatu Slaa kaongea kisiasa; anayajua fika mazingira ya siasa Tanzania, hasa siasa za vyama pinzani, tamko la Rais, ambae ndie M/kiti wa CCM linachukuliwa kama sheria, linatekelezwa na vyombo vya dola. Juzi Bashiru katoka kujisifu kuhusu matumizi ya dola kui-favour CCM, sijui hakusikia hilo, tunamuona Bashiru akizunguka nchi nzima kufanya shughuli za siasa, wakati upinzani hata kufanya mikutano kwenye majimbo yao imekuwa tabu (Sugu), ni Mbatia pekee alieenda Mbeya hivi karibuni tena baada ya kutoka ikulu kwa mazungumzo na Rais.

Mwisho, Dr. Slaa anatoa mfano wa Sweden kwamba watu wakitaka kuandamana wanatakiwa kutoa details zao, atuambie hapa Tanzania wapi waandamanaji walitakiwa kupeleka details zao wakagoma kuzipeleka? Mazingira ya Sweden na hapa kwetu ni tofauti, hilo analijua, anajitoa akili makusudi.

Ile kauli ya "nitawachapa mpaka shangazi zao" aliwahi kuisikia au hakuisikia?
hope alikuwa busy ubalozini!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom