Dkt. Shika kuiaga Tanzania mazima

Dkt. Shika kuiaga Tanzania mazima

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,450
Reaction score
32,291
Dkt. Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za Lugumi, amesema kwamba hivi karibuni anatarajia kwenda kuishi Marekani, baada ya Umoja wa Mataifa kumpandisha cheo.

IMG_0466.JPG

Akizungumza kwenye kipindi cha Weekend Breakfast cha East Africa Radio, Dkt. Shika amesema awali alikuwa anafanya kazi kwenye shirika la Umoja wa Mataifa inlocshughulikia wakimbizi (UNHCR) na sasa amepandishwa cheo, hivyo hata ofisi zake hazitakuwa tena Nairobi nchini Kenya, kwani zitahamishiwa New York Marekani.

"Sasa hivi nina mpango wa kusajili kampuni yangu alafu mimi nisepe, nikiwa hapa nchini nanyanyasika, nilikuwa nafanya kazi na Umoja wa Mataifa Bara la Afrika, sasa ni world wide ofisi itakuwa New York, nimepandishwa cheo, nafaya kazi ofisi ya UNHCR, hata mama Kevela alipogundua mimi ni balozi akasema nyinyi ndio mnaoongoza nchi hii, na watu wajue kuwa uteuzi wangu haukutokea Tanzania, nimeteuliwa kwa veto power, veto power ziko tano kwenye umoja wa mataifa, jina langu lilikuwa projected na Urusi na mwenyewe Putin", amesema Dkt. Shika.

Dkt. Shika ameendelea kwa kusema kwamba kura ambazo alipata zilitosha kwa yeye kuwa balozi wa Umoja wa Mataifa, kwani nchi tatu zilikubali jina lake kupitishwa ikiwemo na Marekani.
 
Singo ya kumalizia mwaka hii[emoji23]
 
Vipi kuhusu nyumba, alishalipia?
Kila la kheri Dr Louis Shika.
 
Dkt. Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za Lugumi, amesema kwamba hivi karibuni anatarajia kwenda kuishi Marekani, baada ya Umoja wa Mataifa kumpandisha cheo.

53652279c3f3db91684c5ff242b323a9.jpg

Akizungumza kwenye kipindi cha Weekend Breakfast cha East Africa Radio, Dkt. Shika amesema awali alikuwa anafanya kazi kwenye shirika la Umoja wa Mataifa inlocshughulikia wakimbizi (UNHCR) na sasa amepandishwa cheo, hivyo hata ofisi zake hazitakuwa tena Nairobi nchini Kenya, kwani zitahamishiwa New York Marekani.

"Sasa hivi nina mpango wa kusajili kampuni yangu alafu mimi nisepe, nikiwa hapa nchini nanyanyasika, nilikuwa nafanya kazi na Umoja wa Mataifa Bara la Afrika, sasa ni world wide ofisi itakuwa New York, nimepandishwa cheo, nafaya kazi ofisi ya UNHCR, hata mama Kevela alipogundua mimi ni balozi akasema nyinyi ndio mnaoongoza nchi hii, na watu wajue kuwa uteuzi wangu haukutokea Tanzania, nimeteuliwa kwa veto power, veto power ziko tano kwenye umoja wa mataifa, jina langu lilikuwa projected na Urusi na mwenyewe Putin", amesema Dkt. Shika.

Dkt. Shika ameendelea kwa kusema kwamba kura ambazo alipata zilitosha kwa yeye kuwa balozi wa Umoja wa Mataifa, kwani nchi tatu zilikubali jina lake kupitishwa ikiwemo na Marekani.

Credit: EATV
 
Huyu wampeleke Milembe tu.

Inanikumbusha theory moja, ni rahisi kuwa maarufu duniani ila ni ngumu sana ku maintain umaarufu. Ndio maana utakuta mtu anapata umaarufu labda kwenye muziki au sinema kisha anashindwa kubaki na umaarufu wa muziki anaanza kupiga picha za uchi au ujinga mwingine ili mradi jina lake liendelee kusemwa semwa
 
Anajiimarisha kwenye kiki zake ameona anaanza kuporomoka
 
Back
Top Bottom