Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,777
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Facebook amesema yupo tayari kuomba silaha kwaajili ya kuilinda Tanzania dhidi ya tishio lolote la usalama na amani kwani aliwahi kufanya hivyo mwaka 1990.
"Mwaka 1990 nikiwa JKT, Chimala, Mbeya, nilikaa miezi 3 nikiwa na bunduki kulinda madaraja ya reli na barabara pale dhidi ya tishio la makaburu wa Afrika Kusini. Leo hii niko tayari kuomba silaha kulinda Taifa langu dhidi ya tishio lolote la usalama na amani ya Tanzania kutoka kwa maadui wa sasa, ambao sisi wengine tunawajua!"