Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,777
Mkurugenzi wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) kupitia ukurasa wake wa Facebook ameweka wazi maono ambayo amedai kuoneshwa na Mwenyezi Mungu.
"Mwenyezi Mungu amenifunulia kwamba njama zote za kuivuruga Tanzania hazitafanikiwa! Amenionesha kuwa ameyafunga maandamano yoyote yale Tanzania na kwamba kila mwenye hila na nia mbaya kwa Nchi ya Tanzania yeye Mwenyezi Mungu, atashughulika naye.
Mwenyezi Mungu ameniambia atamalizana na wanaopanga kuliangamiza Taifa letu! Ninarudia tena ndugu zangu Watanzania.
Mwenyezi Mungu mwenyewe ataisimamia Tanzania na wote walioipangia mabaya atashughilika nao! Tanzania itabaki kisima cha amani na yeyote anayeitakia shari, hukumu yake itatimia ndani ya Disemba! Mimi siyo nabii ila ninawahakikishia kuwa baada ya ujumbe huu wa leo, sitaongea tena!
Endapo niliyoyasema leo hayatatimia, basi msisome tena chochote nitakachoandika hapa kwani kitakuwa ni uongo! Sitaandika tena endapo hayo hayatatimia!"