Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Nawaomba sana Mahashamu Maaskofu na wote walioumizwa na tukio hili baya (kushambuliwa kwa Padri Charles Kitima, Katibu Mkuu Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania) kujikabidhi kwa Mungu pale tunapoumizwa na udhalimu kama tunavyosoma katika Waraka wa kwanza wa Petro, sura ya pili aya ya kumi na tisa ambayo inasema "maana huu ndiyo wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu pale ateswapo isipo haki"
Aidha nawasihi sana watanzania wote tuendelee kupendana na kusimama pamoja kulaani matendo haya mabaya yasiyoakisi Tanzania yetu inayosifika kama kisiwa cha Amani."-Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza kwenye Sherehe za uzinduzi wa Jimbo Jipya la Katoliki Bagamoyo leo Mei 04, 2025.