SI KWELI PreGE2025 Dkt. Nshala ajiuzulu CHADEMA

SI KWELI PreGE2025 Dkt. Nshala ajiuzulu CHADEMA

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
1750832031231.png
 
Tunachokijua
Rugemeleza Nshala alikuwa miongoni mwa viongozi wa viongozi waliothibitishwa na baraza kuu, yeye akiwa mwanasheria mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) lakini pia amewahi kuwa rais wa chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) mwaka 2019 hadi 2020.

Awali Dkt. Nshala aliongoza jopo la mawakili upande wa CHADEMA wakati wa kuanza kusikilizwa kwa kesi namba 8960/2025 Said Issa Mohamed na wenzake dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya Chama.

Mnamo tarehe 10, Juni 2025 mahakama kuu ya Tanzania, masjala ndogo ya Dar es Salaam, CHADEMA ilipigwa marufuku kufanya shughuli zozote zile za kiutendaji na oparesheni mpaka kesi ya msingi iliyofunguliwa na Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA itakaposikilizwa

Wakati maamuzi hayo yanatolewa, upande wa utetezi (CHADEMA) haukuwa na mwakilishi yeyote Mahakamani, hiyo ni baada ya aliyekuwa Wakili wake Jebra Kambole kutangaza kujiondoa kwenye shauri hilo hatua iliyopelekea Mahakama kuendesha kesi kwa upande mmoja.

Katika mtandao wa Facebook kipeperushi kinachoitwa Kishindo kimechapisha taarifa inayosema Dkt. Nshala ajiuzulu nafasi yake ya mwanasheria mkuu CHADEMA kutokana na kuruhusu Wakili Jebra Kambole kujiondoa kwenye shauri lililokuwa likendelea mahakamani.


Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key Word Search) ulijiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani haikuchapishwa sehemu yoyote na vyanzo vya kuaminika. Vilevile hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na CHADEMA juu ya kupokea kwa barua ya kujiuzulu kwa Dkt. Nshala.

Madai ya kuwa Dkt. Nshala alichukua uamuzi huo baada ya kikao cha kamati kuu si ya kweli, kwani hakuna kikao kilichofanyika cha kamati kuu baada ya kuzuiwa kuendelea kwa shughuli zozote za cha na mahakama kuu.

Pia sababu nyingine inayoelezwa kuwa imesababisha kujiuzulu kwake kuruhusu wakili Kambole kujiondoa kwenye shauri lililokuwa mahakamani haina mashiko wala uhalisia wowote kwani wakili Kambole kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X alieleza kuwa alijiondoa kwenye kesi hiyo baada ya kuona uwepo wa ukiukwaji mkubwa wa kiutaratibu, haki na fursa ya kusikilizwa wakati wa shauri.

"Niliamua kujiondoa kwenye kesi ya CHADEMA leo baada ya kuona kuna ukiukwaji mkubwa wa kiutaratibu, haki ya fursa sawa ya kusikilizwa na mambo mengine wakati wa kusikilizwa shauri, niliona siwezi kushuhudia na kuwa sehemu ya ukiukwaji wa haki za binadamu na demokrasia nchini."

Ikumbukwe kuwa kipeperushi hicho mara nyingi kimekuwa kikichapisha taarifa zisizo za kweli na zenye kuchafua watu, hivyo ni vema kuthibitisha taarifa kabla ya kuziamini na kuzisambaza kutoka kwenye kipeperushi hicho
gazeti lenyewe sasa eti kishindo

sasa hio ni habari au headline mbona zimechanganywa frontpage na kurasa za ndani
Ikichanganywa na Headline ndo atakua ameacha kujiuzuru?
 
Huyu dogo anaupuuzi mwingi sana,, anatabia ya kutengeneza front page fake za viongozi mbali mbali..
 
20250612_190153.jpg
 

Attachments

  • 20250612_190153.jpg
    20250612_190153.jpg
    93 KB · Views: 14
Back
Top Bottom