Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema falsafa ya 4R ya Rais wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeakisi sawa sawa tabia ya Mwalimu Nyerere katika dhamira na namna ya kuliongoza taifa la Tanzania, na kuwa Rais Samia anatamani maono na mapenzo ya Baba wa taifa yaendelee kudumu na kuwepo kwa mshikamano katika taifa.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Dkt. Nchimbi ameyasema hayo Aprili 24, 2025 wakati akizungumza na wananchi pamoja na wanachama wa CCM mara baada ya kutembelea ujenzi na upanuzi wa majengo katika Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJNUAT) kilichopo wilayani Butiama mkoani Mara, likiwemo jengo la utawala, ujenzi ambao unagharimu zaidi ya bilioni 100.
Amesema kuwa uamuzi wa Rais Samia kutekeleza ilani ya CCM na kukubali kujenga chuo hicho unaonyesha dhamira yake njema ya kuiendeleza sekta ya kilimo nchini pamoja na umuhimu wake, hivyo ni sehemu ya kuenzi farsafa na mawazo ya Baba wa taifa.
"Baba wa taifa alitaka kilimo kiendelee kuwa ukombozi pekee kwa watu wetu, tuwe na kilimo cha kisasa chenye tija na kuongeza thamani kwa mtanzania, na tuwe na wasomi wanaotumikia taifa letu,.. tunawashukuru wote walioanzisha wazo la kuwa na chuo hiki, na viongozi wote waliosimamia ilani.