Mkuu Jagi,
Jagina , kwanza Asante kwa clip hii, nimeisikiliza yote mwanzo mwisho, huyu mtu wenu boys sana!, anazungumza ka. ... Kuna mtu wa kumpa nchi huyu?!.
Kiukweli na hili nalisema toka ndani ya moyo wangu, huyu ni mwanasheria boya tuu mvunja muungano asiyeujua msingi wa muungano na kuuita ndoa ya jinsia moja, wakati msingi halisi wa huu muungano wetu adhimu, ni kuna binti mrembo Zanzi, akajibebisha kwa Tanganyika, allowed ili apewe ulinzi na Tanganyika badala ya yule bwana wake Mungereza.
Muungano wetu una mke na mume, mke anakula bure, anavishwa na kuhudumiwa huduma zote bure huku mume ndio akimenyeka. Thread 'Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe?'
Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe?
OMO hajui kuwa muungano wetu ni muungano wa union ya nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar, kuungana na zote kupoteza souverenity zake na kuunda nchi moja tuu ya JMT , Thread 'Kuhusu Muungano, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Adai ni Zanzibar Pekee iliyopoteza Sovereignty, Je Yuko Sahihi?'
Kuhusu Muungano, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Adai ni Zanzibar Pekee iliyopoteza Sovereignty, Je Yuko Sahihi?
Kwa sasa hakuna tena nchi inayoitwa Tanganyika wala nchi inayoitwa Zanzibar, nchi ni moja tuu Tanzania, Zanzibar sio nchi bali ni sehemu ya Tanzania yenye utawala wake wa ndani, lakini Zanzibar sio nchi, Nje ya muungano, muungano wetu ni wa union ya nchi moja, ila ndani ya muungano, muungano wetu ni federation ya nchi mbili. Usawa gani huo anao udai?.
Wenzetu kabla ya kufunga ndoa huwa wana saint pre nauter agreement za mali za kabla ya ndoa zisiwe mali za ndoa. By the time EAC Currency board inavunjika, Zanzibar tayari ni mke wa mtu hivyo mali yake ikachukuliwa na mumewe kuwa mali ya ndoa. Usimtukane Nyerere mwizi tusije chafukwa humu tukatoleana maneno makali.
Katika ya Zanzibar ya 2020 Zanzibar inayo jiita nchi, haitambuliwa na katiba ya JMT. Huyu ni mpinga muungano tuu, tena kwa taarifa ni mimi nikajitolea kumshika sikio Dr Shein Thread 'Dkt. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii'
Dkt. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii
Hata Dr Mwinyi nilishauri Thread 'Ushauri wa Bure kwa Dkt. Hussein Mwinyi: Mfute Kazi Haraka Othman Masoud Kabla Hajaendelea Kueneza Sumu'
Ushauri wa Bure kwa Dkt. Hussein Mwinyi: Mfute Kazi Haraka Othman Masoud Kabla Hajaendelea Kueneza Sumu
Kila siku Zanzibar CUF walikuwa wanashinda lakini hawatangazwi, this time ushindi wa CCM ni ile kura ya mapema, hili boya lenu lisubiri tuu ving'ora!
P.