Miaka, miezi na hatimaye siku si nyingi zijazo mchakato wa kumpata Rais wa awamu ya 5 wa JMT. Wengi wanatajwa au kujinadi kuwa ndio watu wanaoweza kuipeleka ktk hatua kubwa kimaendeleo.
Kwa kuzingatia rekodi za utumishi wa umma pamoja na kisiasa sina wasiwasi hata kidogo kumpigia chepuo Dr. Harrison Mwakyembe kuvaa viatu vya Urais ambavyo vimewapwaya wengi baada ya kung'atuka kwa Baba wa Taifa Mwl. J.K. Nyerere.
Ujasiri wake, uzalendo na uadilifu wake pamoja na uchapakazi wake ni mtaji tosha kwa mwanasiasa huyu kuweza kuhimili mikiki ya kiti cha Urais.
Aidha, ifahamike kuwa akiwa Waziri wa Uchukuzi, amejitahidi kupigania maslahi ya nchi na kuondoa uozo uliokuwa umemshinda hata Mkuu pale Bandarini. Mwakyembe amethubutu. Vile vile jitihada zake katika kufufua Reli ya Kati zinaonekana. Vile vile hana masihala na kazi. Ameweza pia kuonesha uthubutu wa kupambana na Rushwa (Richmond) pamoja na upitishaji wa unga ktk viwanja vya Ndege. Kwa mtazamo wangu huyu anafaa.
Mwisho sijasikia popote akigawa fedha ili kurubuni watu kama wengine wafanyavyo. Hongera Dr. Mwakyembe nitakuunga mkono na wenye kulitakia mema taifa hili watakupigania. Nakuomba ungombee Urais hata nje ya CCM endapo itabidi.
Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo awe pamoja nawe.