Dkt Muhammed Seif Khatib na Mohamed Said wazungumzia siasa za Zanzibar

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,914
30,255

20140104_115839.jpg
Dkt. Muhammed Seif Khatib siku alipozindua kitabu cha Mwandishi, ''The Torch on Kilimanjaro,''
(Oxford University Press, Nairobi) Kempiski Hotel Dar es Salaam 2006 Kushoto kwake ni Sheikh Abdillah Nasir

DKT. MUHAMMED SEIF KHATIB AULIZA: HUU NI UUNGWANA?

HUU NI UUNGWANA?

(Dkt. Muhammed Seif Khatib)

Hivi uungwana ni nini? Ni kinyume cha ushenzi. Mtu anayestaarabika. Mtu anayestaarabika huwaje? Huyo huwa na tabia na mwendo unaoendana na maadili ya jamii.

Wengine huita mwendo huo suluhia. Uungwana unaambatana na tamaduni silka, na desturi ya mtu. Namna anavyoishi vizuri na wenzake. Upole wake. Jinsi anavyoweza kuwa na uvumilivu na ustahamilivu kwa kila jambo analokumbana nalo.

Namna anavyopambambanua mambo katika maisha. Hivi basi, uungwana na ustaarabu, hauna uhusiano na elimu ya mtu. Kubwa, ustaarabu na uungwana, haununuliwi kwa shahada.

Ungwana hautokani na nasaba ya mtu au asili yake. Katika ulimwengu huu, hakuna nasaba bora na tukufu kuliko nyingine. Kinyume na wakati wa ukoloni.

Wakati huo tuliambiwa kuwa nasaba bora ni ile ya watawala kutoka ughaibuni. Na hivyo, wenyeji tukajiona mbele ya watawala ni watu duni. Hata yapo maelezo kuwa huko Pemba baadhi ya watu wakawa wananunua kabila za Waarabu ili Waswahili waonekana waungwana.

Na wapo watu wachache waliona aibu kutaja asili zao kwa kuogopa kuonekana silo kabila la kistaarabu. Uungwana siyo rangi ya mtu, kama wapo watu wanaojiona kuwa rangi zao za weupe au hudhurungi, ndiyo kielelezo cha ustarabu, ni kujidanganya.

Zile nyakati za watu wachache kuona ngazi zao ndiyo uungwana na wale wenye ngozi nyeusi ni utwana umepitwa na wakati. Pia ni upumbavu kuona kuwa nywele na nyusi za mtu na ulaini wake kama manyoya ya mbwa ni jambo la kujionea fahari.

Na eti wale wengine wote wenye nywele, nyusi na kope ni kundi la watu wa kuwadharau. Uungwana haupimwi kwa kigezo cha aina ya nywele za mtu. Hoja ya aina hiyo kama ingekubaliwa basi mbwa, nguruwe, paka na panya wangekuwa viumbe bora duniani.

Je, mavazi ya mtu ndiyo vigezo vya ustaarabu wa mtu? Nani bora? Mvaa suti na buti? Mvaa kanzu na kofia? Mvaa sharti na suruali? Mvaa seruni na fulana? Mvaa gauni?

Viwango vya uvaaji wa nguo na uhusiano wa uungwana vikoje? Nani mwenye mamlaka ya kulinganisha na kulinganua?

Kwangu mimi hapana awezaye kusema vazi fulani ndiyo la kistaarabu. Kila vazi latokana na utamaduni wa pahala maalum. Wengine wote lazima waheshimu.

Hivi chakula cha mtu huonesha uungwana wake? Mla matoke au ugari wa uwele, mtama au muhogo siyo muungwana?

Uungwana wa mtu unategemea nini mtu anakula? Walau pilau au biriani ni utashi wao.

Mbona wote hao walao vyakula hivyo huwa havidumu humo matumboni mwao? Wakitaka wasitake watavitoa vyote kwa jina moja tu, ashakum, kinyesi.

Zanzibar ilitawaliwa kwa ubia wa Usultan wa Kiarabu kutoka Omani na Waingereza kwa karne moja na nusu. Kwa muda wote huo wenyeji wa Zanzibar walibatizwa kwa kuitwa “Watwana”, “Washenzi” na “Wajakazi”. Tabaka la wachache, watawala na wale wenye nasaba za kitawala wakawa ndiyo ‘Mabwana’ na ‘Waungwana’ na ‘Wastaarabu’.

Mapinduzi ya mwaka 1964 yaliyoletwa na Afro-Shirazi Party chini ya kundi la Waswahili yalifuta dhambi hii na kuwapatia uhuru na haki walio wengi. Mapinduzi ya Zanzibar ndiyo mkombozi na ndiyo heshima ya Waafrika wa Zanzibar.

Bila ya shaka wapo waliochukia kufanikiwa kwa Mapinduzi hayo. Wapo wanaotamba kwa udi na uvumba kuwa wanaoshika hatamu za serekali ya Mapinduzi lazima wongoke. Wanawataka “watwana”, “washenzi” na “wajakazi” wao wawatumikiye.

Kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar limekuwa pigo kubwa kwao. Nia, na dhamira yao imepanguliwa. Zipo fikra potovu na kasumba za kuwaona hawa wanaoendesha serekali ni wale wale “watwana”, “washenzi” na “wajakazi”.

Hivyo haikuwa jambo la ajabu kuona baadhi ya watu wenye fikra na mawazo hayo ya dharau kujitokeza hadharani na kuanza kumtusi kiongozi wa Zanzibar.

Bado kasumba ya dharau, kebehi na kejeli kwao kwa Waswahili haijawatoka. Wao huamini kuwa wao bado ni watukufu. Wao ndiyo waungwana. Nadhani mwenye kumtusi kiongozi wa nchi anakasumba ya kuwa yeye bado ni “muungwana”.

Kabila yake, rangi yake, nywele zake na damu yake ndiyo kigezo cha kuitawala Zanzibar na Waafrika wa Zanzibar. Kitendo cha kumtusi kiongozi wetu mpendwa na mtu anayeweza kuwa baba yake, ametukera wengi. Nilijaribu kutafakari maana ya neno “mshenzi”.

Nilipotazama katika kamusi likasema hivi; “Ni mtu asiyetaarabika na mwenye tabia ya kuudhi na kukera wengi”. Kwa hiyo kumbe yeye ni mshenzi!

MOHAMED SAID ANAMJIBU

Dkt. Muhammed Seif Khatib,

Hakika kinyume cha uungwana ni ushenzi.

Hili jambo liko wazi na hakuna mtu mwenye akili zilizotimia anaeweza
kukupinga.

Wengi wetu si wageni wa makala zako na hizo makala zako ndizo khasa
zinazoeleza fikra zako na wapi umesimama.

Kwa ajili hii nashukuru kuwa najua nazungumza na mtu wa aina gani.

Chanzo cha fikra zako na makala hii yako ni mapinduzi unayosema kuwa
yaliletwa na Afro- Shirazi Party.

Hii si kweli yote.
Ipo mikono mingi katika mapinduzi ya Zanzibar hadi ya Wayahudi.

Afro-Shirazi haikuwa na nguvu ya kuweza kufanya lolote bila ya msaada
waliopata kutoka Tanganyika.

Naamini unajua mchango wa Oscar Kambona na Abdallah Kassim Hanga.
Sina haja ya kumtaja Ali Mwinyi Tambwe na wengine kwa sasa.

Tanganyika hawakuingia kuipindua serikali ya Zanzibar kwa ajili ati Waafrika
walikuwa ''wanateswa,'' na ''Waarabu.''

Waliingia Zanzibar na lengo lingine.

Ndiyo maana unaona leo masheikh kutoka Zanzibar wameletwa Bara kuja
kuwekwa rumande.

Naamini katika hili wewe utakuwa mjuzi kunishinda mimi.

Ikiwa hujakisoma kitabu cha Dr. Harith Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri
Uhuru,'' fanya hima ukisome.

Kitabu hiki kipo bure mtandaoni.
Umeandika mengi lakini sioni sababu ya kujibu yote.

Itapendeza tukienda hatua kwa hatua na mjadala tukauwekea mipaka ili iwe
wepesi kueleweka.

Sasa ningepeda kurudi katika hoja ya ''Uungwana,'' na ''Ushenzi.''

Nusu karne si kubwa sana katika historia lakini inaweza kutosha kutupa kipimo
cha historia ya Zanzibar baada ya mapinduzi.

Wengi wangependa kupata majibu kutoka kwako kuhusu hii dhana ya ''Uungwana,''
na ''Ushenzi,'' Zanzibar.

Unaweza kuleta ushahidi madhubuti wa ''ushenzi'' uliokuwapo Zanzibar kabla ya
mapinduzi?

Kukusaidia kukufikirisha mimi nakuwekea hapa chini ''links'' ili ziweze kukuongoza:
  1. Mohamed Said: KABLA YA MAZOMBIE KULIKUWA NA AKINA KAUJORE: MWANAMAPINDUZI ALIYEUA WATU MSIKITINI
  2. Mohamed Said: AMAN THANI ANAMWELEZA MANDERA NA MATESO YA KUNG'OA KUCHA 9
  3. Mohamed Said: MASULTANI WALIPATAPO KUUA, KUWEKA JELA ZA MATESO NA KUFANYA DHULMA NYINGINEZO DHIDI YA WAZANZIBARI?
 
Marehem baba yangu mkubwa aliwahi kuniambia namnukuu...
Sisi watu wa mwambao wa afika mashariki tuliishi vizuri sana tuliishi kama ndugu wamoja bila kujuana kwa dini zetu makabila yetu rangi zetu na sehemu zetu tuzo ishi.
Tulitupa lugha zetu za asili tukawa tuna zungumza lugha moja tu ya kiswahili mpaka tukafikia kuitwa waswahili.
Lakini alipokuja muengereza kutawala afrika mashariki mambo yakaanza kuharibika na kubadilika.
Tukaanza kuulizana kabila kuulizana dini na hata rangi zetu mwenyezimungu alizo tujaalia.
Hilo ndio chimbuko la udini na ukabila ktk afrika mashariki.
Muengereza mtu mbaya sana..mwisho kunukuu.
Maneno haya niliyabeba na kuyafuatilia ukweli wake na niligudua kweli ukabila na udini uliletwa na muengereza ktk nchi zetu za afika mashariki.
Na niligunduwa kama waengereza ni watu wabaya sana ktk siasa za uchonganishi.
Mm nimeuliza mara kadhaa kuhusu biashara ya utumwa nimetaka niwekewe picha halisi ya muwarabu anaswaga waafrika watumwa mpaka leo sijawekewa zaidi nawekewa vikatuni vya kuchora tu.
Najiuliza huyu muwarabu 1 au 2 kusaga watumwa waafrika 20 mpaka 50 tokea ujiji mpaka znz hivi hao waafika walikuwa ni watu wa aina gani hasa.
Leo tu wamasai 2 au 3 wanasaga ngombe zisizo na akili kutoka simanjiro mpaka kusini lindi au mtwara na utakuta ktk ngombe 200 ngombe 10 mpaka 20 zinawapotea sembuse binaadam wenye akili?
Hii ni fitna ya muengereza kumgombanisha muarabu na mbantu tu na kwa hakika wamefanikiwa.
Nasikitika kuona maneno makali na ya kutisha yakitamkwa na mtu alie na umri mkubwa elimu kubwa madaraka makubwa mzee wangu muhamed seif khatib.
Sikutegemea lakini juu yayote hayo alio nayo ya umri ya elimu ya madaraka lakini bado ubinaadam haujamtoka na kila binaadam ana kasoro zake na kasoro zakibinaadam ndio ukamilifu wa binaadam.
 
sahimtz, kabla ya kuchangia naomba nikuulize kaswali kadogo, je una umri gani? Nauliza hivyo kwa sababu kwa mchango wako huu umevuruga kabisa mada kama ilivyoletwa na Mohamed Said na kuondoa kabisa hamu kwa watu waliokuwa tayari kushiriki kuijadili. Nachukua nafasi hii pia kukushauri umtake radhi mleta mada kwa kitendo chako cha kujiingiza kwenye mnakasha ambao unaonekana wazi unaokuzidi kimo.
 
Mag 3..kabla ya kuniuliza mm umri wangu ungejieleza ww kwanza umri wako na ungenifafanulia ni vitu gani vimekutoa hamu ww kutoshoriki mjadala huu ingawa tayari umo ktk mjadala.
Siamini kama ww kuna kundi la watu duniani unaliwakilisha mpaka ukafikia kusema hayo uliyo yasema.
Nakama kweli ww unawakilisha kundi fulani au msemaji wa kindi hilo ni vyema ukatueleza kundi lililokuchaguwa uliwalikilishe.
Mm nafikiri ww ndio umtake radhi mzee muhamed said kwa kumchagulia watu kushiriki mjadala na kmchagulia nini waandike.
Ningekuona wa maana sana kama ungenifahamisha nilicho kosea ktk uwandishi wangu.
Kuliko kutaka kujua umri wangu au kunichagulia cha kuandika.
 
20140104_115839.jpg
Dkt. Muhammed Seif Khatib siku alipozindua kitabu cha Mwandishi, ''The Torch on Kilimanjaro,''
(Oxford University Press, Nairobi) Kempiski Hotel Dar es Salaam 2006 Kushoto kwake ni Sheikh Abdillah Nasir

DKT. MUHAMMED SEIF KHATIB AULIZA: HUU NI UUNGWANA?

HUU NI UUNGWANA?

(Dkt. Muhammed Seif Khatib)

Hivi uungwana ni nini? Ni kinyume cha ushenzi. Mtu anayestaarabika. Mtu anayestaarabika huwaje? Huyo huwa na tabia na mwendo unaoendana na maadili ya jamii.

Wengine huita mwendo huo suluhia. Uungwana unaambatana na tamaduni silka, na desturi ya mtu. Namna anavyoishi vizuri na wenzake. Upole wake. Jinsi anavyoweza kuwa na uvumilivu na ustahamilivu kwa kila jambo analokumbana nalo.

Namna anavyopambambanua mambo katika maisha. Hivi basi, uungwana na ustaarabu, hauna uhusiano na elimu ya mtu. Kubwa, ustaarabu na uungwana, haununuliwi kwa shahada.

Ungwana hautokani na nasaba ya mtu au asili yake. Katika ulimwengu huu, hakuna nasaba bora na tukufu kuliko nyingine. Kinyume na wakati wa ukoloni.

Wakati huo tuliambiwa kuwa nasaba bora ni ile ya watawala kutoka ughaibuni. Na hivyo, wenyeji tukajiona mbele ya watawala ni watu duni. Hata yapo maelezo kuwa huko Pemba baadhi ya watu wakawa wananunua kabila za Waarabu ili Waswahili waonekana waungwana.

Na wapo watu wachache waliona aibu kutaja asili zao kwa kuogopa kuonekana silo kabila la kistaarabu. Uungwana siyo rangi ya mtu, kama wapo watu wanaojiona kuwa rangi zao za weupe au hudhurungi, ndiyo kielelezo cha ustarabu, ni kujidanganya.

Zile nyakati za watu wachache kuona ngazi zao ndiyo uungwana na wale wenye ngozi nyeusi ni utwana umepitwa na wakati. Pia ni upumbavu kuona kuwa nywele na nyusi za mtu na ulaini wake kama manyoya ya mbwa ni jambo la kujionea fahari.

Na eti wale wengine wote wenye nywele, nyusi na kope ni kundi la watu wa kuwadharau. Uungwana haupimwi kwa kigezo cha aina ya nywele za mtu. Hoja ya aina hiyo kama ingekubaliwa basi mbwa, nguruwe, paka na panya wangekuwa viumbe bora duniani.

Je, mavazi ya mtu ndiyo vigezo vya ustaarabu wa mtu? Nani bora? Mvaa suti na buti? Mvaa kanzu na kofia? Mvaa sharti na suruali? Mvaa seruni na fulana? Mvaa gauni?

Viwango vya uvaaji wa nguo na uhusiano wa uungwana vikoje? Nani mwenye mamlaka ya kulinganisha na kulinganua?

Kwangu mimi hapana awezaye kusema vazi fulani ndiyo la kistaarabu. Kila vazi latokana na utamaduni wa pahala maalum. Wengine wote lazima waheshimu.

Hivi chakula cha mtu huonesha uungwana wake? Mla matoke au ugari wa uwele, mtama au muhogo siyo muungwana?

Uungwana wa mtu unategemea nini mtu anakula? Walau pilau au biriani ni utashi wao.

Mbona wote hao walao vyakula hivyo huwa havidumu humo matumboni mwao? Wakitaka wasitake watavitoa vyote kwa jina moja tu, ashakum, kinyesi.

Zanzibar ilitawaliwa kwa ubia wa Usultan wa Kiarabu kutoka Omani na Waingereza kwa karne moja na nusu. Kwa muda wote huo wenyeji wa Zanzibar walibatizwa kwa kuitwa “Watwana”, “Washenzi” na “Wajakazi”. Tabaka la wachache, watawala na wale wenye nasaba za kitawala wakawa ndiyo ‘Mabwana’ na ‘Waungwana’ na ‘Wastaarabu’.

Mapinduzi ya mwaka 1964 yaliyoletwa na Afro-Shirazi Party chini ya kundi la Waswahili yalifuta dhambi hii na kuwapatia uhuru na haki walio wengi. Mapinduzi ya Zanzibar ndiyo mkombozi na ndiyo heshima ya Waafrika wa Zanzibar.

Bila ya shaka wapo waliochukia kufanikiwa kwa Mapinduzi hayo. Wapo wanaotamba kwa udi na uvumba kuwa wanaoshika hatamu za serekali ya Mapinduzi lazima wongoke. Wanawataka “watwana”, “washenzi” na “wajakazi” wao wawatumikiye.

Kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar limekuwa pigo kubwa kwao. Nia, na dhamira yao imepanguliwa. Zipo fikra potovu na kasumba za kuwaona hawa wanaoendesha serekali ni wale wale “watwana”, “washenzi” na “wajakazi”.

Hivyo haikuwa jambo la ajabu kuona baadhi ya watu wenye fikra na mawazo hayo ya dharau kujitokeza hadharani na kuanza kumtusi kiongozi wa Zanzibar.

Bado kasumba ya dharau, kebehi na kejeli kwao kwa Waswahili haijawatoka. Wao huamini kuwa wao bado ni watukufu. Wao ndiyo waungwana. Nadhani mwenye kumtusi kiongozi wa nchi anakasumba ya kuwa yeye bado ni “muungwana”.

Kabila yake, rangi yake, nywele zake na damu yake ndiyo kigezo cha kuitawala Zanzibar na Waafrika wa Zanzibar. Kitendo cha kumtusi kiongozi wetu mpendwa na mtu anayeweza kuwa baba yake, ametukera wengi. Nilijaribu kutafakari maana ya neno “mshenzi”.

Nilipotazama katika kamusi likasema hivi; “Ni mtu asiyetaarabika na mwenye tabia ya kuudhi na kukera wengi”. Kwa hiyo kumbe yeye ni mshenzi!

MOHAMED SAID ANAMJIBU

Dkt. Muhammed Seif Khatib,

Hakika kinyume cha uungwana ni ushenzi.

Hili jambo liko wazi na hakuna mtu mwenye akili zilizotimia anaeweza
kukupinga.

Wengi wetu si wageni wa makala zako na hizo makala zako ndizo khasa
zinazoeleza fikra zako na wapi umesimama.

Kwa ajili hii nashukuru kuwa najua nazungumza na mtu wa aina gani.

Chanzo cha fikra zako na makala hii yako ni mapinduzi unayosema kuwa
yaliletwa na Afro- Shirazi Party.

Hii si kweli yote.
Ipo mikono mingi katika mapinduzi ya Zanzibar hadi ya Wayahudi.

Afro-Shirazi haikuwa na nguvu ya kuweza kufanya lolote bila ya msaada
waliopata kutoka Tanganyika.

Naamini unajua mchango wa Oscar Kambona na Abdallah Kassim Hanga.
Sina haja ya kumtaja Ali Mwinyi Tambwe na wengine kwa sasa.

Tanganyika hawakuingia kuipindua serikali ya Zanzibar kwa ajili ati Waafrika
walikuwa ''wanateswa,'' na ''Waarabu.''

Waliingia Zanzibar na lengo lingine.

Ndiyo maana unaona leo masheikh kutoka Zanzibar wameletwa Bara kuja
kuwekwa rumande.

Naamini katika hili wewe utakuwa mjuzi kunishinda mimi.

Ikiwa hujakisoma kitabu cha Dr. Harith Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri
Uhuru,'' fanya hima ukisome.

Kitabu hiki kipi bure mtandaoni.

Back
Top Bottom