Dkt. Louis Shika aeleza Magumu aliyopitia hadi akatoroka Urusi. Alitekwa na kukatwa Vidole, Tanzania ilimtelekeza...

watanzania wengi wanaoenda urusi huishia kuvurugikiwa akili.

Nawafahamu zaidi yA watatu. Sijui kuna jambo gani (japo kuna exception ya wazanzibar)

mimi mwenyewe nawajua baadhi........inaelekea vodka sio rafiki wa mtu mweusi au ni nini......?.......
 
Yani hata media kubwa kubwa za bongo ziliripoti upande mmoja bila kubalance story , makanjanja ni wengi sana
 
Kweli kabisa. Tatizo hili limewakumba wengi waliojihusisha na unywaji wa pombe kali za Kirusi. Si Wazanzibari tu ambao hawakuguswa na janga hili, kuna wale wa Bara ambao wameepuka kwa kutojihusisha na ulevi huo.
Kwani huyu Dr. amesema anakunywa pombe?
 
Pia he seems to be very intelligent,alichosema juu ya balozi zetu ni kweli hazina msaada kwa Watanzania wakiwa nje ......wajitadhimini,sio mtu wa kwanza mwenye genuine problem...kujikuta anasaidiwa na ubalozi wa nchi nyingine hasa .UK Kwa...commonwealth umbrella au US
Wanaweza wakawa shida ni bajeti,lkn hata km ni bajeti unaweza umkapa MTU hata ushauri wa kumlink na nyumbani bongo akapata msaada,kuna mmoja Msumbiji alikuwa anakuambia jinsi ulivokuja ndo utakavorudi.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Anasema akaunti yake INA Kama bilioni 20 hivi halafu hapo hapo anataka marafiki wamchangie laki 3 ili alipie bima hela zije.
Hivi inawezekanaje hii?.
 
Anasema akaunti yake INA Kama bilioni 20 hivi halafu hapo hapo anataka marafiki wamchangie laki 3 ili alipie bima hela zije.
Hivi inawezekanaje hii?.
Atakuwa kadanganywa na matapeli wa mtandaoni ambao mara nyingi wanakutumia email kuwa umeshinda Dollar Kibao in the region of say 10,000. Mwisho wanakuomba taarifa zako za benki na kukutaka ulipie BIMA na kitu wanaita "Administrative cost" pesa kidogo kama dola 500 hivi ili wakutumie BULUNGUTU LAKO. Ukituma ndo kwa heri.

Mimi uwa nawaambia wakate hapo tena wakate nyingi zaidi itakayobaki wanitumie, ukiwaandikia hivyo wanapotea lkn baadaye wanakurudia na hadithi ile ile. Sijui uwa wanatumia vigezo gani kuchagua waanga wao.
 
Mbona alisema ana Kampuni urusi
Anataka ku justify maelezo yake. Huu utapeli ni wa kawaida sana na wanufanya wanigeria. Huyu mzee kakutana na hayo matapeli ya mtandaoni. Kuna jamaa aliwahi kufukuzwa kazi kwa kutaka apate dola 5000 awalipe wamhamishie pesa na akawa anatumia njia za kihalifu kupata hiyo $5000
 
Back
Top Bottom