Dkt. Kipilimba, sasa yatosha!

wakiamua wanamfikia sababu ni watesaji na wauwaji
 
Maboga hayajui kwamba Tanzañia siyo ccm.
 
Hivi bosi Ni Mungu au Tume ndio hutangaza matokeo..ukizingatia na Uhuru wa Tume yetu. Tusimuhusishe Mungu kwenye haya Mambo ya siasa ambazo hazina ukweli hata chembe. Ukweli CCM bara tulishinda tuu..Ila kisiwani hahahahaaa..😄😄😄😄.TISS wanajifahidi mbona ila na wao wanadam wanamadhaifu .😀😊
 
Tatizo mi naona ni kuwa idara moja imerundikiwa majukumu kedekede .

Ningeshauri siku ikivunjwa ziundwe taasisi mbili .

Moja ihusike na ujasusi wa ndani kama vile NSA

Na ingine ihusike na ujasusi nje ya mipaka yetu ya nchi kama CIA

Hapo watakuwa makini zaidi .

Na recruitment itokee jeshini moja kwa moja hao waliopo sasa hapo walete uraini tuuze nao karanga .
 
Walikuwa hawajui
 
Sio vizuri kumtisha mtu mkuu sasa kama walijua hilo kwa nini wasingeishauri serikali ili ndege isiende mda mwingine unapokataa kuambiwa ukweli nako ni shida
 
Nimeongea na watu
Nimeongea na watu wengi wanaofahamu mfumo wa TISS na wanaomfahamu Dr Kapilimba kwa undani. DG-TISS siyo tatizo na taasisi yenyewe iko vizuri ila shida ni Jiwe mwenyewe.

Kwa sasa kuna TISS rasmi chini ya DG -TISS halafu kuna 'rogue TISS' inayofanya kazi kwa maelekezo ya Bashite. Hii 'rogue TISS' inahusisha maafisa wa juu wa TISS ambao wako loyal kwa Bashite kama yule Nyaulingo au yule Musalika aliyepelekwa kuwa RAS Tabora . Bashite ana nguvu sana kuliko mtu yeyote nchi hii ukimuacha Jiwe. Wakubwa wa vitengo nyeti wanajuwa hili kuwa wakimzuia Bashite asitekeleze azma yake basi wanaweza kutemeshwa vibarua vyao na Jiwe kwa shinikizo la Bashite.

Ili kulinda vibarua vyao wanaamua kufanya yanayowahusu na kumuacha Bashite aendelee
 
Kama walizifahamu walichukua hatua gani ili kutuepusha na fedheha. Ninachokiona hatuko salama, kilichopo ni "taarifa za kiitelijensia" za kuzuia mikutano ya vyama vya siasa. Wenzetu wapo kwenye uchumi na teknolojia sisi tumejikita kwenye siasa za kitanzania
 
Unakuta wanahangaika na kudukua simu, wakati kuna mambo makubwa sana wanaweza kuyafanya ili kuliokoa Taifa.
 
Idara hii ipo, na hailali kucha ipo kazini. Tofauti ni malengo yamebadirika, kuhakikisha uimara wa ccm na maslahi mapana ya viongozi wake. Maslahi ya kitaifa si jukumu lao tena. Hata jirani zao TCCB, tofauti hakuna, kama mapacha vile.
 
Inasikitisha sana sijui wanatumia recruitment gani siku izi unabaki kujiuliza wanawatoa wapi

Recruitment zao wanaangalia mtoto wa mjomba kafeli,bas tumpeleke tiss au police hawana mda wa kudeal na intelijensia zao wala uwezo wao wa kufanya hizo kazi
 
ambaye hajui kwamba TISS inatumika kuteka watu akamuulize tajiri wa musoma! asingewawahi tungekua tumemsahau au wangekua wamemnyamazisha kwa kumteka kifikra! maana wakikuteka akili inakua sio yako tena unaish kwa hofu mpaka unakufa! kama hutaki muulize Roma
 
Ni wapi nimeichafua serikali?
Kutoa ushauri ni kuchafua serikali?
Mods wasingeruhusu mada ya kuichafua serikali ikae humu.
 
Kwani mkuu shauri halikuwa exparte ( kusikilizwa upande mmoja)
Maana summons lazima itolewe ku komplay na rule of natural justice
 
Siku hizi hakuna TISS yenye kumaanisha USALAMA WA TAIFA bali kuna TISSS yenye kumaanisha CCM inabaki madarakani daima, acha tuvune tulicho panda,
 
Wewe umeonesha uafrika wapo kwa comment yako.

TISS iko weak, sio tu ktk sakata hili la ndege ila mengi mengi mno, mauaji, vitisho, maadili n.k

Kuna kipindi Lissu alimwambia mpka Kipilimba kwamba yeye anafatiliwa na vijana wa TISS, Lissu akaja kupigwa risasi kweli, mpaka leo kipo wapi kinachoendelea?

Suala la ndege limetuvua nguo, kuonesha ujuha wetu tumeenda kuandamana ubalozini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…