Mwanasheria Dkt. Kilangi atoa ufafanuzi kuhusu mchanga wa madini uliozuiliwa na Rais

Doctor Kilangiee!! nakupinga sasa hatuwezi kuuza nchi kwa ajili ya makaratasi sasa!!!!!!

1. Umezungumzia suala la common heritage kuwa kwa kuwa baadhi ya nchi hazina madini basi iwe ruksa kwenda kuchota kwenye nchi zilizonayo .........Haikubalikiii!!!!! madini ni yetu na suala la madini si kama kwenye "high sea" amabapo kila mtu anaruhusiwa kutembea na kuvua ( shammba la bibi ) @ " RESCOMUNIIS"

2.Eti tutaenda kunyolewa bila maji huko ICSID kwa ku breach 'fair and equitable treatment' Hakuna hiyooo!!! wao wametutendea equity gani mpaka na sisi tuwatendee equity wanatuibia halafu waseme equity " IF YOU NEED EQUITY DO EQUITY:

3. Kwa kuwa hakuna mkataba wa kimataifa ambayo haina claus ya " PACTA SUNT SERVANDA" na kwa kuwa hao "mabwana wakubwa" hawakuiheshimu na wakaendelea kusafirisha mchanga kwa udanganyifu " maana yake hawajaheshimu mkataba" basi automatical doctine ya '' REBUS SIC STANTIBUS '' ita apply na kuufanya huo mkataba usitekelezeke !! yaani umevunyika nganganyanga beyond repair.

Nani aliyethibitisha kwamba walikuwa wanasafirisha mchanga kwa udanganyifu so far? Ni ile Kamati ya "maprofesa"? Ina mamlaka hayo kwa mujibu wa mkataba tulioingia na hao "wezi" wetu?

Mpaka sasa ACACIA wanapinga matokeo ya uchunguzi wa kamati ya "maprofesa", na wana hoja zao ambazo ikibidi zitaenda kupambanishwa kule ambao wakati tunaingia nao mkataba tulikubali kuwa inapotokea mgogoro baina yetu na wao tutaenda kusuluhishwa au kumalizana.

Nani anathibitisha kuwa tulikuwa tunadanganywa?
 
Hili ni andiko la Dr Adelaus Kilangi,mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine tawi la Arusha,mwanasheria kitaaluma aliyebobea kwenye sheria za madini!
............................................
Wandugu,
1. Nitaomba tuvumiliane. Niliombwa kusema kitu. Nitaandika kwa kirefu kidogo. Kwa kuwa ninaandika muda huu, nina advantage ya kuwa nimesoma maoni mengine yaliyotangulia.

Nilicheka sana kaka yangu Ngwilimi aliposema halali hadi nimetoa maoni. Sipendi kumkosesha usingizi. Nitaandika kwa paragraphs ili kurahisisha rejea.

2. Nimeangalia maoni mbalimbali yaliyotolewa humu. Yanagusa maeneo yafuatayo:

i)Statement ya Acacia.
ii)Suala la sovereignty over natural resources na tatizo la 'state capture'.
ii) Suala la smelting na mchanga wa makinikia.
iv)Nini tunaweza kufanya kwenye mikataba:
- kuvunja mikataba?
- kushitaki kwa kutuibia?
- ku-review mikataba?
- au kuweka mikataba wazi?
vi) Sheria za kimataifa.

3. Haya ni mambo mengi na mazito. Sio rahisi kuya-summarize kwenye text ya simu. Pia ni vema kukubaliana kuwa kwenye mjadala kama huu itikadi, vyama na mihemuko iwekwe pembeni. Hoja zitawale.

4. Sitaingia kwenye mtego wa kulaumu au kutetea mtu. Nitajikita kwenye masuala ya msingi yanayotengeneza chimbuko la tatizo. Matatizo katika sekta yetu ya Madini, kama ilivyo ktk nchi nyingi zinazoendelea, nyingi zikiwa Africa, na Tanzania ikiwemo, yana chanzo chake ktk maeneo matatu:

i) Falsafa inayotuongoza,
ii) Sheria inayotuongoza.
iii) Mfumo wa utawala.
FALSAFA INAYOTUONGOZA

5. Malalamiko kuwa nchi zinazoendelea na zenye kumiliki resources zinapunjwa hayakuanza leo. Yalianza miaka ya 1950. Haya yalipelea kuibuka kwa falsafa mbili: resource nationalism na resource liberalism. Kila moja ina implications kwenye sheria na kwenye namna nchi itasimamia raslimali zake.

6. Wale wa resource nationalism walitaka nchi iwe na mamlaka kamili kwa resources zao na ziwasaidie na wakatengeneza principle ya permanent sovereignty over natural resources. Walitaka mambo haya yasimamiwe zaidi na sheria za nchi.

7. Wale wa resource liberalism wanataka raslimali ziwe wazi kwa dunia nzima maana mgawanyo wake duniani hauna usawa (japokuwa wao wamelinda teknolojia yao).

8. Katika vision ya nchi, nchi inachagua falsafa ya kufuata. Falsafa inayofuatwa huathiri sera na sheria.

9. Baada ya Uhuru Tanzania ilifuata falsafa ya resource nationalism hadi 1979. Kuanzia 1979 Tanzania ikaanza kufuata resource liberalism baada ya shinikizo la World Bank na IMF chini ya kitu kinaitwa Washington Consensus. Falsafa hii ilifikia kilele miaka ya 1990 mwishoni. Kwa hiyo ikaathiri sera na sheria.

10. Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 2000 nchi imejaribu kurudi kwenye resource nationalism lakini inakwama. Sasa hivi resource nationalism sentiments ziko very high.

SHERIA INAYOTUONGOZA
11. Kama nilivyosema, falsafa huja kuathiri Sera na Sheria. Sheria muhimu hapa ni (nitachanganya lugha kidogo hapa):

i) investment law
ii) mining/petroleum law
iii) tax law.
Investment Law

12. Hiki ni chanzo kikubwa cha ugomvi. Nchi zilizoendelea zimeshinikiza uwepo wa mfumo wa sheria wenye kugandamiza nchi zinazoendelea. Mfumo huu unagawanyika kama ifuatavyo na kila kipande kina matatizo makubwa na mengi.

i) Customary international law. Humu kuna principles nyingi ambazo nchi inaweza kuambiwa kuwa imezivunja. Nchi zilizoendelea na zinazoendelea zinagombana juu ya principles hizi.

ii) multilateral framework. Hapa kuna mikataba ya mataifa mengi. Tanzania ni mwanachama Wa mikataba miwili yaani unaoanzisha Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA) na unaoanzisha International Centre for the Settlement of Investment Disputes (ICSID).

iii) bilateral framework. Hii ni mikataba kati ya nchi na nchi (bilateral investment treaties - BITs. Ila inawalinda wawekezaji toka nchi hizo mbili. Nchi inaweza kushindwa kesi sio sababu ya mikataba ila kwa sababu ya BITs.

iv) National framework
(mining and petroleum acts) - hizi zina certain aspect fulani za investment.

v) State-investor agreements (tunayoita mikataba na wawekezaji).

Wengi tunaangalia hii tu. Hatuangalii hizo frameworks zingine ambazo baadaye zinatukandamiza.
Pia, framework No. i, ii, na iii ziko chini ya himaya ya sheria za kimataifa.
Mining/petroleum law

12. Mining and petroleum law hutengenezwa na nchi yenye resources. Lakini nchi zilizoendelea huwa zina-influence mno zoezi la utngenezaji sheria hizi, maana hizo ndio hutoa mineral or petroleum rights. Wako tayari hata kuidanganya nchi kwa misaada wanayojua tunahitaji sana.

Wanaweza kutudanganya kuwa wanatupatia technical support. Kumbe wanatutengenezea sheria itakayowezesha kutuibia.
Tax Law

13. Tax law ni Eneo jingine ambalo linatumika sana kutuibia. Mnapokuwa mnatengeneza sheria zenu za kodi hawa jamaa hawaachi kuwazungukieni na kuwa-influence.

MFUMO WA UTAWALA

14. Kuna tatizo kubwa sana linalozikumba hasa nchi za Africa na baadhi ya zinazoendelea zilizo nje ya Africa. Hili ni tatizo la 'state capture'. Kama ilivyo concept ya 'river capture' kwenye geography, basi state capture means influence by the elite or business people or investors such that the state (led by its government) fails to think on its own and it follows the thinking of the group that has captured it.

15. Wakati wa kufuata falsafa ya resource liberalism, Tanzania iliingia kwenye total 'state capture'. Ndio kusema tuliondoa kichwa chetu tukaweka kichwa kingine. Tukawa tunafikiri kwa mfumo wa hicho kichwa kingine. Sasa tumeanza kurudisha kichwa chetu.

SUALA LA MCHANGA WA MADINI
Utangulizi

16. Suala hili wote tunajua background yake. Kamati ya Pili natumaini itafanya kazi ya na uchambuzi Wa kutosha.
Mchanga kwenye Madini ni Mali ya nani?

17. Principle ya 'permanent sovereignty over natural resources inasema huu ni Mali ya nchi. Article 27 of the Constitution of the URT inachukua mwelekeo huo huo. Hata Section 5 of the Mining Act says the same. And the same position was in Mining Acts za 1998 na 1979. Zile za kabla ya Hapo ziikuwa zinazungumzia mwingereza.

18. Hata hivyo kuna ubishi kuwa pale nchi inaposaini state-investor agreement (Mineral Development Agreement) na kutoa mineral rights je nchi inakabidhi sovereignty yote kwa companies. Makampuni yatasema 'ndiyo'. Nchi zinatakiwa ziseme 'hapana'.

19. Mineral rights means rights to extract minerals and sell them. Does it include transporting them outside the country in order to extract minerals? I don't think if contracts say so.

And if they do, that defeats the principle of permanent sovereignty over natural resources!
Nini Tunaweza kufanya kuhusu mikataba?

20. Kuivunja? Hatuwezi kuivunja. Tumesaini mkataba wa MIGA na wa ICSID. Tutashtakiwa kwa kuvunja customary law principle ya 'fair and equitable treatment', na 'state responsibility' na ya 'respect for acquired rights'. Tutapelekwa mbele ya ICSID na kuhukumiwa, kisha tutaminywa na MIGA itakayokamata mali zetu popote zilipo.

21. Kuwashtaki makampuni kwa kutudanganya? Tunaweza, na tutatumia argument kuwa wamevunja customary law principle ya 'good faith and prohibition of abuse of rights'. Lakini wakisema uchunguzi wa mchanga tumeufanya kwa upande mmoja wanaweza kushinda.

22. Ku-review mikataba? Lazima tuwe tume -incorporate kwenye mkataba kipengele kinachohusiana na doctrine ya 'clausula rebus sic stantibus'. Hii ni doctrine inayoruhusu ku-review mkataba kama conditions Fulani zikibadirika. Lazima kifungu hiki kiwe kwenye mikataba. Hawa jamaa walihakikisha hakimo kwenye mikataba yetu. Kwa hiyo ukianza process ya ku-review unilaterally watasema umevunja principle ya 'fair and equitable treatment'.

23. Kuiweka wazi mikataba ili watu wote waione? Investors wataegemea kwenye principle of confidentiality of investment agreements. Hii principle IPO katika international law. Ingawa sasa kuna mabishano makubwa. Wengine wanaipinga. Ndio maana japokuwa tuna sheria mpya ya uwazi na uwajibikaji - Extractive Industries (Transparency and Accountability) Act, 2015, ambayo inasema mikataba yote iwekwe wazi, makampuni yamekataa kwa kusema kuwa wakati wanasaini mikataba hiyo sheria hiyo haikuwepo. Mnavyojua sheria hairudi kinyume. Kumbe watadai bado canal in sea na principle hiyo.

24. Kwa hiyo kumbe tunaweza kufanya nini sasa? KAMA ALIVYOSEMA MHESHIMIWA RAIS, HII VITA, NA HII NILIYOTOA HAPA NDIO PICHA HALISI YA VITA HII.

Basi wandugu siku nyingine msinitafute ili nitoe Maoni yangu. Vinginevyo mjiandae kusoma kitabu.

Dr. Adelatus Kilangi
Mwalimu wangu kwa vile unafundisha chuo nilichosoma asante kwa maelezo yako ya kitaalamu.
Kwa ufahamu wangu naona hapa ni vita kati ya Sayansi, sheria, biashara na UTAIFA.
Nini tufanye
Tuifanye biashara hiyo sisi wenyewe kwa kuweka mtaji bila hivyo tutatumbuana sana.
Botswana wameweza

Jedwali Na.12 Umiliki wa Makampuni ya Madini Botswana

1. kampuni
Debswana Diamond LTD

Wenye hisa

Serikali ya Botswana (50%) De Beers (50%)

madini
Almasi, makaa ya mawe, shaba na nikeli


2. Bamangwato Concession ltd

wenye hisa
Serikali ya Botswana (30%)

Anglo american (30%)

Wengine (40%)

Madini

Nikeli na kobati


3.Tati Nickel Mining Co.
Wenye hisa
Serikali ya Botswana (15%)

Canadian Lionore Mining International (41%)

Anglo American (43%)

Wengine (1%)
Madini
Nikeli na kobati

Kwa kuangalia hapo juu ni dhahiri kuwa serikali ya Botswana imewekeza katika biashara ya uchimbaji wa madini katika nchi yake hivyo kustahili kupata mgawo sawa na ukubwa wa uwekezaji wake. Wabotswana hawapewi mgao wa asilimia 50 kutokana na mauzo ya almasi kwa sababu tu almasi ipo Botswana bali ni kwa sababu wamewekeza katika uchimbaji wa almasi.

Sisi ni Nationalism Nationalism- tumetumia nationalism tukapata uhuru bado tunauwana tu

Mwalimu wangu niruhusu nitoe mfano mwingine kwa kizungu unachokifahamu vuzuri pia

Let us preface ourselves with a remarkable case study from South Africa.

Bafokeng is a small tribe in South Africa of around 150,000 (300,000 if it include these in Zimbabwe) people that for a long time have occupied an area of around 1,200 square kilometers north west of Johannesburg. Underneath their dwellings, shrubs, grazing land, and arable land, sits the world’s largest deposit of platinum.

The area was invaded by whites who displaced the indigenous. When the Bafokeng were displaced their King dispatched the brightest young men to work in diamond mines in order to earn money with it they could buy back their land.

Meanwhile in 1925 mineral explores discovered the platinum and started mining it in 1960s; the Bafokeng had repossessed their land and were in the long legal battle for gaining the mineral right. They got it in 1999 through the court of law. The loyalty they earned from the mineral rights was converted into shares. As of now Bafokeng as tribe owns 13.2 percent stake in the Impala Platinum, the world’s second largest platinum miner on top of getting 22 percent of loyalty.

Bafokeng is guided by Vision 2020 that challenges the Bafokeng people to reduce their dependency on their diminishing mineral assets and to become a self-sufficient community within the first 20 years of this century, whilst also maintaining the Bafokeng culture.

The main areas of emphasis of Vision 2020 fall into the following areas: Investment diversification; Economic Development; Education Planning; Infrastructure Development/Master Plan; Health and Social Planning; and Crime Free Environment.

The Bafokeng has established a sovereign wealth fund, Royal Bafokeng Holdings (RBH), which is responsible for overseeing the growth and maintenance of the community’s income streams. RBH has invested royalties and dividends in a number of projects, and in civic administration and social services. These include: Royal Bafokeng Sports, which is in charge of sport development among the residents of the area; Royal Bafokeng Administration (RBA), which is principally a town planning unit charged with service delivery and monitoring the progress of the Master Plan across all the regions. And Royal Bafokeng Institute (RBI), whose goal is to improve education and learning in the Royal Bafokeng Nation. Bafokeng have also recruited several manufacturing companies as part of a drive to expand the nation's exports beyond raw materials.


The gaining of the mineral rights was the first step and probably the easiest one. The second step was to ensure sustainability: What does the Loyal queen mother say:-

“I keep telling the women of the Nation: if we spend all the money what will happen? What will happen tomorrow? Platinum is not our wealth, our wealth is through leadership”

The third step was to make everyone see it that he or she is benefiting from the fight for regaining the land and subsequent mineral rights as well as the communal investment that made to day:

· Bafokeng the wealthiest tribe in Africa

· Bafokeng public rise their expectation to live a lavish life style

· Public to put pressure for swift and more distribution of wealth to individuals

The loyal king provides the leadership where he says:

“We are facing a challenging situation. The expectations are bigger and bigger. All we have to do is ask people to exercise constraint, but this is hard to sell to people with high expectation. (Russell, 2009: 157-180).

From the above case study we can have some few question to help us find answers to the issues of sustainability that are always overlooked.

Again, the issue of nationalism did not play in the favor of Bafokeng, they had to invest using income generated from the loyalty.
What are we doing with the loyalty we have gained so far- tumekula tu mwalimu

MAONI YANGU

Turudi kwenye sayansi
Invest ili ule jasho yako
 
Nani aliyethibitisha kwamba walikuwa wanasafirisha mchanga kwa udanganyifu so far? Ni ile Kamati ya "maprofesa"? Ina mamlaka hayo kwa mujibu wa mkataba tulioingia na hao "wezi" wetu? Mpaka sasa ACACIA wanapinga matokeo ya uchunguzi wa kamati ya "maprofesa", na wana hoja zao ambazo ikibidi zitaenda kupambanishwa kule ambao wakati tunaingia nao mkataba tulikubali kuwa inapotokea mgogoro baina yetu na wao tutaenda kusuluhishwa au kumalizana. Nani anathibitisha kuwa tulikuwa tunadanganywa?
Ni hivii?????? kwenye sayansi hakunaga majibu mawili ukifanya mfano quatitative analysis ya mineral flani ukishafikia mwisho na kusema labda 10kg ya dhahabu basi jibu ndio hilo. Hao waliochukua muda wao wameapa, na ni wataalamu walibobea kwenye fani hizo. Sayansi sio kama sheria muanze kuleta mambo ya " NEMO JUDEX IN CAUSA SUA" haipogo
 
Ni hivii?????? kwenye sayansi hakunaga majibu mawili ukifanya mfano quatitative analysis ya mineral flani ukishafikia mwisho na kusema labda 10kg ya dhahabu basi jibu ndio hilo. Hao waliochukua muda wao wameapa, na ni wataalamu walibobea kwenye fani hizo. Sayansi sio kama sheria muanze kuleta mambo ya " NEMO JUDEX IN CAUSA SUA" haipogo
Kwahiyo hili ni suala la kisanyansi au la kisheria zaidi? Kuapa sio tatizo hata wanaotumbuliwa wanakuwa wameapa! Nilitaka tu kujua kama ripoti ya "maprofesa" ni "duniani na mbinguni"-kwamba sasa imethibitishwa, with no reasonable doubt kwamba ACACIA ni wezi?
 
Ukweli unauma. Mkuu punguza hasira.

Hata hivyo kuna kanuni ya Kiutawala inayosema ni bora kufanya uamuzi hata kama uamuzi huo ni mbaya. Kwani ukiwa mbaya utasahihishwa kuliko kukaa kimya wakati unajua kitu hicho siyo siyo sahihi.

Hii ni vita hivyo tukubali kutakuwa na maumivu. Inawezekana tukashindwa hivyo kulipa fidia, sawa tu ila tutarekebisha baadhi ya mambo ambayo ni wizi dhahiri. Kama kweli mchanga huo hauna faida kiasi hicho mbona wanapiga kelele na kukimbilia mahakamani! Wanajua walivyokuwa wanafaidi na sasa povu linawatoka.

Cha msingi waletwe wachunguzi wengine kuthibitisha uchunguzi uliofanywa na Tume halafu walipe fedha zote walizotuibia. Kisha mikataba ifanyiwe review

Ndiyo tunawasahihisha tulizeni mshono.
 
Kwahiyo hili ni suala la kisanyansi au la kisheria zaidi? Kuapa sio tatizo hata wanaotumbuliwa wanakuwa wameapa! Nilitaka tu kujua kama ripoti ya "maprofesa" ni "duniani na mbinguni"-kwamba sasa imethibitishwa, with no reasonable doubt kwamba ACACIA ni wezi?
Hakuna jibu zaidi ya hilo. Hivi unajua kuwa Mji wa geita unaelea ardhi yote chini hawa " MABOSI WAKUBWA " @ as per lissu. Wamechimba underground kuchukua kila kitu???
 
Agent of imperialist at work. Ahadi mojawapo Ya mwana Tanu ilikuwa ikisema nitajiellimisha kwa kadri Ya uwezo wangu kwa faida Ya watanzania walio wengi .mleta maada kajielimisha sana kwa faida ya imperialists. Very sad.Yeye na tundu lisu wamejielimisha sana kwa faida ya imperialists
Tatizo siyo yeye, tatizo ni walio tunga sheria na mikataba chini ya CCM na wabunge wao ambao wemyewe kila kitu ndiyo
 
Maelezo ya Dr. Kilangi ni namna nyingine yenye ufasaha zaidi ya maelezo ya Mhe. Tundu Lissu. They have the same position. Na kwa maelezo ya Dr. Kilangi kweli hii ni vita, na mshindi wa vita anajulikana wazi kwa mujibu wa maelezo hayo ya Dr. Kilangi.

Kwa mtazamo wangu kabla ya kuanza vita, maelezo ya namna ya Dr. Kilangi yalitakiwa kutumika kwenye kupanga vita hii ili kuona kama kuna faida kubwa hasara kidogo au hasara kubwa faida kidogo. Pia ingesaidia kutoa options nyingi na kuchagua favourable option kama ingekuwepo kati ya hizo options.

Mimi ni mmoja wa watu tutakaopenda tusome 'kitabu' ili kupata mwanga zaidi. Kwani ili chapisho liitwe kitabu linakuwa na features zipi? Tena kitabu ndio kizuri zaidi kwani tutaona na references au bibliographies zaidi ambazo zitatusaidia tuone hoja zao kamili.
Tundu lissu msomi aliyeasiliwa na siasa so uchambuzi wa Dr kilangi ni madhubuti
 
Yawezekana jambo hili likaisha kwa hasara kwa nchi yetu,lakini kwa kutokea kwake ni Mwanzo wa kuwa na msingi imara kusimamia maliasili zetu Siku zijazo.Pia ni jambo jema wajuzi wa mambo wanapotuelewa juu ya hili.La msingi ni kuungana na kupambana kwenye hii vita.Ndio maana mabepari wameungana kupitia vyombo vya mfano MIGA ili kutetea unyonyaji wao.Nasi tunapaswa kuungana kupigania tulipokosea
 
Wenzako wanachambua mambo kitalaam wewe unaleta ushabiki na ufia chama.
Hakuna cha utaalamu wala nini magufuli go ahead endelea kusimama na shareholders ripoti usiikabidhi management ya Acacia tuma mawakili wakaisome kwenye mkutano mkuu wa shareholders au ipeleke huko usiwape board wala management ya accacia. Findings zote wape shareholders
 
YEHODAYA mbona unaleta matusi ndugu yangu?Lete hoja ili mjadala upambe moto sio kumtukana mtu.
Usimjadili mtu mwenye kimo kifupi cha fikra. Yeye anachojua ni matusi na kushambulia watu. Umeona hoja yoyote ya maana toka kwake? Yaani kama sheria zinasema mchanga ni halali kwa ACACIA, halafu menejimenti yao ikawaibia wanahisa nao wakashtuka baada ya umbea wetu, sisi tutafaidika nini kama kila kitu ni chao? Au tutapewa posho ya Informer?
 
Ndio maana hawa waliotuingiza katika hili lidude wanajua jinsi linavyotisha mpaka akina muongo walibaki kumezea tu maana haligusiki kizembe zembe duuuh, aisee nyie wabunge wa ndio na viongozi wote mlioingia mikataba hii Mungu awaongezee umri mrefu ili muyaone mliyoyafanya
 
Maelezo ya Dr. Kilangi ni namna nyingine yenye ufasaha zaidi ya maelezo ya Mhe. Tundu Lissu. They have the same position. Na kwa maelezo ya Dr. Kilangi kweli hii ni vita, na mshindi wa vita anajulikana wazi kwa mujibu wa maelezo hayo ya Dr. Kilangi.

Kwa mtazamo wangu kabla ya kuanza vita, maelezo ya namna ya Dr. Kilangi yalitakiwa kutumika kwenye kupanga vita hii ili kuona kama kuna faida kubwa hasara kidogo au hasara kubwa faida kidogo. Pia ingesaidia kutoa options nyingi na kuchagua favourable option kama ingekuwepo kati ya hizo options.

Mimi ni mmoja wa watu tutakaopenda tusome 'kitabu' ili kupata mwanga zaidi. Kwani ili chapisho liitwe kitabu linakuwa na features zipi? Tena kitabu ndio kizuri zaidi kwani tutaona na references au bibliographies zaidi ambazo zitatusaidia tuone hoja zao kamili.
true. one and the same thing...
Lissu ameongea kama mwanasiasa.
Kilangi kama academician.
wamedeseana kidogo lakini - ila sijui nani kamdesa mwenzake!
 
Ni hivii?????? kwenye sayansi hakunaga majibu mawili ukifanya mfano quatitative analysis ya mineral flani ukishafikia mwisho na kusema labda 10kg ya dhahabu basi jibu ndio hilo. Hao waliochukua muda wao wameapa, na ni wataalamu walibobea kwenye fani hizo. Sayansi sio kama sheria muanze kuleta mambo ya " NEMO JUDEX IN CAUSA SUA" haipogo
Wewe sayansi umeisoma au umekaririshwa? Nani aliyekuambia sayansi haina majibu mawili? Hao waliokuandikia vitabu vya sayansi unavyotumia kukariri walikua na majibu zaidi ya mawili
 
Sawa mkuu ila mwisho wa siku tunataka mali zetu ziwe salama ma nchi yetu iwe salama.

Tumechoka kuibiwa.

Hakuna cha utaalamu wala nini magufuli go ahead endelea kusimama na shareholders ripoti usiikabidhi management ya Acacia tuma mawakili wakaisome kwenye mkutano mkuu wa shareholders au ipeleke huko usiwape board wala management ya accacia. Findings zote wape shareholders
 
Hao hawana tofauti na akina chief Mangungo sijui wa nini huko.

Ni aibu sana kwa huu upuuzi.

Ndio maana hawa waliotuingiza katika hili lidude wanajua jinsi linavyotisha mpaka akina muongo walibaki kumezea tu maana haligusiki kizembe zembe duuuh, aisee nyie wabunge wa ndio na viongozi wote mlioingia mikataba hii Mungu awaongezee umri mrefu ili muyaone mliyoyafanya
 
Wananchi wetu wanaangalia tu kama muvi! Wanacheka, wanalia, wanashangilia na wanabet! Yote kwa yote, kila mtu anatabiri hili picha kwa namna yake, hasa kwa kuegemea ktk mwisho anaoutaka yeye!

Binafsi nimemuelewa doctor-Loud and Clear!
Dokta ameandika vizuri sana tena bila kuonyesha siasa, na kama hili jina ni la Musoma, Kilangi basi ni ukoo mmoja na Muhongo, lakini huyu si ni Commissioner of Petroleum Upstream sijui madudu gani hata siyajui, huu ushauri nadhani atakuwa kamshauri Magufuli maana kateuliwa juzi tu kwenye uteuzi wa kina Mchwampaka
 
Hakuna kitu kaandika mtetezi wa wahuni tu huyo. Atuachie wazalendo tupambane yeye abaki na vifungu koko vya sheria alivyokariri kutetea mabeberu management ya Accacia.

Msomi Gani koko huyo asiyejua kuwa kilichokuwa kikifanywa na management ya accacia hakikuwa na baraka ya wanahisa wa Accacia? Ndio maana namuona kibaraka tu wa management ya accacia sio wanahisa wa accacia.

Management ya Acacia wamewaibia sana wana hisa wao subiri na ripoti ya makontaina waliyosafirisha miaka yote itoke wanahisa wapate taarifa yake. Huyu mwanasheria koko na wenzie akina lisu watatafuta shimo la kujificha. Mleta mada ni kati ya wanasheria finyu wasioangalia swala kwa upana wake.

Kabeba cv kubwa hewa. Kwa sasa wanahisa wako busy kuhakiki je kilichotoka Tanzania kiliwafikia kama kilivyo? Na je makontaina yaliyoondoka nchini yote yalienda kule kiwanda walichokubaliana au kuna yaliyochepushwa kwenda smelters zingine? Macho Ya wanahisa yote yako kwa magufuli wako naye asilimia 100 kwani wanataka ukweli ujulikane kujua kama management imewaibia au la.

Wakati wanahisa wako na magufuli wasomi sheria koko kama mleta maada wako na management ya accacia na wanapiga filimbi Ya hamelini kuitetea management. Mleta mada ona aibu nakala mpelekee tundu lisu na chadema. Hii vita tuachieni wazalendo nyie kaeni na mavyeti yenu koko ya sheria
acha uvivu wa kusoma,
 
Back
Top Bottom