Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Ni kauli ya Dkt. Khalid Salumu Mohamed, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapindizi Zanzibar (SMZ) aliyoitoa wakati akifungua rasmi mafunzo ya Dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa Maafisa Habari na Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Zanzibar, ambapo amewataka wanahabari hao kulinda taarifa kwakuwa zinathamani kubwa.
==================================
“Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inalenga kuhakikisha tunalinda Utu na Faragha na ni Sheria ambayo inazingatia katiba yetu”Haya ni maneno ya Dkt. Emmanuel Mkilia, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wakati akizungumza na Maafisa Habari wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Zanzibar kwenye hafla ya Uzinduzi wa Mafunzo ya siku moja ya Dhana ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa wanataaluma hao.
Pia soma:
~ Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC): Tunalinda Taarifa Binafsi ili zisiende kwenye mikono isiyo sawa
~ Je, unazifahamu haki zako kama mhusika wa taarifa binafsi?
~ Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) ishughulikie wanaosambaza taarifa zetu kiholela