Dkt. Gwajima: Wanaume wanaopigwa wawekewe utaratibu wao

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima ameiagiza Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, kuweka utaratibu wataalamu wanaume kutoka Idara hiyo kusikiliza na kupokea malalamiko ya wanaume wanaopigwa na kunyanyaswa.

Amesema sio kwamba wataalamu Wanawake hawawahudumii vizuri bali kusikilizwa na wanaume kunawafanya wawe huru kusema matatizo yao.

Akizungumza leo, Februari 2 na Waandishi wa Habari kuhusu vitendo vya ukatili katika jamii.

Waziri Dk. Gwajima amesema Wizara yake inataka ipate maoni ya kina baba wanaopigwa ili waweze kujua matatizo yao.

“Masuala ya wanaume yashugulikiwe na Wanaume naagiza Idara kuu wekeni wanaume katika kushughulikia matatizo hata kwenye choo kuna Me na Ke basi tufanye wahudumu wetu wawe mchanganyiko sisemi kwamba Wanawake hawawezi kusikiliza matatizo ya wanaume ile ni taaluma.

“Mambo ya kusikiliza mtu yanahitaji taaluma. Kwa wanaume sasa hivi nendeni kwa wanawake nendeni kwa wanaume ili tatizo lako liweze kutatuliwa,”amesema.
 
Wanaume hatuwezi kusikilizana, mfano mm nitakuwa nacheka sana Bora haohao wanawake wanahuruma ,huyu mama anaijua Psychology ya wanaume kweli? Babaangu tu siwezi kumwambia ndo nimwambie mtu nisiyemjua baadae tunakitana bar ananioneshea vidole.
 
Duh hapo kuna wanawake wa mkoa fulani watausika zaidi kwa malalamiko

Ova
 
Wanaume hatuwezi kusikilizana,mfano mm nitakuwa nacheka sana Bora haohao wanawake wanahuruma,huyu mama anaijua Psychology ya wanaume kweli??babaangu tu siwezi kumwambia ndo nimwambie mtu nisiyemjua baadae tunakitana bar ananioneshea vidole
Kwa wenye kuelewa hapo kazi imeisha
Watafute lingine
 
Huyu mwanamke mwenzetu naye! Matatizo ya wanawake yameshaisha mpaka arukie ya wanaume? Anajua kwanini historically wanawake watoto wamewekwa kuwa kundi special katika jamii? Anaijua vizuri ego ya mwanaume!?
 
mwanaume utajiona na mapungufu kisa kwenda kushtaki unadundwa na mkeo!naamini hamsa fil mia ya wanaume wanateswa sn na wake zao.wanaume muwe na mipaka na wake zenu bora iishie kwenye kunyimwa unyumba kuliko kipondo.kingine sijui kwanini wanaume wadogo dogo wembamba wanaoa madada makubwa unategemea nini km sio kichapo
 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima ameiagiza Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, kuweka utaratibu wataalamu wanaume kutoka Idara hiyo kusikiliza na kupokea malalamiko ya wanaume wanaopigwa na kunyanyaswa.

Amesema sio kwamba wataalamu Wanawake hawawahudumii vizuri bali kusikilizwa na wanaume kunawafanya wawe huru kusema matatizo yao.

Akizungumza leo, Februari 2 na Waandishi wa Habari kuhusu vitendo vya ukatili katika jamii.

Waziri Dk. Gwajima amesema Wizara yake inataka ipate maoni ya kina baba wanaopigwa ili waweze kujua matatizo yao.

“Masuala ya wanaume yashugulikiwe na Wanaume naagiza Idara kuu wekeni wanaume katika kushughulikia matatizo hata kwenye choo kuna Me na Ke basi tufanye wahudumu wetu wawe mchanganyiko sisemi kwamba Wanawake hawawezi kusikiliza matatizo ya wanaume ile ni taaluma.

“Mambo ya kusikiliza mtu yanahitaji taaluma. Kwa wanaume sasa hivi nendeni kwa wanawake nendeni kwa wanaume ili tatizo lako liweze kutatuliwa,”amesema.
Ni aibu kubwa kumwambia mtu yoyote kuwa unapigwa na mkeo.

Ni aibu kubwa sana kumwambia mwanaume mwenzio kuwa mkeo anakupiga nyumbani.

NB.
Never marry a woman with big feet.
 
mwanaume utajiona na mapungufu kisa kwenda kushtaki unadundwa na mkeo!naamini hamsa fil mia ya wanaume wanateswa sn na wake zao.wanaume muwe na mipaka na wake zenu bora iishie kwenye kunyimwa unyumba kuliko kipondo.kingine sijui kwanini wanaume wadogo dogo wembamba wanaoa madada makubwa unategemea nini km sio kichapo
Unakuta jamaa ana vipumbu vidogo vidogo lakini anajitutumua kuoa jimama la miraba minne la kinyakusa lazima apigwe tu
 
Kuanza kumuadithia dume mwenzako kuwa kila siku unapigwa na mwanamke yataka moyo
 
Hivi mwanaume unapigwaje na Mwanamke kiumbe dhaifu kuliko wote kama sio uchoko ni nini??
 
Muombe radhi mama yako mkuu....unamaanisha alikuwa dhaifu sana kukubeba miezi tisa na kukusukuma utoke uje duniani?

I wish kungekuwa na kodi ya mdomo,ingesaidia sana.
 
Back
Top Bottom