Dkt. Dorothy Gwajima: Kama unataka nitumbuliwe ili uchukue nafasi yangu, fanya kazi zaidi yangu sio ufitini

Mh....wewe naona hoja zako ni dhaifu dhaifu ( In Prof Assad Voice).

Yaani umesahau kuwa waliotuhumiwa kuchota fedha za Escrow ni mawaziri.?Ndo maana nasema wizi upo kila mahali na ni kosa la jinai.

Majukumu ya waziri ni kutengeza sera nzuri na mifumo mizuri ya usimamizi ili dawa zimfikie mlaji wa mwisho na vile vile kuongeza morali wa kazi na ubunifu kwa mtoa dawa.
Kwani sera na mifumo ya kufikisha dawa kwa mlaji hazipo? Tatizo siyo sera na mifumo, tatizo ni kwamba nyie ni WEZI. Badilikeni muache wizi muone kama dawa hazitamfikia mlaji!
 
Mwacheni atekeleze majukumu yake. Ni mfuatiliaji wa karibu. Yafaa hata kuwa rais ajae. Hadangayiki.
 
Katika sekta ambazo zilikuwa na huduma mbovu kwa muda mrefu ni hii ya Afya.

Yeyote atayeiboresha atakuwa amefanya jambo jema sana.

Watu wengi wanamalalamiko yao juu ya madaktari na wauguzi, unakuta mgonjwa hatakiwi kufanyiwa jambo flani kulingana na ugonjwa wake ila daktari anafanya kwa tamas zake, ethics hakuna kabisa.

Mimi naona inahitajika nguvu kubwa mno kuishape sekta ya afya hapa nchini.
 
Kiukweli huyu mama style yake ya uongozi inashangaza. Naona anawagawa watumishi badala ya kuwaunganisha.

Hili ni tatizo kubwa!
Kutafuta lugha mwororo ya kumshugulikia mwizi inataka kipaji.
Juzi ameenda wilayani, wamekuwa wakikusanya milioni 24 kabla ya mfumo.

Wameweka mfumo leo hii wakikusanya Million 790.
Tofauti ya karibu millioni 760. Makusanyo haya ambayo haya kukusanywa bila ajizi hii million 960 ilikuwa inaibiwa tuu.

Kwa wizi wa namna hii kiongozi lazima UCHANGANYIKWE.
 
Acha maza aendelee kutuburudisha kwa vichambo.

Nampenda huyu mama kwa staili yake ya kuongea.

Madaktari mtanyooka tu na mimi nasema awanyooshe tu cumamae zenu maana hakuna namna nyingine.

Lugola alikua ananinyooshea polisi, huyu mama amekuja kuwanyoosha madaktari. Safi sana.
Huyu mama ni Mlokole na anefunga kila jumanne, mama wa mikesho, hii michambo kajifundishia wapi ?.
 
Ili useme dawa haziibwi lazima uwe na ushahidi wa amekunywa nani.
1. Ziwe ziliingia stoo ya dawa na kurekodiwa kwenye kitabu husika.
2. Zinapotoka zionekane kumbukumbu za aliyeomba na aliyepokea.
3. Zinapoenda kwa mgonjwa risiti ya mgonjwa aliyepewa iwepo nakala moja kituoni na ingine aende nayo mgonjwa.

Hivi ni vitu muhimu. Sasa vituo vingi hicho cha pili na cha tatu havipo. Unaweza kusema nini hapo. Je unaweza kwenda benki ukaweka hela ukaondoka bila risiti?? Sasa inakuwaje mgonjwa apewe dawa asipewe risiti??

Huyu mama hamtamshinda kwa kelele. Kwanza asili yake hanaga hata muda wa kujadili vitu ambavyo havina data.
 
Typical behaviour ya Wasukuma, there is no wonder kwa tuliosoma nao na kuishi nao.. kwa usaliti ndio wao na tulipokuwa shuleni tulikataa kuwashirikisha waskuma katika KUNJI, watakusaliti tu! (Wasukuma mlio tofauti mnisamehe)
 
Akiendelea hivi atatumbuliwa madaktari Ni watu muhimu sio vizuri kuwazalilisha bila kutumia ustaarabu.
Huyuu kapaniki kuwa waziri bado wenge la kuwa waziri halijamuisha.

Akiendelea hivi lazima kamgoma baridi na hujuma katokee.
Mtaani tuna vijana kibao hawana ajira
 
Binafsi namuona kama baadhi ya nati zimelegea kichwani mtu gani anaongea hana mpangilio wa maneno.
Ni kweli mkuu hata Mimi ananitia mashaka utakuta akianza kuongea sentesi mwisho inakaa ya kwanza na ya kwanza inaenda mwisho mikwara mingi ni heli awe anafanya vitendo zaidi kuliko maneno asiyoyaweza,ukimcheki alivyojitoa ufahamu kama mzee wa mwibara basi naona kama heshima ya udokta inashuka kabisa.
 
Mleta hoja muogope Mungu wewe ni dhahiri kwamba ni mwizi wa madawa.
Umeandika ki majungu na kifitinishi zaidi.
Kwani huyu mama anapoongea huwa anaongea bila uthibitisho wa WIZI?
Jibu ni kwamba huwa anakamata ndio anaanza kuonya.
Wezi wa madawa mmetuulia ndugu zetu kwa muda mrefu.
Sasa amekuja game changer na hakuanzia baada ya kuteuliwa uwaziri bali alianza tangu akiwa katibu wizarani clips zipo.
Acheni majungu na ufitinishi.
Badilikeni wezi nyie.
MUNGU anawaona.
 
Huyu mama amegeuka mwimba taarabu,sikubaliani hata kidogo na watendaji Wa serikali wanaokiuka miongozo ya kanuni na maadili ya utumishi Wa umma kwa kuwavuruga watumishi Wa umma huku wakidhani kuwa kufanya hivyo ndo utendaji kazi bure kanisa

Tabia kama hii alikuwa nayo mkuu Wa mkoa Wa Lindi ndugu Zambi

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Kutafuta lugha mwororo ya kumshugulikia mwizi inataka kipaji.
Juzi ameenda wilayani, wamekuwa wakikusanya milioni 24 kabla ya mfumo.

Wameweka mfumo leo hii wakikusanya Million 790.
Tofauti ya karibu millioni 760. Makusanyo haya ambayo haya kukusanywa bila ajizi hii million 960 ilikuwa inaibiwa tuu.

Kwa wizi wa namna hii kiongozi lazima UCHANGANYIKWE.
Anachofanya ni Sawa na kuwachapa viboko hadharani. Naona sio sawa.

Itapendeza Sana akitumia kanuni na miongozo ya utumishi wa umma kuwashughulikia wezi na matapeli.
Hilo tu.
 
Jibuni hoja acha nalalamiko yaliyojaa kashfa.
Mimi namfuatilia na yupo sahihi. Dawa zinaibiwa sana.

CHAPA KAZI BIBIE. MPAKA TUJUE DAWA ZINAENDA WAPI...
Aunde kamati maakumu ichinguze dawa zinaibwaje na ni njia gani itumike kuthibiti hilo tatizo
 
Back
Top Bottom