Dkt. Bashiru: Wakulima ni lazima muwafanye Watawala wawaheshimu, msikubali kuburuzwa na Wanyonyaji wachache

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,137
Najiuliza Huyu Dkt. Bashiru ni mjamaa? Maana wajamaa ndio hupenda kutumia hili Neno Wanyonyaji

Wakati wa Nyerere tuliimba
"Mabepari walia kukatiwa mirija ya unyonyaji walipotangaziwa Azimio la Arusha"

Dkt. Bashiru amesema Wakulima ndio wanawalisha Watawala hivyo ni lazima wawafanye wawaheshimu wasikubali unyonyaji

Labda angeyasema awamu ile angeeleweka zaidi lakin CCM back ni ile ile

Mungu ni mwema!
 
Unaweza kudhani labda enzi za Jiwe wakulima walinufaika na chochote kumbe Ni mpumbavu tu.

Wakulima wapi wanaoweza kubali kurudi zama za Jiwe?

Bora hata angeishia hapo ila kuwacjochea kufanya uasi na eti wasishukuru au kupongeza hatua za Serikali za kuwasaidia ikiwemo mbolea na kuwahakikishia soko kwake Ni nongwa.
 
Ndani ya CCM bado kuna wajamaa na wazalendo wa chache sana kama wakina Dkt Bashiru.

Babeli itakuja na mkombozi Atatokea umo umo ndani yao.

Najua Magufuli hayupo lakini kweli yupo Magufuli mwingine Ataibuka miongoni mwao naye Atatufikisha kwenye Nchi ya Ahadi.

Vilio vimekua vingi na watawala wameziba masikio. Wanapenda kusikia wanayoyapenda na sio wasiyoyapenda.

Maisha yamezidi kuwa magum sana kwa watanzania Leo elf 10, kwa familia ya watu 3 haitoshi?

Waliokua wanajitafutia Riziki zao wamefukuzwa kwa kuitwa wachafuzi wa mazingira na hao wamerudi majumbani familia zimepoteza Riziki.

MUNGU saidia watu wako.
 
Ujamaa ni falsafa iliyo na mkanganyiko mkubwa sana, inahitaji mwanachama wake awe na moyo shupavu sana kuweza kuitekeleza.

Sifa kuu na nambari moja ya mtu kuweza kutambulika kama ni mjamaa halisia ni lazima awe"EGALITARIAN” kama muumini wa hii falsafa hajitanabaishi hivyo basi huyo sio mjamaa halisia bali bepari aliye jificha katika kichaka cha ujamaa.
 
Back
Top Bottom