Rais Magufuli na Dkt. Bashiru Ally ni hazina za chama na nchi, tuzitunze. Tusikubali watumiwe kama mtaji wa kisiasa na upinzani

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,486
4,408
Katika zama hizi kupata viongozi kama Rais Magufuli na Dkt. Bashiru Ally ni nadra sana na ni bahati kubwa sana. Ni viongozi wajamaa wanaojali sana utu, haki na usawa katika jamii. Kama inavyosemwa’ ujamaa ni imani’ ya kujali misingi ya utu, haki na usawa na ni jambo la kushukuru ndani ya Tanzania kuna viongozi wajamaa wanaoiishi misingi hiyo.

Kulikuwa na wajamaa kama Mwalimu Nyerere, Edward Sokoine, Mzee Kawawa na wengine ambao walifanya kazi nzuri ya kusimamia misingi na baada ya kazi hiyo wametwaliwa kwenda makao yao ya milele ila kazi zao zimetunzwa na kuenziwa. Zama za wajamaa kama Mzee Mangula na Mzee Malecela zinaelekea ukingoni kutokana na umri wao kuwa mkubwa sana lakini licha ya kwamba umri wao umesogea sana bado nchi ina hazina kubwa ya viongozi wa Kariba yao. Rais Magufuli na Dkt. Bashiru Ally ni wachache kuwataja wenye sifa, Imani na mienendo ya kujali utu, haki na usawa kama misingi ya ujamaa.

Kauli, mienendo na vitendo vya viongozi hao ni ishara tosha ya kuiva katika ujamaa na misingi yake. Ni ukweli usiopingika kuwa viongozi hao wana sifa moja kubwa inayofanana nayo kuwa waadilifu na kutohusika na vitendo vinavyotia shaka. Na haya ndio matokeo halisi ya kuwa mjamaa ni uadilifu usiotiwa shaka. Mjamaa ni muadilifu wa maneno( kauli), mienendo na vitendo vyake.

Uadilifu huo wa kauli, mienendo na vitendo ambazo ni sifa kubwa ya hao viongozi wetu ni hazina kubwa sit u kwa CCM bali kwa serikali na Tanzania, tuzitunze. Lengo la kutunza hazina hizo ni kuweka kumbukumbu ya nini walifanya, nini walijaribu kufanya ili vizazi vijavyo wajifunze kutoka kwao. Uadilifu wao ni historia nzuri ya Tanzania.

Hazina hii ni muhimu kwa Tanzania ya sasa nay a baadaye, hivyo sisi watanzania tusikubali watumiwe kama mtaji wa kisiasa wa upinzani. Tuilinde wasichafuliwe na siasa za mizengwe za upinzani pale wanapokosa agenda na kufanya hazina hizo kuwa mitaji yao ya kisiasa.
 
Jiulize kama wao ni hazina ya chama, kwanini wakubali kutumika kama mtaji na wapinzani?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom