Dkt Bashiru USO kwa USO na Manyanguro wa Kimasai Monduli

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Dkt.Bashiru Ally ameitaka jamii ya kifugaji ya kabila la Kimasai kupitia viongozi wao wa Kimila(Laigwanani) kuendelea kuenzi mila na tamaduni zao nzuri kwa kuwekeza kwenye elimu kama mtaji pekee utakao ikomboa jamii hiyo.


Kauli hiyo ameitoa jana katika sherehe za Kimila za kabila la kimasai za kuwatoa kwenye rika vijana maarufu kwa jina la Nyanguro ,ambao ni zaidi ya 300 kutoka Mikoa ya Arusha,Manyara,Kimanjaro na Nchi jirani ya Kenya ,kuweza kubarikiwa waweze kuoa,zilizofanyika katika kata ya Sebeko wilaya ya Monduli ,Mkoani hapa.


Dkt Bashiru alisema kuwa Tanzania haina Kabila bali inamakabila yenye haki sawa na hakuna kabila bora kuliko jingine lakini ni lazima kuheshimu Mila na desturi nzuri za makabila hayo.


"Namna pekee ya kudumisha Mila na tamaduni zetu nzuri kwa jamii zetu ni kuwasomesha watoto wetu wote wakike na kiume na viongozi wa kimila ,Laigwanani waendelee kuhamasisha jamii za kufugaji kuwekeza kwenye elimu " Alisema


Aidha alisisitiza kuwa Tanzania inaheshimu watu wake wenye dini na wasio na dini ,na kutoa rai kwa wasio na dini wasilazimishwe kufuata dini yoyoye na ukiona mtu anakulazimisha ujue huyo ni

tapeli.


Katika hatua nyingine Dkt Bashiru aliwataka wananchi kuachana na wanasiasa uchwara wenye nia ovu ya kutaka kuchonganisha wananchi na mataifa yao kwa nia ya kujijenga kisiasa kwa masilahi yao binafsi na kuwataka wananchi kuendelea kushikamana kwa umoja wao ili kulinda amani iliyopo.


Awali Mkuu wa Laigwanani,Elikisongo Meijo alitaka Mila ya kimasai kuachwa huru bila kuingiliwa na Madhehebu ya dini kwa kuwa wao wanaheshimu dini zao na hawajawahi kuingilia imani ya mtu yoyote.


"Sisi atuingilii dini ya Mtu wala kabila la mtu yoyote hivyo na sisi hatutaki kuingiliwa na mtu yoyote" Alisema Elikisongo


Aliitaka serikali kuwasaidia ili madhehebu ya dini yanayoweka makanisa ya mahema na kuwarubuni wananchi wa jamii hiyo ili kuachana na Mila zao,jambo hilo linaashiria uvunjifu wa amani na kutaka dini zifuate taratibu za kuendesha makanisa yao na si kurubuni watu.


Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalumu,Mkoa wa Arusha,Amina Mollel (Ccm)alisema jamii ya wamasai ndio iliyobaki hapa nchini inayodumisha na kujivunia utamaduni wake,hivyo alitaka kabila hilo liendelee kuenziwa kwa kuwa linaliletea heshima taifa kwa watalii wanaoingia nchini na kufurahia tamaduni zao.


Alitaka akinamama wa kabila hilo la kimasai wanaokabiliwa na changamoto ya Ukosefu wa maji safi kusaidiwa ili kuhakikisha wanasogezewa Huduma hiyo ili waache kufuata Huduma ya maji umbali mrefu.

IMG_20190706_150836.jpeg
IMG_20190706_132757.jpeg
IMG_20190706_132812.jpeg
 
Back
Top Bottom