Dkt. Bashiru asema Jimbo la Mbowe(Hai) si ngome ya CHADEMA

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally ametaja sababu ya ziara yake mkoani Kilimanjaro kuanzia Wilaya ya Hai lilipo jimbo la Hai ambalo mbunge wake ni mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Amesema ameanzia Hai kimkakati kwa maelezo kuwa jimbo hilo si ngome ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Julai 7, 2019 katika kikao cha ndani kilichofanyika katika uwanja
wa Sabasaba.

"Katika Mkoa wa kilimanjaro nimepanga kupita wilaya kwa wilaya kwa sababu ya uzito na umuhimu. Nimeanzia Hai kimkakati na mahesabu yametumika kuamua kuanzia Hai katika ziara yangu," amesema Dk Bashiru.

Katibu mkuu huyo ametoa maelekezo kwa mabalozi kupewa nafasi katika mikutano pindi wanapofika viongozi wa kitaifa mikoani.

Naye katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya, amesema mwaka 2015 chama hicho kilipoteza majimbo kadhaa mkoani Kilimanjaro kutokana na makundi baada ya kumalizika kwa kura za maoni.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, CCM iliibuka na ushindi katika majimbo mawili kati ya tisa mkoani humo na madiwani 52 kati ya 169.
 
Wananchi wa hai wapo kimya tu, wanasubiri wakati muafaka, huwezi kumpiga nyoka kama bado yupo ndani ya shimo mpaka atoke ndiyo unaponda kichwa
 
Wananchi wa Hai wameshamchoka Mh. Mbowe. Ni miaka sasa, haijulikani amefanya nini jimboni kwake. Sasa hivi ni bendera za CCM zinapepea kila mahali. Kama Mbowe ana akili ameshajua muda na majira yake yameshaisha.
 
Katika Mkoa wa kilimanjaro nimepanga kupita wilaya kwa wilaya kwa sababu ya uzito na umuhimu. Nimeanzia Hai kimkakati na mahesabu yametumika kuamua kuanzia Hai katika ziara yangu

tehteh narudia tena kwa sababu ya uzito na umuhimu.
 
Wananchi wa Hai wameshamchoka Mh. Mbowe. Ni miaka sasa, haijulikani amefanya nini jimboni kwake. Sasa hivi ni bendera za CCM zinapepea kila mahali. Kama Mbowe ana akili ameshajua muda na majira yake yameshaisha.
Watu wa Hai wana akili wewe usiwafananishe na wala viwavi jeshi.
 
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally ametaja sababu ya ziara yake mkoani Kilimanjaro kuanzia Wilaya ya Hai lilipo jimbo la Hai ambalo mbunge wake ni mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Amesema ameanzia Hai kimkakati kwa maelezo kuwa jimbo hilo si ngome ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Julai 7, 2019 katika kikao cha ndani kilichofanyika katika uwanja
wa Sabasaba.

"Katika Mkoa wa kilimanjaro nimepanga kupita wilaya kwa wilaya kwa sababu ya uzito na umuhimu. Nimeanzia Hai kimkakati na mahesabu yametumika kuamua kuanzia Hai katika ziara yangu," amesema Dk Bashiru.

Katibu mkuu huyo ametoa maelekezo kwa mabalozi kupewa nafasi katika mikutano pindi wanapofika viongozi wa kitaifa mikoani.

Naye katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya, amesema mwaka 2015 chama hicho kilipoteza majimbo kadhaa mkoani Kilimanjaro kutokana na makundi baada ya kumalizika kwa kura za maoni.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, CCM iliibuka na ushindi katika majimbo mawili kati ya tisa mkoani humo na madiwani 52 kati ya 169.
Kwa utaratibu wa sasa wa uchaguzi Majimbo yote ni mali ya ccm kwani ni suala la kuagiza Wakurugenzi na Tume
 
Kama CCM inajiamini, basi iachie siasa huru, mikutano/kampeni kwa vyama vyote; halafu tuone nani atashinda.

Kwa hali ya sasa, majimbo yote ji mali ya CCM kwa mbinu za hila na wizi wa kura!
 
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally ametaja sababu ya ziara yake mkoani Kilimanjaro kuanzia Wilaya ya Hai lilipo jimbo la Hai ambalo mbunge wake ni mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Amesema ameanzia Hai kimkakati kwa maelezo kuwa jimbo hilo si ngome ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Julai 7, 2019 katika kikao cha ndani kilichofanyika katika uwanja
wa Sabasaba.

"Katika Mkoa wa kilimanjaro nimepanga kupita wilaya kwa wilaya kwa sababu ya uzito na umuhimu. Nimeanzia Hai kimkakati na mahesabu yametumika kuamua kuanzia Hai katika ziara yangu," amesema Dk Bashiru.

Katibu mkuu huyo ametoa maelekezo kwa mabalozi kupewa nafasi katika mikutano pindi wanapofika viongozi wa kitaifa mikoani.

Naye katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya, amesema mwaka 2015 chama hicho kilipoteza majimbo kadhaa mkoani Kilimanjaro kutokana na makundi baada ya kumalizika kwa kura za maoni.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, CCM iliibuka na ushindi katika majimbo mawili kati ya tisa mkoani humo na madiwani 52 kati ya 169.
Haaa! CCM wana kila kitu lakini bado wako eti kimkakati zaidi ''Kobe amelala'' akiamka hiyo mikakati yeyu itageuka kuwa hewa ''A reward in business comes after beating your competitor''
 
Back
Top Bottom