Hii Dunia ni ndogo sana hawa DKT BASHIRU ALLY na POLEPOLE walifikiria watakuwa viongozi wa maisha.
- Ilifika wakati walikuwa wanatoa hongo na kununua wapinzani hasa wabunge na madiwani.
- Waliahidi vyeo kwa wapinzani wanaokuja CCM bila kujali uwezo wao na nchi kwa ujumla
- Walirekodi kwa kudukuwa simu za Raia binafsi ilimradi tu kwa wao waliowaona kama wapinzani. Hizi rekodi za simu zao ni bila kufuata sheria! lakini walitoa maaagizo hayo
- Waliharibu uchaguzi wa Tanzania 2020 kwa kutoa maelezo kwa polisi na usalama waibe kura tena waziwazi
- Walitaka nchi yetu isiwe na vyama vya upinzani kabisa kinyume na sheria
- Walitaka turudi kwenye ujamaa na kujiweka karibu ya vyama vya kikandamizaji vya China
- Waliwadharau Madaktari na kuweka kampeni zisizo na tafiti kwenye Corana mpaka tukapoteza viongozi wengi wa juu
- Wapinzani walikuwa maadui mpaka kupigwa risasi na vikosi vya usalama wa taifa vya siri.
Dunia tenda wema Sasa Kinana karudi, Magufuli kafariki, Membe kasamehewa, Ridhiwani waziri, Nape waziri na Makamba waziri!!!