Dkt. Abbas ataja sababu za mradi wa SGR kuchekewa

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,

Katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbas.

Dodoma. Serikali imesema mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) umechelewa kukamilika kwa sababu ya mvua zinazoendelea kunyesha nchini, na si ukosefu wa fedha kama baadhi wanavyodai.

Februari 13, Serikali ilitiliana saini na benki ya Standard Chartered kukopeshwa Sh3.3 trilioni kwa ajili ya awamu ya pili ya ujenzi wa mradi huo kutoka Morogoro hadi Makutopora.

Jana, katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbas alisema kipande cha reli kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kilipangwa kukamilika Desemba mwaka jana na kwamba hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 75.

Alisema ujenzi wa kipande cha Morogoro hadi Makutopora uko asilimia 28.

Alisema gharama zilizotumika hadi sasa katika ujenzi huo ni Sh2.95 trilioni ambazo ni fedha za ndani.
“Kuna watu wamesikia juzi tu kuna mkopo tunakopa kumalizia kidogo, tayari wameshaanza kusema kuwa mradi umewashinda. Brother tulia mradi tunautekeleza kwa fedha za ndani na tutaendelea kutekeleza kwa fedha za ndani na hizo fedha zikitoka tutatumia,” alisema.

Abbas, ambaye alitakiwa na Rais kuendelea na jukumu la Msemaji Mkuu wa Serikali, alisema hivi karibuni watatangaza zabuni ya ujenzi wa reli hiyo katika kipande cha kuanzia Mwanza, kupitia Isaka hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Alisema ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro na Morogoro hadi Makutopora sasa utakamilika ndani ya mwaka huu.

Aidha, Dk Abbas alisema makatibu wakuu na manaibu wao watafanya ziara ya siku mbili kutembelea utekezaji wa mradi wa SGR.

Kuhusu mradi wa kufua umeme wa maji katika Mto Rufiji, alisema daraja ambalo litatumika kwa ajili ya kuchepushia mto limekamilika kwa asilimia 100.

Hata hivyo, alisema kilichobakia ni matengenezo madogo ya kujenga kuta na matoleo katika daraja hilo.
Alisema katika mradi huo hadi sasa zimetumika Sh1.275 trilioni kati ya Sh6.5 trilioni zitakazogharamia ujenzi wa mradi huo.

Alisema maandalizi ya ujenzi wa bwawa hilo yanatarajiwa kuanza wakati wowote baada ya kukakamilika kwa ujenzi wa daraja la kuchepushia mto.

Dk Abbas alisema Machi mwaka huu wanatarajia kufanya uzinduzi wa eneo maalum kwa ajili ya matengenezo ya meli (mradi wa cheleza) katika Ziwa Victoria.

Kwa mujibu wa Dk Abbas, ujenzi wa mradi huo hadi sasa umefikia asilimia 90 na unatekelezwa kwa gharama za Sh32 bilioni.

“Wakati tukitarajia kuzindua mradi huu mwezi wa tatu, tunafanya ukarabati wa meli kubwa mbili. Ya kwanza ni MV Victoria ambayo hadi sasa asilimia 89 tumetumia Sh14 bilioni kati ya Sh22 bilioni ambazo zitatumika,” alisema.

Alisema meli nyingine inayokarabatiwa ni MV Butiama ambayo ukarabati wake umefikia asilimia 86 na umetumia Sh4 bilioni hadi sasa.

Pia Dk Abbas alisema wanaunda meli kubwa Ziwa Victoria ambayo utengenezaji wake umefikia asilimia 52.
 
Asante taarifa. Usiache kutupatia na taarifa ya mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima - Uganda kwenda Tanga - Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom