Unafikiri kuwa Rais ndio kujali maslahi ya wananchi?au kuwa Mbunge ndio kutokujali hali za wananchi?
Siku zote usiwe mwepesi kutafsiri maneno ya mtu ikiwa huelewi maana. Upumbavu ni pamoja nadhania mtu mwingine anafikiria nini ama alikuwa na maana gani.. kama hujui Uliza mkuu wangu sii dhambi wala haikufanyi wewe mjinga.
Huwezi kugombea Urais ikiwa hujali maslahi ya wananchi wako. hili sii swala la kufikiria hata kidogo ila kiongozi anaweza kuwahadaa wananchi kwamba anawajali kinyume cha imani yake..Sidhani kama Dr Slaa ni mtu wa aina hiyo na ndio sababu nilitegemea zaidi kugombea kjwake kuliko mtu mwingine yeyote.
Pili, Sikusema kuwa Ubunge ni kutojali hali ya wananchi isipokuwa niimani yangu kwamba mbunge hawezi badilisha kitu kwa kuzingatia hali halisi ya watu na mazingira ya uchaguzi huu. Tanzania ya leo inahitaji Mapinduzi na sii kugombea Ubunge ambao bado upo chini ya utawala wa katiba ya chama kimoja. Changes zinaanza kabla ya uchaguzi na kiti cha Urais ndicho kinalinda machungu yote.
Ikiwa mgombea yeyote anapinga muundo wa katiba iliyopo, lakini bado akagombea ubunge chini ya katiba ile ie anayoipinga kuwayanyasa wananchi, basi bila shaka Mgombea huyo kajiunga na utawala mbaya. Sidhani kama Mandela angekubali kujiunga na Uchaguzi mkuu wa South Afrika hata Ubunge chini ya Utawala wa Apartheid..Na kwa wale wote waliokubali kujiunga na kufanikiwa hutokea siku watakayo amua kumwondoa rais..Kenya ni mfano mdogo mzuri sana kwa awamu zote..Walijipanga kumwondoa Moi wakaweza kubadilisha katiba yao lakini majuzi tu kina Raila walipokubali ubunge wa majimbo na sii utawala wamejikuta ktk hali ngumu zaidi. wajaluo leo wapo ktk wakati mgumu kuliko wakati wowote na juhudi zao zimegota ukutani.
Sasa wewe nambie, huyo Dr. Slaa akirudi bungeni atawezesha kipi ikiwa CCM wataendelea kutawala. Hivi kweli unaamini kabisa kwamba CCM inaweza shindwa ktk uchaguzi ambao wao wenyewe ndio mahakimu? Unatumia kigezo kipi haswa..
Dr.Slaa bila shaka atashinda hili halina Ubishi lakini CCM nao wanabadilisha wagombea wake wengi sana kwa kutumia kura za maoni. wasiopendwa wataenguliwa mapema na kilichobakia ni mchele unaweza kuuzika! Kisha wanatumia wanawake zaidi kupata ushindi kwani wapiga kura wengi ni wanawake na unajua fika hii habari ya uuwiano ktk madaraka ni hadithi mpya. Tatizo la wanawake lipo ktk vyama vya upinzani, kama lilicyokuwa la udini mwaka 2005, hivyo tumepigwa tayari bao la kwanza..
Kwa njaa ya Mtanzania wagombea wengi wameisha anza kulisha sumu ya utajiri wao -Takrima. Na wenye uwezo mkubwa ni wagombea wa CCM..Matajiri wengi wako CCM na hakuna tajiri atakaye changia Chadema,Nccr wala CUF akaachwa na hasira za CCM..huu ndio ukweli na matajiri wote wanafahamu hilo, hivyo huo uwazi wa michango ni mtego mkubwa kwa wapinzani kwa hesabu Wabunge wengi CCM wapo kwa maslahi yao binafsi.. hili pia halina Ubishi.