Majukumu ya uraisi ni mengi ni zaidi ya kujua lugha 7,lakini kila kitu kina mwanzo,kazi nzuri aliyoifanya akiwa mbunge n.k.Ila serikali ni zaidi ya kuwa na raisi mwadilifu,bado kutakuwa na baraza la mawaziri.Isitoshe kuna bunge kujadili na kupitisha miswaada,haitakuwa kazi rahisi ukichukulia CCM itakuwa na idadi kubwa ya wabunge, kazi ngumu kweli kweli.Bado atakuwa anawajibika kwa chama chake CHADEMA.Wananchi watakuwa na matarajio mengi na itakuwa ngumu kuyatimiza kwa muda mfupi.