Dk. Slaa, Lema wanusurika kusota rumande | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa, Lema wanusurika kusota rumande

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by lifeofmshaba, Jun 1, 2011.

 1. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  UPEPO wa kuswekwa rumande jana nusura uwakumbe Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa na Aquelini Chuwa mkoani Arusha baada ya polisi kutaka kuwakamata walipokwenda kujisalimisha mahakamani.

  Wiki iliyopita Mei 27, Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha Charles Magesa alitoa
  amri ya kukamatwa kwa Lema, Dk. Slaa, Freeman Mbowe, Philemon Ndesamburo na Josephin Slaa kwa kushindwa kuhudhuria mahakamani bila ya taarifa yoyote na kuamuru polisi kuwakamata popote walipo.

  Sakata hilo lilianza saa 8.15 mchana wakati watuhumiwa hao waliporudi mahakamani saa
  saba baada ya kufika saa 3 asubuhi na kuambiwa kurudi muda huo.

  Baada ya kukaa kwa muda wa saa 1.15 mawakili wa washitakiwa hao Method Kimomogolo na Albart Msando walimwona Hakimu Mfawidhi kumjulisha kuwa watuhumiwa Lema na Slaa walikuwa nje na walikwenda kujisalimisha, hatua iliyopingwa na Hakimu Magesa.

  Kwa mujibu wa Msando, Hakimu Magesa alisema yeye alishatoa amri ya watuhumiwa wote
  kukamatwa kwa kudharau mahakama wao na wadhamini wao hivyo kilichotakiwa ni kukamatwa na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi na baadayekuletwa mahakamani.

  Wakili Msando alisema, sababu hiyo iliungwa mkono na Wakili wa Serikali Mwandamizi EdwinKakoraki na kupiga simu polisi kuwaita ili wawakamate Lema, Slaa na Chuwa ili waende
  kwanza rumande na baadaye kuletwa mahakamani kujibu shitaka la kuidharau mahakama.

  Muda mfupi tu magari mawili ya polisi yaliwasili yenye namba za usajili PT 1177 na PT 1414
  yakiwa na askari wasiopungua 12 huku wakiwa na silaha tayari kuwapeleka watuhumiwa hao rumande.

  Ubishi ulizuka kwa Dk. Slaa na Lema kugoma kwenda polisi na kudai kuwa wao wamekwenda
  wenyewe mahakamani kujisalimisha baada ya kutolewa hati ya wao kukamatwa “hivyo
  mwenye mamlaka ya sisi kukamatwa kwenda rumande ni hakimu mwenyewe na sio nyie polisi hapa hatuondoki,” alisema Dk. Slaa.

  Wakati malumbano hayo yakiendelea mawakili wa washitakiwa walikuwa katika chumba cha
  hakimu Magesa wakimsihi asikilize sababu za watuhumiwa kujisalimisha; alikubali kusikiliza
  hoja zao.

  Alisikiliza hoja za upande wa utetezi kuhusu kutokufika mahakamani kwa wateja wao na kutolewa sababu mbalimbali, lakini upande wa serikali uliomba muda kupitia uhalali wa vyeti kwa watuhumiwa ambao walidai kwamba walikuwa wagonjwa.

  Hakimu huyo aliahirisha kesi hiyo hadi leo saa 7 mchana ili asikilize sababu za wakili wa serikali na kutoa uamuzi wa jumla ya juu ya kufuta dhamana na kutofuta dhamana kwa washitakiwa kwa kukiuka kuhudhuria mahakamani bila ya sababu za msingi.


  maoni: huyu hakimu anatimiza majukumu yake au majukumu aliyotumwa, watu wameshafika mahakama kwenda rumande ni suna
   
 2. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,682
  Likes Received: 637
  Trophy Points: 280
  Ukishindwa kwenda mahakamani,na hakimu akakataa sababu iliyokufanya ushindwe kwenda mahakamani...
  Unatakiwa uripoti polisi kama warrant imekuwa issued,siyo mahakamani.
   
 3. n

  nitasemaukweli Member

  #3
  Jun 1, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr Slaa na Lema wakienda jela na mkapa na kikwete wapo mtaani kweli tutaona justice ya Tanzania ikonja damu kwa mara ya kwanza, one word jaribuni tu muone.
   
 4. O

  Omr JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwendo mdundo kijana, bora wajenge nyumba karibu na mahakama. Na kama wana mikutano yeyote basi watafute sehemu karibu na mahakama. Nyie CDM mtapiga kelele lakini mwisho mtanyamaza...CCM ndio Tanzania na wavuta bangi wachache wala hawata sumbua CCM.
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Pole sana dada! CDM hawapigi kelele ila wanasimamia sheria. Ule wakati wa kuonewa na kunyanyaswa kwa kutokuifahamu sheria umeshapita.
  Halafu ccm sio Tanzania, wala Tanzania sio ccm hata siku moja. Tanzania ni nchi ya watu zaidi ya 45 milion wakati ccm ni chama cha watu wasiofika hata 5milion! Note, Tanzania ilikuwepo kabla ya ccm na ccm inakaribia kufa wakati Tz itakuwepo milele!
   
 6. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,163
  Likes Received: 1,122
  Trophy Points: 280
  another fisadi puppet at work!!!
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Unafananisha vichuguu na Milima?
   
 8. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,141
  Trophy Points: 280
  Kwanza hivyo vyeti vya kuumwa vichunguzwe, kuna uwezekano kubwa vyote ni vya kughushi, hatujasikia wakiumwa, au wana maradhi mengine?

  Kukaidi mahakama waswekwe ndani tu.
   
 9. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Wewe bwabwaja tu.........hata hujui kuwa MKAPA na KIKWETE wanatakiwa mahakamani kujibu kesi ya MAHALU na hawataki kwenda
   
 10. moblaze

  moblaze JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  tanzania nakupenda...:A S-rose:
   
 11. Ole Tetian

  Ole Tetian Member

  #11
  Jun 1, 2011
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  And Vice Versa
   
 12. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Acha uongo, Lema amecharazwa marungu, amepigwa makofi na kisha kuswekwa ndani mbona hamku mwaga hiyo damu? Sana sana walipo wasweka ndani akina Ndesamburo ndio mkamwagwa damu ninyi wenyewe.
   
 13. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Cha Dr Slaa ni cha ukweli kabisa ukimuangalia tu na baadhi ya vitendo vyake utagundua huyu mzee ni mgonjwa kabisa.
   
 14. F

  FUSO JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,823
  Likes Received: 2,302
  Trophy Points: 280
  kumbambikizia kesi DR. ni kumpandisha juu tena juu zaidi. wote tunajua huyo ndiye Rais wetu mpendwa mkubali au mkatae - CCM kwisha kazii. Ref. Mwanahalisi Page ya kwanza. :biggrin1: magamba hayavuliki teh teh teh
   
 15. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #15
  Jun 1, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Maradhi yapi hayo? Au ni yale ambayo Tundu Lissu alitishia kuyataja hadharani wakati kampeni za mwaka jana kule Singida? Kwamba kuna wagombea urais wanaumwa magojwa mengi tu.
   
Loading...