Dk Slaa kuishikia bango kampuni ya Deep Green Bungeni kwa ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa kuishikia bango kampuni ya Deep Green Bungeni kwa ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Mar 16, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,417
  Likes Received: 81,463
  Trophy Points: 280
  Date::3/16/2009
  Dk Slaa kuishikia bango kampuni ya Deep Green Bungeni kwa ufisadi

  Na Mussa Juma, Moshi
  Mwananchi

  MBUNGE wa jimbo la Karatu, Dk Wilbrod Slaa amesema anakusudia kuwasilisha hoja binafsi kwenye mkutano ujao wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kulitaka kuunda kamati maalum ya kuichunguza kampuni ya Deep Green Finance Ltd ambayo inahusika na ufisadi wa zaidi ya Sh10 bilioni za umma.

  Mwaka juzi, Chadema ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikidai kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliilipa kampuni hiyo jumla ya Sh10,484,005.39/- katika mazingira yaliyojaa utata yaliyofanyika kati ya Agosti 1 na Desemba 10, 2005.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hakukuwepo na shughuli nyingine hadi Deep Green ilipoomba kutangazwa mufilisi.

  Juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kimanganuni, Kata ya Uru Mawela, Dk Slaa alidai kuwa kampuni hiyo kwa kushirikiana na benki moja ya Afrika Kusini iitwayo Ned Bank inatuhumiwa kuhusika kwenye ufisadi wa fedha hizo za umma na hivyo ni lazima uchunguzwe na bunge kwani kuna ushahidi mkubwa ambao umepatikana hivi sasa.

  Alisema hivi sasa serikali ya Afrika Kusini imeanza uchunguzi juu ya wahusika wa Ned Bank ambao walishirikiana na Deep Green kuchota fedha hizo kutoka BoT.

  “Nitapeleka tena hoja hii bungeni... kama ikikataliwa tutalipeleka suala hili kwa wananchi na kueleza kwa kina na wao watachukua hatua. Ni aibu hivi sasa serikali ya Afrika Kusini kuchunguza suala hili wakati Tanzania limeachwa,” alisema Dk Slaa.


  Alidai kampuni hiyo ilianzishwa Machi 18, 2004, ikiwa ni takriban mwaka mmoja kabla ya kuchota fedha hizo katika mazingira ya kutatanisha. Kwa mujibu wa Taarifa za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wakurugenzi wa Deep Green Finance walikuwa ni bwana Mark Ross Weston, ambaye ni raia wa New Zealand; Anton Taljaard wa Afrika Kusini na Rudolph van Schalkwyk pia wa Afrika Kusini.

  Alidai wote watatu ni wakazi wa Afrika Kusini na kwamba wanaonekana kuwa ni maafisa au wafanyakazi wa Nedbank Ltd ya Afrika Kusini.


  Dk Slaa alisema inashangaza kuwa kampuni hiyo iliruhusiwa kufungua na kuendesha akaunti bila ya kuingiza hata senti moja kwa zaidi ya mwaka mmoja kuanzia Mei 1, 2004 hadi Julai 31, 2005.

  Alisema uchunguzi uliofanywa na Chadema kwa kupitia nyaraka mbalimbali hususan rekodi za kibenki, ulibaini kuwa jumla ya shilingi 10,484,005,815.39 ziliingizwa katika akaunti ya Deep Green Finance katika kipindi cha miezi minne tu.

  “Fedha zote hizo ziliingizwa katika akaunti ya Deep Green Finance, katika kipindi cha miezi minne tu, kati ya tarehe 1 Agosti na 10 Disemba 2005," alidai.


  "Hiki kilikuwa ni kipindi cha mchakato wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika Desemba 14, 2005.

  “Ni muhimu kurudia kwamba kwa ushahidi huu wa nyaraka za kibenki, kampuni ya Deep Green Finance haikuwa na hata senti moja kabla ya tarehe 1 Agosti 2005 na wala haikupokea hata senti tano baada ya tarehe 10 Desemba 2005.’’

  Dk Slaa ambaye pia ni mbunge wa Chademaalisema chama hicho hakiwezi kukaa kimya wakati nchi inatafunwa na watu wachache huku maisha ya wananchi yakiendelea kuwa magumu.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama atafanikiwa. wanamtandao hawatakubali tena yatokee kama yale ya Richmond. Mfano mmoja ni suala la Masha na nitambulisho, Bunge limeshindwa kujadili.

  Deep Green ni suala la Masha pia na pia kuna tetesi kumhusisha Ridhwani Kikwete kwa namna kwamba alifaidika na ufisadi huo kwa namna moja au nyingine.

  Aidha kuna tetesi kuwa Club ya Yanga ilifaidika kutokana na kashfa hiyo, zaidi ya Sh 500 milioni zilitumika (kupitia Ridhwani) kufanya usajili kabambe wa club hiyo msimu huu. Manji yeye anawekwa kama "front man" tu na inaonekana kama analazimishwa vile -- kwani mguu moja ndani na mwingine nje.

  Lakini hili suala la Yanga ni nyeti sana sasa hivi na nina hakika wengi, hasa mashabiki wake, watakataa kata kata Club kuhusika, kwani wana uhakika ni fedha za mfadhili wao Manji. Uchunguzi wa kina unaweza kutoboa siri yote.
   
 3. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Unachosema ni sawa, lakini Wananchi tutajua kuwa Dk Slaa ametimiza wajibu wake na kazi itabakia kwetu wapiga kura.
   
Loading...