Dk. Slaa: Kikwete ahadaa wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa: Kikwete ahadaa wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 14, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Jabir Idrissa

  [​IMG]

  MUSWADA wa serikali wa “Sheria ya Marejeo ya Katiba” wa Mwaka 2011, umeelezwa kuwa ni kitanzi kwa wananchi.

  Unazuia wananchi kujadili mambo makuu yanayogusa maisha yao na mustakbali wa taifa.

  Kwa mfano, muswada unapendekeza kuzuia wananchi kujadili masuala ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na mahakama.
  Dk. Willibrod Slaa ameliambia gazeti hili kuwa hii ni hadaa. “Rais Kikwete alirukia hoja ya katiba kukidhi siasa. Kwa mwenendo huu wa serikali, katiba itakayopatikana itakuwa “chafu kuliko hii ya sasa.”

  Ameahidi chama chake kuhamasisha wananchi kuikataa katiba iliyopatikana kwa mfumo wa muswada huu.

  Maeneo hayo ambayo serikali haitaki yajadiliwe ndiyo yamesheheni kero ambazo zimekuwa vinywani mwa wananchi kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

  Wakati muungano umetajwa kutenguka, kuwa na mambo mengi ambayo hayakuwepo awali, kuegemea upande mmoja na kutoonekana muhimu kiuchumi kwa pande zote mbili; serikali inataka hoja hizo zizikwe.

  Mahakama ambazo zimekuwa chanzo cha malalamiko, tuhuma na shutuma kwa kutosimamia haki, muswada wa serikali unasema zisijadiliwe hata kidogo.
  Mambo mengine ambayo muswada wa serikali unataka yasijadiliwe katika utaratibu wake wa kupata maoni ya katiba ni uchaguzi, rais na bunge.

  Suala hili limeshangaza na kutatiza watu wengi: wataalam wa sheria na katiba, watetezi wa haki za binadamu, wanasiasa, wafanyakazi, wanafunzi na wakulima.
  Mshagao huu unatokana na muswada wa serikali kutokubali kuwa masuala makuu yanayoleta kutoelewana na hata vita katika mataifa mengi, na hasa Afrika, ni wizi wakati wa uchaguzi, udikiteta wa marais na udhaifu wa mabunge.

  Kuwazuia wananchi kujadili na kuchangia hoja kuu ambazo zinaleta mitafaruku na hata vita vya wenyewe kwa wenyewe, ni kukalia bomu litakalolipuka wakati wowote.
  Akijadili muswada wa serikali, jaji mkuu mstaafu Barnabas Samatta, alisema Jumamosi iliyopita kuwa pale ambapo haki hazisikiki, “…vimesikika risasi na mabomu.”

  Muswada wa serikali unaenda mbali na kukataza kujadili masuala ya ulinzi na utetezi wa haki za binadamu; misingi ya kidemorasi na umoja wa kitaifa.

  Katika hali ya kawaida, vile vyote ambavyo serikali inazuia wananchi kujadili, ndivyo vinaweka misingi ya utawala bora na ndio chemchemi ya makubaliano rasmi ya wananchi; yaani Katiba.

  Alikuwa wakili Mabere Marando, ambaye baada ya kujadili muswada huo alisema, “Kama hatuna fursa hata ya kujadili matendo ya tume, maana yake wale Watanzania tulio na nia njema na nchi hii, huu ndio wakati wa kuhamasishana kuanza mchakato wa kukataa sheria hii.”

  Mbali na mkakati wa serikali wa kuzuia wananchi kujadili mambo muhimu – kwa maana ya kuwachagulia wajadili nini na waache nini – muswada unazuia wananchi kuhoji utendaji wa tume ambayo rais ataunda kukusanya maoni ya katiba.
  Kwa mujibu wa muswada, atakayehoji kazi ya tume atashitakiwa na iwapo atathibikita kutenda kosa hilo, hatatozwa faini bali atatupwa jela kwa miaka miwili.
  Muswada pia unazuia vyama vya siasa kushiriki kuamsha wananchi na kuwapa ulelewa juu ya suala la Katiba; ingawa watendaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndio wanatajwa kusimamia jukumu la kuamsha wananchi.

  Hatua hii imekizana wengi hasa wanapokumbuka katika nchi jirani ya Kenya, waliona vyama vya siasa vikichukua jukumu kubwa la kuelimisha, kushawishi na hata kuchochea uelewa miongoni mwa wananchi kuhusu umuhimu wa kuwa na katiba yao.

  Kwa taratibu hizi, wananchi wamefungwa akili na midomo. Hawataweza kusema wanachotaka na wakikisema, watachukuliwa hatua; ama ya kushitakiwa au kauli zao kupuuzwa.

  Muswada wa serikali umechukua utaratibu uleule wa zamani wa kutunga katiba ambazo haziwahusishi wananchi moja kwa moja.

  Kwa ufupi serikali inakataa utaratibu wa kuwa na tume ambayo haikuchaguliwa na rais; inakataa mkutano wa katiba, bunge la katiba; bali inataka bunge lililopo ndio litageuzwa kuwa bunge maalum la kupitisha katiba.

  Muswada unaonyesha kuwa kitakachofanyika ni kutekeleza matakwa ya rais na serikali yake.

  Ni hapa ambapo Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Francis Kiwanga anasema, “Tumeporwa mamlaka ya kuandaa katiba sisi wenyewe.”

  Wananchi waliohudhuria kongamano la Katiba Mlimani, Dar es Salaam, walionekana kukubaliana kuwa serikali ya CCM, na hasa rais Kikwete, hana nia ya kuwa na Katiba mpya bali marekebisho ya hapa na pale katika katiba ya sasa.

  Profesa wa sheria, Issa Shivji alisema muswada wa serikali umejaa makosa hata ya lugha ya kikatiba, kimuundo na kimantiki.

  Alitaka serikali kuchukua maamuzi magumu kwa kukubali maoni na marekebisho yaliyofanywa na wadau, nia ikiwa ni kuja na katiba mpya badala ya viraka.
  Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema njia ya kupeleka muswada muhimu chini ya hati ya dharura ni uthibitisho tosha wa nia mbaya ya serikali ya CCM.

  Naye Peter Kisumo, mwenyekiti wa baraza la wadhamini wa CCM amesema, hakuna nafasi ya kukwepa kuwapatia wananchi katiba wanayoitaka.

  Amesema, “…suala hili liendeshwe vizuri katika namna ya kuongeza wigo wa watu wote katika maeneo yao kutoa maoni yao kwa uhuru; maana hapa hatuangalii maslahi ya vyama au chama cha siasa.”

  Anasema alipoanza kusikia harakati za CHADEMA kuhangaikia mabadiliko alidhani kwamba ni jambo lao peke yao kama chama, lakini baada ya kusikia maneno yao na mantiki yake, “…nikabaini kumbe wanazungumzia shauku ya wananchi kutaka mabadiliko.

  “Sasa hili ni jambo muhimu kuangaliwa kwa uzito wake,” amesema.
  Wakili wa Mahakama Kuu, Damas Ndumbaro, amesema mjini Dar es Salaam kuwa ni hatari kwa taifa “kwa serikali kubainisha mambo ambayo haitaki yajadiliwe.”
  Amesema uhuru wa kisiasa katika kupatikana katiba ya wananchi ni nyenzo muhimu isiyoepukika.
   
 2. koo

  koo JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kamwe dr asije akababaika au kusita kutueleza wananch lini anashauri nisiku muafaka kuingia mtaani kupinga mswada kama huu wala hatuna haja yakusubiri mpaka ifike hatua yakuundwa katiba tunapaswa kupinga pasipo kuchoka hata ikiwezekana tuanze leo dr usichoke kupigania nch yako tuko pamoja
   
 3. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kamwe wananchi tusikubali kuburuzwa na hoja za ki-CCM wakati huu wa marekebisho ya katiba. Aliyoyasema Dr. wa ukweli tutayazingatia na hatuko tayari kuwekewa katiba na Jaji Werema (kiraza wa CCM) na timu yake. Katiba yote lazima itoke kwa wananchi na mambo yote yawe ya muungano ama ya bara au visiwani pekee ni lazima yajadiliwe.
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Twende kazi!
   
 5. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Jumamosi ndio kazi inaanza.
   
 6. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Point taken na tutaifanyia kazi
   
 7. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kweli sikio la kufa halisikii dawa, hivi tunataka katiba iige mfumo wa vitabu vya Mungu kama Qurani na Bible? Haiwezekani mtu mwenye akili kuja na mswada butu kama ule! Eeeeeh Mungu labda katiba yetu ni mali ya serikali na si wananchi kama vilivyo vitabu vyako ambavyo wewe pekee ndiye uliwafunulia mitume wako kutuonya sisi! Yaani naanza kuona dalili za kiza kwa mbali na ile nuru niliyodhani kumbe ni hadaa!
   
Loading...