Dk. Slaa: JK ameliingiza taifa vitani

Status
Not open for further replies.
Kwa hiyo serikali imeshindwa kazi, CCM inabidi waingie wasaidie ......................!!!
 
Dr.Slaa yaani nyie mnawapiga mapanga raia na kuwamwagia tindikali muachwe tu.

Yani mmwagiane TINDIKALI wenyewe halafu mtuingize VITANI. Nyinyi teteeni tu hii kauli ya UCHOCHEZI ya Mh. RAIS, halafu atakaposimamishwa the HAGUE tuone kama mtaenda kumtetea.

 
Last edited by a moderator:
April 1994, Rwanda ilipatiwa mapanga kutoka China na hivyo Nterahamwe wakafanya kazi yao kama ilivyopangiliwa na wakuu wa dola. Hapa kwetu kilichotamkwa sina hakika kama ni maneno matupu au tayari mzigo upo njiani kutokea China kwa ajili ya utekelezaji wa kazi iliyoagizwa na Mkuu wa kaya na msaidizi wake.
 
Mbona wengi mnao-coment hii mnailenga CHADEMA tu wakati wamezungumza Lipumba, mbatia na Dr. Bashiru Ally? Kweli CHADEMA wanawapa headache CCM.

heading imebeba kila kitu hapa mkuu.slaa ni janga la nji hii
 
viongozi wa ccm na serikali yao tulionao zama hizi ni mumiani wao mauuaji utesaji na kushika damu za watu mikononi mwao jambo la kushangaza ni pale wanapomwaga vyeo kwa watuhumiwa wa maandaaji ya mauaji
 
Haya drama ingine kutoka kwa Dr.Slaa sasa sijui Bavicha watafuata yapi ya Lema au Dr.Slaa.

Sio kila kitu lazima ujibu au utetee, great thinker unachambua kilichosemwa kisha unakiboresha kwa manufaa yetu sote sio kwa ushabiki kama wa Simba na Yanga. Taifa hili liko mikononi mwetu na tunapaswa kuwaachia watoto wetu Taifa lenye heri.
Sasa kama viashiria vya machafuko hatuta vijadili kwa weledi tutayatafuta yanayotokea huko kwa wenzetu,ambako madhara yake yanawagusa zaidi raia wa kawaida na viongozi wanakuwa wamesha sepa zao na kuishi kwa ufahari na familia zao ughaibuni.
 
dr. Silaa ulivyosema nchi haitawalika ulikuwa unamaanisha nini?? Hwawa vijana unaowalisha viroba wanaanza kuwapiga watanzania wenzao, ujui wewe ndio wakushtakiwa???

Ukipanda mahindi , usitegemee kuvuna mihogo. CHADEMA kuweni wavumiivu tu kwa kuwa wakati mnayafanya haya mliona kama CCM wamelala.
 
Huyu rais mbona haelewiki, aliongeo hivyo kwenye kikao cha harusi au CC? Mbona siwaelewi! Habari ya bomu la Soweto, Arusha na shambulizi la Mwangosi, Iringa aliongelea? Yule kiongozi wa CDM aliyekatwa kichwa kule Arusha je? Mauaji ya wanaCUF Zanzibar chini ya mzee Mkapa je?

Kwanini amekuja na jamaa wa tindikali ambaye kimsingi alimwagiwa na wapambe wenzie baada ya kuwadhulumu mgawo ambao imekuwa kawaida kwa CCM kugawa fedha hovyo kila kunako uchaguzi? Kijana katobolewa macho, hilo pamoja na hayo mengine ni makosa makubwa sana kwani yananyima haki na uhuru wa watanzania wenzetu, kama amiri jeshi mkuu anatueleza nini juu ya wahusika? Maana kuwabambikia kesi watu haisaidii. Kuliondoa tatizo ni kutenda haki kisheria bila kujali nani kahusika. Kama ni wapinzani wawajibike kisheria na kama ni chama tawala pia wahusika wawajibike kisheria. Kujibu mapigo ni kutuletea utawala wa Mugabe ktk nchi yetu ambayo Mungu katupendelea kwa mengi isipo uongozi bora, unyenyekevu na unyonge kwa kila tuambiwalo na watala wasiotujali.
 
kama ccm ilituma kada ambaye kapewa unaibu waziri kwenda china kununua mabomu majambia mashoka bunduki na visu na wameshayajaribisha huko arusha mwenyekiti wa ccm anataka kutanua uwigo wa kuyatumia kauli yake na ya pinda ni ushahidi tosha wa yale wanayoyapanga kwenye vikao vyao vya siri kwa jinsi ya kuendeleza nauaji
 
Acha kumtia maneno Jk wewe. Kakutuma? Hakusema ulivyosema wewe punda. Kasema wazi ccm wajibu mapigo. Kwa sababu wapinzani wao wanavurugu. Katoa mfano wa tindikali na bisibisi. Hizo ni hoja za sera au ni vurugu ? Wewe mburula?
 

Lazima watu tuzichape ili CHADEMA waufyate
 
Haya drama ingine kutoka kwa Dr.Slaa sasa sijui Bavicha watafuata yapi ya Lema au Dr.Slaa.
Hongera wewe unaeishi angani unaefurahia uchochezi wa CHAMA TAWALA.Kikiwaka bora hata mie nnaeishi mpakani kuliko wewe uliye kinondoni.KUNA SIKU MTATAKA MSAADA WA AKINA LEMA na AKINA SLAA ila wakati huo hawapatikani.
 
Acha ujinga wewe, hakuna raia mwema anayeua wananchi kwenye chaguzi.

Wewe unaushahidi kuwa mimi nahusika kwenye mauaji ya wananchi kwenye CHAGUZI? Hao wauwaji mbona wanaachiwa na POLISI tena MAHAKAMANI? Unamkumbuka Marehemu Msafiri Mbwambo aliyekuwa Mwenyekiti wa CDM wa kata ya USA-River huku ARUSHA? Kesi ya watesi na wauwaji wake imeishia wapi pamoja na wahusika kukamatwa na kutoa vidhibitisho vya SILAHA walizotumia? Nyie watu mmepandikiziwa chuki dhidi yetu, na mnachukulia kishabiki kutuonea ndani ya nchi yetu. Usiwe mshabiki wa kitoto.....

View attachment 139695
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…