Dk Slaa awatimua viongozi 33 Sengerema

BigMan

JF-Expert Member
Feb 19, 2007
1,096
135
baada ya chadema kushindwa kuvuna wanachama wa ccm wilayani sengerema,katibu mkuu wa chadema dk wilbroad slaa amewatimua viongozi 33 na kuvunja kamati ya utendaji ya chama hicho wilayani sengerema.

viongozi hao walitimuliwa usiku wa manane kwenye kikao cha ndani na hawakutakiwa kugombea tena uongozi ndani ya chadema katika uchaguzi wa kuziba nafasi zao na badala yake aliyejiunga na chama hicho ni aliyekuwa diwani wa kata ya ibisabageni hamisi tabasamu

viongozi hao wamefukuzwa kwa kushindwa kuwashawishi wananchi wengi wakiwemo wanaccm kujitokeza katika mkutano wa dk slaa uliofanyika jumamosi iliyopita mjini humo.

miongoni mwa waliotimuliwa yumo said shabani ambaye ni mwenyekiti wa jimbo la sengerema,rafiki rufunga ambaye ni katibu na manyama mayeye ambaye ni katibu mwenezi.

katibu wa chadema mkoa wa mwanza wilson mushumbushi aliyedaiwa kuhudhuria kikao hicho alipotakiwa kuzungumzi sakata hilo alidai liko juu ya uwezo wake na kuthibitisha kutimuliwa kwa viongozi hao wa wilaya.

CHANZO: Gazeti la Uhuru
 
baada ya chadema kushindwa kuvuna wanachama wa ccm wilayani sengerema,katibu mkuu wa chadema dk wilbroad slaa amewatimua viongozi 33 na kuvunja kamati ya utendaji ya chama hicho wilayani sengerema.

viongozi hao walitimuliwa usiku wa manane kwenye kikao cha ndani na hawakutakiwa kugombea tena uongozi ndani ya chadema katika uchaguzi wa kuziba nafasi zao na badala yake aliyejiunga na chama hicho ni aliyekuwa diwani wa kata ya ibisabageni hamisi tabasamu

viongozi hao wamefukuzwa kwa kushindwa kuwashawishi wananchi wengi wakiwemo wanaccm kujitokeza katika mkutano wa dk slaa uliofanyika jumamosi iliyopita mjini humo.

miongoni mwa waliotimuliwa yumo said shabani ambaye ni mwenyekiti wa jimbo la sengerema,rafiki rufunga ambaye ni katibu na manyama mayeye ambaye ni katibu mwenezi.

katibu wa chadema mkoa wa mwanza wilson mushumbushi aliyedaiwa kuhudhuria kikao hicho alipotakiwa kuzungumzi sakata hilo alidai liko juu ya uwezo wake na kuthibitisha kutimuliwa kwa viongozi hao wa wilaya

Tabasamu amekuwaje? sijakusoma mkuu!
 
Ahsante Mungu wa israel kwani hiyo ndo" operesheni wajibikaji" na bado tukichukua nchi kwa wale wote watendaji legelege ndo mtahesabu nyota tu, kwani uwajibikaji ni lazima uanzie kwenye chama na baada ya hapo baada ya chama kushika nchi basi ndio mwendo mdundo.
Big up Rasis wangu slaa.
Mungu wa israel akulinde. Amen
 
Hakuna kulea uovu hata kidogo,ni mwendo mdundo na atakaye shindwa kuendana na hiyo supersonic speed apishe ili wengine wakalie usukani.Umagambagamba hatuuhitaji.Ukivaa combart ni kwamba hautakiwa tena kuwa legelege ni kukaza kweli.
 
baada ya kukosa mavuno aliyotegemea badala yake aliyejiunga alikuwa ni tabasamu tu
Uongo mwingine wala haufai kwani tulijionea Live ITV watu wanarudisha kadi za CCM wengine wanavua Tshirt, Kofia na Kanga za magamba. Labda kama Sengerema ziko mbili, na hata Mwenyekiti wa Halmashauri Mathew Lubongeja amemlaumu Tabasamu na diwani wa Lugata Bw Tizeba kwa kuhamia CDM sasa wewe unasema hakuvuna alivyotemea, umeingia moyoni kwa Dr Slaa na kujua alitegemea nini? Uongozi wa CDM Sengerema ulikuwa dhaifu sana, Ngeleja alikuwa anawanunua anavyotaka yeye so kuwamwaga naunga mkono
 
Acha Bangi wewe,
Au unataka tumwage mboga????

Unaweza kueleza kwa nini mliwafungia ndani wale wengine?????????????
Mtakoma Lema yuko kazini
Nipe masaa 48 utapata jibu.
 
Hii habari imeandikwa na "gazeti" moja tu leo nalo sio jingine bali gazeti la UHURU. Changanya na zako!
 
Hao jamaa wa sengerema wamefukuzwa kwenye uongozi kwa sababu ya kutoandaa mazingira ya Mkutano. watu walikuwa wengi lakini wao walishindwa kukodi vifaa vya kufanyia mkutano zikiwepo spika na mic. wakawa wanategemea kutumia spika zilizokuwa kwenye gari iliyokuwa kwenye msafara wa dr.slaa ambayo ilikuwa haikidhi haja ukilinganisha na watu walio hudhuria. hiyo ilichukuliwa na dr slaa kama hujuma.
 
Unadhani wataandika nini maana ni aibu, wanajaribu kama inalipa kwa kuandika hivyo. Pole mwe!!!!!
 
Kwa macho yangu nimeisoma hii habari kwenye gazeti la UHURU la leo, mweka uz sema source- gazeti la uhuru plz.
 
chanzo cha habari hiyo ni gazeti la UHURU ambalo ni mali ya CCM unategemea waandike nini
 
Kwa macho yangu nimeisoma hii habari kwenye gazeti la UHURU la leo, mweka uz sema source- gazeti la uhuru plz.

hata mimi hili gazeti nimeliona leo lakini kinacho nifanya nilidharau gazeti la Uhuru ni ile taarifa ya habari ya ITV jana.
Nakushauri chagua magazeti ya kutoa fedha zako.
 
Jamani: Huko CHADEMA demokrasia ni adimu sana! These decisions will backfire in future, let's wait and see!
Chama sio kama serikali; ndio maana Mkapa alikuwa Rais Mzuri sana lakini alikuwa mwenyekiti wa chama mbaya! Na JK ni rais mbaya lakini mwenyekiti wa chama mzuri!
 
Back
Top Bottom