KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbroad Slaa amewataka viongozi wa dini nchini kufanya utafiti kabla ya kutoa matamko yao katika vyombo vya habari.Kauli hiyo ya Dk Slaa imekuja siku moja baada ya Sheikh Mkuu wa Tanzania , Mufti Issa bin Shaaban Simba kukishutumu chama hicho kwamba maandamano yake kinayofanya hivi sasa yana lengo la kuvuruga amani ya nchi.
Katibu Mkuu huyo wa Chadema alisema ameshangazwa na kauli iliyotolewa na Mufti Simba kuwa chama chake kina lengo la kuvuruga amani nchini.Nimeshangazwa sana na kauli ya Sheikh Mkuu, Mufti Simba aliyoitoa kwa vyombo vya habari.
Kimsingi kama alitaka kujua undani wa maandamano yetu angetuuliza kuliko kutoa tamko bila kujua hata undani wa Chadema, alisema na kuongeza kuwa baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakitoa tamko bila ya kufanyia utafiti jambo ambalo linawafanya watoe maelezo yasiyo na ukweli na yanayolenga kuwapotosha na kuchochea chuki kwa wafuasi wake.Dk Slaa alisema Chadema inajua inachokifanya, hivyo kama mtu anahitaji kujua madhumuni ya maandamano yao ni vyema akawauliza ili
kitoe ufafanuzi kwa kuwa kila jambo liko wazi kwa maslahi ya wananchi wenyewe.Sioni haja ya kulumbana na kujibizana kila kukicha kupitia vyombo vya habari. Kama wana hoja ya msingi wailete sisi tutaijibu kwa hoja siyo kuongea mambo kwa mtazamo na propaganda za kisiasa. Unapozungumza ni lazima kuwe na utaratibu wa kutafiti unachokizungumza, alisema Dk Slaa.
Aliwataka viongozi wa dini kuhudhuria mikutano ya chama hicho ili kusikia na kujua kinachozungumzwa na Chadema kuliko kusubiri kusimuliwa na watu na kisha kuyaamini maneno yao.Alisema amelazimika kumjibu Mufti Simba kwa kuwa amesikitishwa na kauli hiyo ambayo alisema badala ya kuwasaidia Watanzania, inachochea chuki na kuruhusu ufisadi kuendelea.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam juzi, Mufti Simba alisema: Wanasiasa wanataka kuivuruga nchi kwa visingizio kuwa wanataka kuilinda amani, hivyo Waislamu tumeamua kuvunja ukimya uliodumu kwa muda mrefu na kuamua kukekemea vitendo hivyo.Mjadala wa uhalali wa mikutano na maandamano ya Chadema uliibuliwa na Rais Jakaya Kikwete alipolihutubia taifa kupitia redio na televisheni mwishoni mwa Februari kwamba chama hicho cha upinzani kina lengo la kuleta machafuko nchini.
Kauli hiyo ilifuatiwa na onyo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira kuwa Chadema kisije kuilaumu Serikali itakapokosa uvumilivu na kuanza kutumia dola kukishughulikia.Wakatihuo huo; Dk Slaa amesema ziara zinazofanywa na Rais Jakaya Kikwete katika wizara mbalimbali ni matunda ya maandamano ya chama hicho katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Alisema Serikali imeanza kutekeleza madai mengi ambayo Chadema ilitaka iyafanyie kazi ndani ya siku tisa. Hata hivyo, alisema chama hicho kitaendelea kutia shinikizo hadi mambo yote yatakapokamilishwa.Hayo ni matunda ya maandamano yetu japo utekelezaji wake hauridhishi kwa kiwango tulichotaka.
Lakini imedhihirika kwamba mambo hayo yanaweza kupatiwa ufumbuzi. Inashangaza kuona wengine wanayaita maandamano kuwa ni ya kuvuruga amani, alisema.Alisema kuwa matunda mengine ya maandamano ya Chadema yaliyofanyika mkoani Mwanza ni tamko la Rais la kupunguza bei ya sukari kutoka Sh2,200 hadi Sh1,700.Rais Jakaya Kikwete anatembelea wizara mbalimbali kukagua utekelezaji wa maagizo ya yake.